Sera za faragha za WhatsApp zimekuwa zaboreshwa tangu mwaka jana mwezi Julai.
Itakumbukwa WhatsApp walitoa tangazo la kuboresha sera za faragha na hii ya kuongeza kipengele taarifa za mtumiaji wakawekea hapo.
Taarifa hizo za faragha za mtumiaji ambae ana akaunti ya Facebook zaweza kujumuishwa kwa pamoja baina ya mitandao hiyo miwili pale mtumiaji atumiapo mitandao hiyo kwa shughuli za kibiashara.
Hivyo sera za kugawana, kubadilishana au kuchangiana taarifa za watumiaji wa mitandao hiyo kwa nje ya bara la Ulaya ni rahisi zaidi kwani barani Ulaya wana sera ngumu za kuwakinga raia wao wasianikwe taarifa zao za faragha.
Nje ya bara ya Ulaya nchi kadhaa hutumia mwanya huo kutafuta taarifa za faragha za watumiaji ambao hukosa serikali za nchi hizo.
Tukumbuke pia pamoja na taarifa hizo zilizotajwa hapo juu, pia kutatakiwa kutolewe taarifa za kujsajili kwenye WhatsApp, namba ya simu, mabadilishano ya ujumbe au "transactions data", taariza za kutumiana ujumbe wa papo kwa papo au "interaction"na anuani ya protokali ya simu ya mtumiaji au IP address.
Yawezekana kabisa kuwa serikali za nchi hizi ambazo zingine zimepitisha tayari sheria za mitandao na zipo "active" kwa kutumia mamlaka za mawasiliano na kuna vipengele kadhaa ambavyo vyabinya mitandao hii inapotaka kujipenyeza kwa upana wake katika nchi hizo.
Kwa mfano bara la Afrika kama uchumi ukuao au "emerging economy", uwingi wa watumiaji wa hii mitandao khasa vijana inakuwa ni sumaku ya kuvutia uwekezaji wa mitandao hii kibiashara.
Lakini katika kuingia kuwekeza barani humo na mabara mengine kama Asia masuala kama kuwekeana kamba za masharti "String attached" yanakuwa yalazimishwa kwa nguvu zote.