Sera iliyoboreshwa na mtaala mpya ni Danganya toto ya kisiasa huko mashuleni hakuna kinachoendelea

Mama Naa

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2020
Posts
453
Reaction score
1,104
Amani iwe juu yenu...

Tanzania ilianza mchakato wa sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023, mwaka 2022. Mpaka sasa Kwa shule za msingi utekelezaji ulishaanza na wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la nne wanaendelea nao.

Kwa shule za sekondari mtaala huo umeanza mwaka huu 2025 Kwa kidato Cha kwanza. Na kidato Cha tano utaendelea mwaka huu 2025 baada ya kusitishwa mwaka Jana.

Sasa yanayoendelea mashuleni Kwa kweli yanasikitisha na kutia uchungu sana.

Yaani serikali mlichokifanya ni kubadilisha vitabu na kupunguza au kuhamisha mada pia kuwaongezea walimu kazi za kuchakata hivyo vitabu vyenu.

Huko shule za msingi hakuna kipya chochote ni mwendo wa content based curriculum sasa huo ufundi, ushonaji, uashi sijui umakenikia uko wapi ????!!!

Sekondari nako hadi sasa vitabu hakuna, business studies, Computer studies, Science subjects and Mathematics HAKUNA WALIMU!!!! I WONDER!!

Hivi mlikuwa na haraka Gani ?? haraka ya kula posho?? au haraka ya kuwahi uchaguzi 2025 ili ndio iwe ajenda yenu!!??

Hivi Mkenda !! zile semina ulizowapa mawaziri, wabunge, viongozi wa dini, wanasiasa,, wakurugenzi na wakuu wa mikoa na wilaya,,...!! Kwa nini hukuzielekeza Kwa WALIMU?? ambao ndio watekelezaji wakubwa wa huo mtaala mpya!

KWALI SISI WAAFRIKA HATUNA AKILI..!

Kuwapa semina wabunge kuwaacha walimu !! ndio janga linaloenda kuiua hiyo sera yenu, HAKUNA KIPYA tuliona 2005, baadae 2010 na 2015 mlipokuja na mambo ya DISTINCTION....

Ndugu watanzania hii sera ni Kwa ajili ya watoto wetu maskini, wakwao wapo FEXA
tuifuatilie na kuipigia kelele Kwa sababu mwisho wa siku ni watoto wetu wanaoumia sio wakwao.

Kwanza wameleta sera iliyoboreshwa na mitaala mipya wakati mpaka sasa Kuna walimu bado wapo CONTENT BASED CURRICULUM hawajafika hata COMPETENCE BASED CURRICULUM.

NI MAJANGA KWA KWELI...
 
Mabadiliko yanaanza taratibu mtaala wenyewe ndio kwanza una mwezi mmoja kuna usambazwaji wa vifaa vya kufundishia,vitabu, na mambo mengi...ni process tuwe na subira
 
Mimi naamini kitu chochote kilichoboreshwa, kilichorekebishwa au kinacho anzishwa hakiwezi kuwa na ufanisi kwa haraka.
Hii inaweza kupita hata miaka 5 kuendelea ilinkupata matokeo chanya pamoja na ufanisi.

Sina hakika kama serikali kusudio lake sio sahihi, bali kuna namna wangefanya matokeo mazuri yaonekane mapema.
 
Ilihitaji maandalizi ya kutosha kutosha ku implement mtaala huu mpya kwa sababu hakuna miundombinu wezeshi wala training ya kutosha kwa walimu. Watalazimika kuwafaulisha wanafunzi kwa lazima ili isionekane kwamba sera imefeli, ukiacha wahitimu wasio na ajira sasa hivi watatengeneza janga jipya mtaani, janga la waliohitimu ufundi wasio na ujuzi.
 
Mama ameweza, amewafikia, hana deni😌 🇹🇿
 
Amani iwe juu yenu...

Tanzania ilianza mchakato wa sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023, mwaka 2022. Mpaka sasa Kwa shule za msingi utekelezaji ulishaanza na wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la nne wanaendelea nao.

Kwa shule za sekondari mtaala huo umeanza mwaka huu 2025 Kwa kidato Cha kwanza. Na kidato Cha tano utaendelea mwaka huu 2025 baada ya kusitishwa mwaka Jana.

NI MAJANGA KWA KWELI...
Nakubaliana na wewe,

Pamoja na hayo, naomba nikukumbushe mwaka 2006 wakati shule za kata zinaanza, mitazamo ya wengi ilikuwa kama yako lakini unaweza ona matokeo yake, watu walizibeza hazina walimu na ilkuwa ni kweli
Mifano iko mingi

Nataka kusema kwamba hakuna mabadiliko yasiyo na changamoto, hata kwa level ndogo ya familia, mfano, wazazi wakianza ujenzi utaona mabadiliko hata aina ya chakula 😜 inabadilika kwasababu ya ufinyu wa bajeti watoto kwa akili ndogo watasikitika, lakini huwa ni mapito

Mwisho, nikupongeze kwa kuonesha kasoro zilizojitokeza bila shaka wahusika watazifanyia kazi

wasalaamu
 
Mabadiliko yanaanza taratibu mtaala wenyewe ndio kwanza una mwezi mmoja kuna usambazwaji wa vifaa vya kufundishia,vitabu, na mambo mengi...ni process tuwe na subira
Ndugu yangu mtaala na walimu kipi ilitakiwa kianze?

nimetoa mifano hapo juu mabadiliko ya sera na mitaala iliyofeli !!

