Senzo Masingiza na Manara hakika mnalichafua soka la Tanzania

Senzo Masingiza na Manara hakika mnalichafua soka la Tanzania

Kwa ninachokiona mimi , simba na Yanga siyo watani tena. Kwasasa ni maadui. Hii imetokana na viongozi wa hivi vilabu kuwa na kauli za ovyo tena za kichonganishi

Manara ni tatizo kwa mpira wa Tz. Huyu mtu asipoonywa ataligawa taifa kwa itikadi za usimba na uyanga na ipo siku atasababisha maafa kwa tabia zake za kinafiki .

Senzo hana cha kupoteza. Ipo siku atarejea kwao huku akiacha ametugawa.
 
Jambo muhimu wanalopaswa kuelewa Makolo ni kuwa msimu huu kombe lao litakuwa la Mapinduzi pekee
Mkuu Kwani tatizo liko wapi? Mmekaa miaka 4 bila hata kikombe cha kahawa. Je , mlikufa kwasababu ya kukosa kombe? Mpira ndivyo ulivyo. Huwezi kuwa bora muda wote. Na lazima tukubaliane na hiyo hali.
 
Yani huu mpira unafanya watu timamu sasa kuwa kama vichaa, immigration rules zipi ambazo amevunja Senzo?

Morrison haruhusiwi kuingia Afrika kusini kwa sababu ambazo ziko wazi na ni criminal pia.
Sidhani kama mleta mada kuna sehemu amehusisha matatizo ya morisson na senzo.
 
Mtalii Mnigeria baada ya kutoa tuhuma ya kubakwa kwenye hotel, serikali imetoa tamko. Manara , Abdi Banda wanaituhumu simba kwamba wako tayari kuhatarisha usalama wa wapinzani wao ili kupata ushindi,serikali kimya wakati wanajua kazi ya kulinda usalama wa mtu yoyote aliyeko Tanzania ni wao.

Simba ifute hayo maneno visit Tanzania wayaandike kwenye jezi za mautopolo walio wasafi.
 
Mtalii Mnigeria baada ya kutoa tuhuma ya kubakwa kwenye hotel, serikali imetoa tamko. Manara , Abdi Banda wanaituhumu simba kwamba wako tayari kuhatarisha usalama wa wapinzani wao ili kupata ushindi,serikali kimya wakati wanajua kazi ya kulinda usalama wa mtu yoyote aliyeko Tanzania ni wao.

Simba ifute hayo maneno visit Tanzania wayaandike kwenye jezi za mautopolo walio wasafi.
Yani serikali iingilie siasa za mpira? Wewe utakuwa haupo serious.
 
Yani unamuogopa Abdi Banda aliyesema ukweli unawasingia Senzo na Manara.
Akili ndogo mnadhani Ni SIMBA tu I anaharibiwa sifa, kumbe Ni timu zote za Tanzania, pamoja na Utopolo itakayoenda kucheza mechi 2 za klabu bingwa mwakani na kurudi.
 
Akili ndogo mnadhani Ni SIMBA tu I anaharibiwa sifa, kumbe Ni timu zote za Tanzania, pamoja na Utopolo itakayoenda kucheza mechi 2 za klabu bingwa mwakani na kurudi.
This is shabiki Wa simba😅😅line ya tatu imenichekesha.😅
 
Hawa hapa watu wako

4EE48A86-89F1-4915-9EE1-88DED2837069.jpeg
 
Hii nchi imejengwa Kwa misingi ya chuki unafiki na kujipendekeza.
Watu wanaishi Kwa kuombeana mabaya na kulogana TU.

Kosa kubwa sana walilolifanya waasisi wa nchi hii ni kujenga Taifa lisilo na tamaduni Wala miiko iliyowekwa Kikatiba.

