Sera mpya ya Elimu, PPP ya David Kafulila ndani

YAY

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2024
Posts
362
Reaction score
381

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzània Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akiizundua Sera mpya ya Elimu ya Taifa hilo amezitaka mamlaka zinahusika kuhakikisha mashirikiano baina ya Serikali na Sekta binafsi PPP yanaingia kwenye Sera hiyo Mpya ya Elimu ili kufundishwa mashuleni.

Huko mbele Taifa la Tanzania na Dunia ziendako Kuna wasiwasi huenda nchi na mataifa mbalimbali tajiri duniani kuendelea kuzisaidia Serikali zetu itakuwa ni jambalo gumu ila itawezekana tu kwa kupitia Sekta binafsi.

Serikali inaweza ikavuna mitaji, teknolojia pamoja na Utaalamu kutoka katika sekta binafsi kwa kutumia PPP alihimiza Rais Samia.

Tumejaribu kupita katika tovuti ya kituo hicho PPPC, kinatarajia kuvuta mitaji na huduma zenye thamani ya $9bn zaidi ya Trilioni 25 za Kitanzania kwa kutumia miradi ya PPP.

Rais Samia aliahidi kwenye hotuba yake ya kumaliza mwaka 2024 kuwa nchi yake kwa mwaka 2025 itatekeleza miradi mingi zaidi kwa misingi ya Ubia na Sekta binafsi toka ndani na nje ya Tanzania.

 
Namkubali sana mama apewe mitano Kisha mitano mingine
 
Hii kama ni kweli basi ni nzuri sana
 
Hili ni jambo jema sana Leo kwa sababu watu hawaifahamu PPP Kafulila anaonekana kama anatumika.
 
Mzee wa promo Kafulila nadhani Kwa Sasa huyu Kafulila ndio namba moja kumpigia debe Samia
 
PPP ilionekana kama kichaka Cha kupiga dili nadhani kama utaanza kufundishwa mashuleni italeta uelewa mpana japo upigaji ni mkubwa hasa kwa Wawekezaji toka nje, PPP imezitia nchi nyingi hasara duniani
 
PPP ndio mkombozi wa dunia
 
PPP itaanza kufundishwa katika level gani ya Elimu?

Mimi ningependekeza walau kuanzia darasa ya sita ambalo ndio darasa la mwisho kwa level ya msingi
 
PPP itaanza kufundishwa katika level gani ya Elimu?

Mimi ningependekeza walau kuanzia darasa ya sita ambalo ndio darasa la mwisho kwa level ya msingi
Huko ni mbali, darasa la nne au la Tano itafaa sana, Hii PPP itawafanya vijana wetu wakue na kuja kuwekeza kwenye nchi yao
 
PPP lazima pia tuiangalie kwa ukaribu Kuna mataifa yanalia kwa hii PPP umakini unahitajika
 
Hapa namuunga mkono huko mbele hakuna mwekezaji ila wabia watakuwepo
 
PPP hata Mwl Nyerere aliitamani ila hii ya Samia Nina mashaka nayo
 
Hii ni nzuri sana aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…