Mwaka Jana sekondari ya juu ( A level) ilibidi uahirishe Kwa sababu ya mambo kama haya.
 
Mimi naamini kitu chochote kilichoboreshwa, kilichorekebishwa au kinacho anzishwa hakiwezi kuwa na ufanisi kwa haraka.
Hii inaweza kupita hata miaka 5 kuendelea ilinkupata matokeo chanya pamoja na ufanisi.

Sina hakika kama serikali kusudio lake sio sahihi, bali kuna namna wangefanya matokeo mazuri yaonekane mapema.
vipi kuhusu Yale mabadiliko ya 2005? vipi kuhusu 2010 ?? yalileta tija Gani ?

Kuna walimu mpaka Leo hawajui kilibadilishwa nini hasa !?

wangine wanajua ni mada na mpangilio wake tu hakuna kingine....

Serikali haitaki kujifunza na maana WATOTO WAO HAWASOMI HIZO SHULE.
 
Ilihitaji maandalizi ya kutosha kutosha ku implement mtaala huu mpya kwa sababu hakuna miundombinu wezeshi wala training ya kutosha kwa walimu. Watalazimika kuwafaulisha wanafunzi kwa lazima ili isionekane kwamba sera imefeli, ukiacha wahitimu wasio na ajira sasa hivi watatengeneza janga jipya mtaani, janga la waliohitimu ufundi wasio na ujuzi.
walitoka CONTENT kwenda COMPETENCE lakini mashuleni watoto waliendelea kufundishwa content...
 
Nakubaliana na wewe,

Pamoja na hayo, naomba nikukumbushe mwaka 2006 wakati shule za kata zinaanza, mitazamo ya wengi ilikuwa kama yako lakini unaweza ona matokeo yake, watu walizibeza hazina walimu na ilkuwa ni kweli
Mifano iko mingi

Nataka kusema kwamba hakuna mabadiliko yasiyo na changamoto, hata kwa level ndogo ya familia, mfano, wazazi wakianza ujenzi utaona mabadiliko hata aina ya chakula [emoji12] inabadilika kwasababu ya ufinyu wa bajeti watoto kwa akili ndogo watasikitika, lakini huwa ni mapito

Mwisho, nikupongeze kwa kuonesha kasoro zilizojitokeza bila shaka wahusika watazifanyia kazi

wasalaamu
Yale waliolalamikia mwaka 2006 ndio yalizaa watumishi incompetent na Wala rushwa wanaolalamikiwa katika Utumishi wa umma.

madhara ni makubwa mnooo.
 
Nafikiri mambo yanafanyika taratibu.
Unajua Elimu yenyewe bure, kumaanisha serikali itakuwa inachota pesa sehemu nyingine ili kuendesha sekta ya Elimu.

Kuajiri waalimu wapya wa Masomo kama ya ushonaji, Muziki, Ususi, kufunga Solar n.k ni mchakato ila Ajira zimetolewa ingawaje hazitoshelezi

Kuandaa Majengo na vifaa vya kufundishia Masomo mapya nayo ni kipengele kingine.
Kote huko wanahitaji pesa.

Ni vizuri Wazo lishawekwa Kati, utekelezaji umeanza kidogokidogo.

Mpaka 2027 mambo yatakuwa angalau
 
Ilihitaji maandalizi ya kutosha kutosha ku implement mtaala huu mpya kwa sababu hakuna miundombinu wezeshi wala training ya kutosha kwa walimu. Watalazimika kuwafaulisha wanafunzi kwa lazima ili isionekane kwamba sera imefeli, ukiacha wahitimu wasio na ajira sasa hivi watatengeneza janga jipya mtaani, janga la waliohitimu ufundi wasio na ujuzi.
Serikali wanazingua sana!
 
Nafikiri mambo yanafanyika taratibu.
Unajua Elimu yenyewe bure, kumaanisha serikali itakuwa inachota pesa sehemu nyingine ili kuendesha sekta ya Elimu.

Kuajiri waalimu wapya wa Masomo kama ya ushonaji, Muziki, Ususi, kufunga Solar n.k ni mchakato ila Ajira zimetolewa ingawaje hazitoshelezi

Kuandaa Majengo na vifaa vya kufundishia Masomo mapya nayo ni kipengele kingine.
Kote huko wanahitaji pesa.

Ni vizuri Wazo lishawekwa Kati, utekelezaji umeanza kidogokidogo.

Mpaka 2027 mambo yatakuwa angalau
Wangeacha wasubiri wakiwa tayari Kwa uzoefu wangu mabadiliko ya Elimu yote Nchi hii hayajawahi kuwa na tija.
 
Ndugu yangu mtaala na walimu kipi ilitakiwa kianze?

nimetoa mifano hapo juu mabadiliko ya sera na mitaala iliyofeli !!

Mwaka Jana sekondari ya juu ( A level) ilibidi uahirishe Kwa sababu ya mambo kama haya.
Wewe ni mwalimu? Unatakiwa uelewe vizuri kuwa lazima ubadirishwe mtaala ndio utekelezaji ufate. Kwa hiyo tulia usiwe na haraka.
 
Wewe tu ndio uelewi labda kwasababu ya umri wako, lakini nchi hii inaeleweka, kila waziri wa elimu huwa anakuja na mauza uza yake, na akiondoka anaondoka nayo.

Ulitegemea kuona nini?
 
  • Thanks
Reactions: K11
Back
Top Bottom