Septemba 1973 yalifanyika maandamano makubwa kupinga mavazi yasiyo na heshima! CCM walianza zamani kupoteza muda kwenye mambo ya ajabu

Septemba 1973 yalifanyika maandamano makubwa kupinga mavazi yasiyo na heshima! CCM walianza zamani kupoteza muda kwenye mambo ya ajabu

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Yaani kutoka TANU mpaka kufikia CCM bado wameendeleza kuweka nguvu kwenye mambo yasiyo na maana na kuacha vitu ambayo vinadidimiza taifa kwenye maendeleo ya sekta mbalimbali.

Yaani watu na akili zao walitoka barabarani kupinga vimini, wavaa vikaushi sijui na zile suruali skini za wanaume :BearLaugh::BearLaugh::KEKLaugh:.

Kama sasa hivi tu wapuuzi wako bizd na makongamano na maandamano ya kumtukuza mama:BearLaugh::BearLaugh: khaaah... wenzetu wakiwa bize kuunda magari na simu,kufungua maviwanda ya hatari sisi tuko bize kupinga vini na skini jinzi🤦‍♀️🤦‍♀️.

====


Mnamo siku ya Ijumaa Septemba 7, 1973 maandamano makubwa sana ya wananchi yalilifanyika jijini Dar es Salaam kuunga mkono kampeni rasmi dhidi ya mavazi yasiyofaa.

Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Rashidi Mfaume Kawawa, maafisa wa serikali, Vijana wa TANU na mashirika mbalimbali walihudhuria kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mwisho wa maandamano hayo katika makao makuu ya TANU Mtaa wa Lumumba.

Serikali ikaweka Oktoba 1 kama tarehe ya mwisho kwa kuanza msako huo, lakini tayari Mkoa wa Mwanza ulikuwa umeanza kuchukua hatua.

Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) uliunga mkono kampeni hii na kutoa mihadhara mashuleni kuhusu mavazi yanayofaa.

Hii inakumbusha enzi zile za siasa za ujamaa zenye nidhamu kali, ambapo mavazi yasiyofaa yalionekana kama ishara ya mmomonyoko wa maadili na utamaduni wa Kitanzania.

Kampeni hii ya 1973 ilikuwa sehemu ya msisitizo wa utawala wa Mwalimu Nyerere juu ya maadili, utu na nidhamu katika jamii.

Hata hivyo, leo hii, kampeni kama hii ingekumbwa na upinzani mkubwa kutoka kwa vijana wa kizazi cha sasa ambao wanathamini uhuru wa mavazi na kujieleza.
 
Back
Top Bottom