Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzània Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akiizundua Sera mpya ya Elimu ya Taifa hilo amezitaka mamlaka zinahusika kuhakikisha mashirikiano baina ya Serikali na Sekta binafsi PPP yanaingia kwenye Sera hiyo Mpya ya Elimu ili kufundishwa mashuleni.
Huko mbele Taifa la Tanzania na Dunia ziendako Kuna wasiwasi huenda nchi na mataifa mbalimbali tajiri duniani kuendelea kuzisaidia Serikali zetu itakuwa ni jambalo gumu ila itawezekana tu kwa kupitia Sekta binafsi.
Serikali inaweza ikavuna mitaji, teknolojia pamoja na Utaalamu kutoka katika sekta binafsi kwa kutumia PPP alihimiza Rais Samia.
Tumejaribu kupita katika tovuti ya kituo hicho PPPC, kinatarajia kuvuta mitaji na huduma zenye thamani ya $9bn zaidi ya Trilioni 25 za Kitanzania kwa kutumia miradi ya PPP.
Rais Samia aliahidi kwenye hotuba yake ya kumaliza mwaka 2024 kuwa nchi yake kwa mwaka 2025 itatekeleza miradi mingi zaidi kwa misingi ya Ubia na Sekta binafsi toka ndani na nje ya Tanzania.
Loading…
www.mwananchi.co.tz