Patrick Girigo
Member
- May 30, 2020
- 68
- 108
Ilikuwa majira ya saa 7 mchana, Kanzda ya KATI nikiwa napata chakula cha Mchana na wazee wawili ambao kwa sasa wana miaka 60, wamestaafu KAZI ya serikali, mmoja alikuwa Mchumi na mwenzake alikuwa Mkaguzi wa Ndani; Tukiwa tunafurahia coke baridi, ghafla nikaangalia fb, page ya ITV nikaona habari mbaya kabisa kuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amepigwa risasi Dodoma, nilipowaambia wazee wangu walishituka sana na tulishangaa sana; Kila mmoja alishikwa na butwaa na watu wote ambao walikuwepo hapo walishikwa na hofu kama baridi kali sana. Tuliporudi baada ya chakula,hatukuwezi kuendelea na majukumu yetu kama kawaida isipokuwa tulijikusanya, tukiwa tunashangaa aina ya tukio baya namna hiyo, ghafla wale wazee 2 wakaniambia kuwa tayari jamaa amekata moto.
Nikiwa na ujasri wa Kiroho kabisa, niliwaambia kuwa kamwe hawezi kufa, Mungu atampigania. Ilipofika saa 11 jioni wakati tunaagana kila mmoja kwenda kwao, waliniambia tena kuwa huko Mwanza wametangaza kuwa jamaa tayari hatunaye tena, Nilirudia kuwa kamwe hawezi kufa, Mungua atampigania, hadi kesho yake tulipoonana tena, tulimshukru na kumtukuza Mungu kwa namna alivyompigania.
Miaka 4 baadaye (2021), habari hiyo mbaya imekufa na imepotea kabisa,watu wote wanaimba sifa na utukufu kwa Mungu kwa muujiza wake alioutenda, habari hii inafanana na habari njema za Nabii EZRA 8:1- 9 kuhusu kelele za shangwe kwa taifa la Israel lilipoachiliwa kutoka katika utumwa wa Babeli kurudi Israel kujenga madhabahu ya kumwabudu Mungu wa kweli.
#NINI TUNATAKIWA KUFANYA SASA?
Kwa mujibu wa tamko la dunia kuhusu HAKI za binadamu la 1948 kwamba binadamu wote ni sawa na wameumbwa sawa bila kujali aina yeyoye ya ubaguzi au tofauti ziwe za kiuchumi, Kisiasa, Kijamii au Kiimani. Mwaka 1977 na 1984 Waasisi wa Taifa la Tanzania waliandika katika Katiba yetu ibara ya 12 kuwa binadamu wote ni sawa mbele ya sheria na ibara ya 13 inakazia kuwa watu ni sawa hata kama mtu anatuhumiwa kwa makosa ya jinai,hatakiwi kutendewa kama mhalifu na ibara ndogo ya 5 inakaza kabisa aina zozote za ubaguzi. Huu ndio mtizamo wa Kikatiba na ndio utamaduni wa Tanzania ya Mwl Nyerere, Mwinyi, Mkapa,JK nk. Hatutakiwa kabisa kuruhusu utamaduni mpya wenye ubaguzi, unyanyasaji au kutendeana kama mhalifu. Vitabu vyetu vyote vya sheria vinakataza kabisa shambulio lolote na kwa mujibu wa sheria ya Kanuni ya adhabu cap 6 .(R.E 2002) ni Kosa kubwa kumshambulia mtu yeyote kwa sababu yeyote
Kitendo kilichotokea 7/9/2017 kinatakiwa kukemewa na kila mtanzania bila kujali nafasi ya mtu au elimu linapokuja suala la uhai na usawa. Ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa raia wake wanakuwa salama na kuwakamata wote wanaotenda makosa yote ya Jinai na kufikiwa katika Vyombo vya sheria na HAKI ionekane kuwa imetendeka. Bila kujali TUKIO hilo lilitekelezwa kwa makusudi ya Kisiasa au ya kigaidi, ni lazima wahusika watafutwe ili isionekane kuwa ukiwa kwenye madaraka, unaweza kuamua nani aishi leo au nani aishi kesho. Mwaka 1995, Mtoto wa Mwl Nyerere ambaye kwa sasa anahudumu kama RC Manyara, aligombea Ubunge wa Arusha Mjini na akashinda kwa NCCR Mageuzi wakati Baba yake alikuwa Rais miaka 24 na alimpigia kampeni Benjamini Mkapa kuwa Rais; wazee wetu walikuwa na ndoto ya kujenga Nchi nzuri inayovumilia tofauti zetu za Kisiasa,Kidini,kijamii au kiitikadi.
Ni muhimu kuhakikisha kuwa Nchi hii inakuwa salama kwa watu wote bila kujali background zao au mrengo wowote wa Kisiasa au wa Kidini.
Our natural rights protect our ability to pursue our natural inclinations free from government interference: To live, to love, to acquire property, to be productive, to be left alone. If a human or if a government transgresses those rights, then it is violating those rules of social interaction, and hence the Natural Law. Stated simply, because natural rights protect our human nature and are based on the eternal law, they are described as self-evident and inalienable. Humans have a natural inclination to preserve their own lives: Although we can certainly try to understand precisely why it is that humans try to preserve their lives, it can stand by itself and needs no further explanation or rationalization.