Ndio maana watu wanaamini sana katika kufanya figisu ili wapate mafanikio. Watanzania wengi wanaamini kuwa huwezi kufanikiwa Kwa kusimama katika Haki na kweli. Hata biashara watu wanaamini kuwa huwezi kufanikiwa bila kutumia uchawi au biashara HARAMU na kukwepa Kodi na biashara za magendo. Hili limejengeka sana vichwani mwa watu. Hata walioajiriwa wanaamini kuwa hakuna mafanikio bila ujanja ujanja na wizi maofisini. Hali hii imegeuka kuwa ndiyo desturi ya watanzania. Serikali tangu uhuru imechangia sana kujenga Taifa ovu na ndilo linalorithishwa Kwa vizazi vijavyo. Mwaka 2020 Kuna watu walikua wanapora mpaka watu fomu za uchaguzi ili washinde wao kirahisi. Ni nchi ya hila na figisu. Sasa kila mmoja haamini katika kushinda Kwa uhalali. Ndio maana wanawaambiwa Wageni Mila zao na desturi za watanzania ni udanganyifu na figisu hata kama Simba wanaupiga mwingi lakini Kuna desturi za watanzania zimeathiri akili za watu.
Chanzo cha yote ni CCM
 
Kwani mambo ya kuchaguliana marafiki yameanza lini? Yaani serikali ianze kuhangaika na maoni yatolewayo michezoni!
 
Kwani mambo ya kuchaguliana marafiki yameanza lini? Yaani serikali ianze kuhangaika na maoni yatolewayo michezoni!
Ndo nashangaa mkuu.....yaani tuanze mambo NATO na urusi[emoji23][emoji23] kuchaguliana ma friends
 
Wote hao wamefanya kazi Simba na kwa muda mrefu, pengine walikuwa sehemu ya utekelezaji wa hayo yanayolalamikiwa.
 
O
Nilikuwa nafuatilia interview ya kocha wa Orlando Pirates kabla ya mchezo na hata baada ya mchezo,

Nilichogundua ni kuwa Kuna watu wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kwa wageni kuhusu Simba. Taarifa hizo zimekuwa zikipandikiza chuki kwa wageni kwa kuamini kuwa kucheza na Simba nyumbani ni vita.

Mfano interview ya kwanza ya kocha wa Orlando pirates alianza kuilaumu Simba bila ya kuwa na sababu za mashiko eti kwamba hawakupewa escort ya kutosha "mambo ya hovyo kabisa".

Orlando walikuja na kila kitu chao kuanzia msosi na kila kitu haikutosha wakakataa kupanda bus waliloandaliwa na Simba, baada ya mchezo kocha pia anarudi akisema Simba haikustahili kushinda kwa sababu walipewa penati ya bure na wao wakanyimwa penati halali.

Haya yote yanaonesha kuwa kuna watu nyuma ambao kazi yao ni kutoa taarifa za uongo na kupandikiza chuki kwa wageni kwamba Ili Simba ishinde basi inahitaji kufanya figisu na hili linakaa vichwani kwa wageni ndo maana unakuta wageni wanakuwa wanalaumu kwa kila kitu wakiamini ni zile figisu walizoambiwa na manara pamoja na senzo.

Manara kama alithubutu kuongea ujinga wa kuwaambia Asec Mimosas kwamba wasafishe vyumba vya kubadilishia nguo kwa maana Simba wamepuliza dawa atashindwa vipi kuzungumza haya ninayoyasema na ukizingatia yeye alikuwepo Simba msimu ulopita, hii inawafanya wageni wamuamini kwa asilimia zote.

Hii tabia inalishusha sana soka la bongo kwa kuonekana ni la kibabaishaji.

Pua senzo!, Pua manara!, Pua!, Pua kabisa!!

Orlando walichemsha uwanjani. Takwimu za mchezo zinaonesha kuwa Simba ilikuwa juu kwa karibuni vigezo vyote vya kitakwimu! Ndio maana Simba ikaingiza wachezaji 5 kwenye timu ya wiki kwenye confederation cup! Kwenye timu ya wiki hata ukiwatafuta Orlando Pirates kwa tochi hutawaona!
 
Back
Top Bottom