Septemba 5, Siku ya Kimataifa ya Hisani Duniani

Septemba 5, Siku ya Kimataifa ya Hisani Duniani

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Siku ya Kimataifa ya Hisani inaadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Septemba na iliidhinishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo 2012

Siku hii ilianzishwa kwa madhumuni ya kuhamasisha watu, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wadau kote ulimwenguni kusaidia wengine kupitia shughuli za kujitolea na za uhisani

Siku hii pia ni kumbukumbu ya Mama Teresa wa Calcutta ambaye alipokea Tuzo ya Amani ya Nobel, 1979 kwa kujitoa kwa ajili ya wasiojiweza

Kwa nini hisani ni muhimu katika jamii zetu
Hisani, kama vile dhana za kujitolea na ufadhili, hupelekea uhusiano halisi wa kijamii na huchangia katika uundaji wa jamii jumuishi na stahimilivu

Misaada hupunguza athari mbaya zaidi za majanga ya kibinadamu, kuboresha huduma za umma zikiwemo afya, elimu, makazi na ulinzi wa watoto

Pia inawezesha utetezi wa haki za waliotengwa na wasiojiweza, kueneza ujumbe wa ubinadamu katika maeneo yenye migogoro pia kukuza maendeleo ya utamaduni, sayansi, michezo, na ulinzi wa urithi wa kitamaduni na asili

Chanzo: Umoja Wa Mataifa
 
Sawa tuendelee kuwakaribisha wahisani sehemu zote zenye uhitaji wa hisani.
 
Back
Top Bottom