September AMATB - Niulize Chochote Kuhusu Tehama na Biashara

September AMATB - Niulize Chochote Kuhusu Tehama na Biashara

Halafu mkuu ni kwa namna gani tunaweza kuishauri serikali kuondoa sheria zinazozuia ubunifu mfano sheria inayowataka bloggers &youtubers kulipa $500 ya usajili kila mwaka
 
Mkuu nini mawazo yako kuhusu uwekezaji kwenye cryptocurrencies kwa sasa na baadaye

Je unaweza kuwashauri watu kuwekeza huko fedha zao
Kuhusu CC siwashauri watu kuwekeza fedha ambazo wanatarajia ziwasaidie. Kama una fedha ambazo hata ukipoteza hakuna tatizo basi weka huko.

Kuna risk nyingi sana lakini mbili ni kubwa.
1. Mara zote system nzima inategemea mtu au kikundi cha watu (you are at mercy of one or few elites). Mfano mpaka leo wangapi wanajua nani ni founder wa bitcoin na kwamba hakuna siku wataamka na kukuta system nzima ime corrupt? Wengi wataleta utetezi mzuri lakini hakuna anayejua Achilles heel ya hii system asilimia 100. Pia kuna fraud ilishafanyika niliisoma somewhere sipakumbuki but ilinipa picha kubwa juu ya huu uwekezaji wenye mashaka.

2. Hakuna regulator wa CC. Kwa asili yake CC ni non regulate-able. Facebook walijaribu kuja na Libra currency ila naona kama wamekwama. Financial systems ambazo haziko regulated ni hatari kwa fedha zako.

So long story, usiwekeze fedha zako kama zitakuuma zikipotea. Ni kamari!
 
Halafu mkuu ni kwa namna gani tunaweza kuishauri serikali kuondoa sheria zinazozuia ubunifu mfano sheria inayowataka bloggers &youtubers kulipa $500 ya usajili kila mwaka
Kwa maoni yangu tatizo la kwanza sio serikali. Serikaliinakuja tu na miswada inayodhani itasaidia kama msimamizi na mtendaji wa mambo mbali mbali katika nchi. Tatizo lipo kwa wawakilishi wetu, yaani wabunge. Wao wana uwezo mkubwa sana wa kutuletea sheria bora na kuhakikisha sheria inakuwa bora kabla hawajaipitisha. Since huu ni mwaka wa uchaguzi tuna nafasi ya kuwahoji wabunge wetu juu ya hili.

Pili tujitahidi kuchagua bila mihemko ya kisiasa na kivyama, watu ambao watasimamia maslahi yetu.

Lakini la tatu ambalo linaweza kusaidia ni kusubiri Bunge lijalo na kuhamasishana kila watu kwa jimbo lao wawasialiane na wabunge wao kuhakikisha Bunge linatafuta namna ya kufanya review ya hizi sheria na kuziboresha ili zitusaidie kuishi vizuri badala ya kuwa kikwazo kwa maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla.

Kifupi ni kuwa inatubidi kutafuta njia halali kisheria na kiutaratibu kuhakikisha sheria zisizo na msaada kwa nchi na wananchi wake zinarekebishwa. Naamini linawezekana ila litahitaji muda na uhusiano mzuri kati ya wananchi, wawakilishi wetu bungeni na serikali.
 
Back
Top Bottom