Kwanza kabisa napenda kumpongeza Rais wetu kwa hatua kubwa aliyofikia na kubwa zaidi ya yote ni hili la sera mpya ya elimu.Siku zote nimekuwa naamini hakuna mapinduzi makubwa duniani kama kujipundua mwenyewe kimawazo na kifikra.Je ni vipi mtu unaweza kijipindua? Ni kupitia elimu tu.
Kwa muda mrefu sana tumenyanyanyisa na elimu inayojenga uwezo wa kukuza uchumi wa mataifa yaliyotutawala ,kwa muda tumebaki kuwa wasindikizaji na watumwa wa fikra. Elimu mbovu imepelekea hili Taifa kuwa kwenye njia panda. Leo hii Tatizo la ajira ni kubwa mno na hata kama nafasi za ajira zipo basi hakuna watu wanaoweza kumudu nafasi. Tatizo la elimu limepelekea tutawaliwe na kundi la watu wachache ambao kila walichokisema basi tulikifuata.
Suala la Lugha limekuwa kilio changu kwa muda mrefu sana. Miaka michache iliyopita nilitoa maada hii lakini bahati mbaya watu wengi walinipinga sana.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-and-the-future-of-tanzanians.html#post884255
Walinipinga ni kwa sababu hawana uwezo wa kuliona Taifa letu miaka mia moja ijayo. Manufaa ya kutumia lugha ya Kiswahili kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu yanawezekana hatutayaona leo lakini miaka kumi na tano ijao tutaona matunda yake. Matunda ambayo kila Mtanzania atajivunia. Matunda ambayo kila mtu atapenda kuyala. Kiswahili ndo lugha yetu na si Kizungu na si Kigermani na Kichina. Naongea si kwamba mimi mbaguzi ila sioni umuhimu wa kutumia Kizungu wakati mimi ni Mtanzania.
Leo tumeona wimbi la nchi zetu za jirani Congo, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda na zingine nyingi zitafuta upepo sijui Mozambique, Malawi, Zambia na hilo ndo litatakiwa lile lengo letu-Kama leo haya mataifa yanataka kutumia lugha yetu Je kuna sababu ghani sisi kudharau lugha yetu?
Kama leo Kiswahili kitatumia kwa mataifa mengine kama ilivyo kwa kenya leo basi kuna uwezekano Tanzania likawa Taifa kubwa sana kwenye uso wa ulimwengu, Taifa - kiuchumi, kiulizi, kisiasa na mengineyo..
Hakuna umuhimu wa kuogopa eti kwa tutawezaje kujihusisha na biashara za kimataifa. Je nchi kama Poland,Norway,Urusi,China, na zingine nyingi nyingi ambazo sijazitaja wamewezaje kukuza uchumi wao na kufanya biashara za kimataifa? Wameweza kwa nini na sisi tusiweze...Warabu wameweza kwa nini Watanzania tusiweze?
Kuna faida nyingi sana zitapatika kwani tutatengeneza wataalamu wetu kwenye fani zetu je ni mara ngapi tumesikia wanafunzi wanashindwa kuelewa somo kwa kizungu na mwalimu anaanza kufafanua kwa Kiswahili?
Je tunakihitaji kizungu? Binafsi mimi sikihitaji. Pia faida nyingi sana za kimaendeleo zitapatikana, suala kubwa kuna uwezekano wa kutatua tatizo la ajira kwa kiwango kikubwa.
WAZO LANGU:
Sera hii ni nzuri ila kwa siku za usoni lazima tuanze kuliangalia na suala la shule binafsi. Hakuna nchi iliyofikia maendeleo makubwa kwa kuruhusu shule binafsi. Nguvu kubwa lazima ielekezwe kwenye shule za serikali, tuboreshe shule ziwe za kisasa zaidi na wanafunzi wapate elimu yenye kiwango cha dunia ya elimu bila gharama zozote. Kuruhusu shule binafsi ni sawa na kujenga nyumba bila msingi, vipi kama pakitokea mafuriko?
Mwisho kwa sera hii mpya naomba tuungane nuvu na Rais wetu bila kujali kasoro za kabira,dini,rangi. Hii ni elimu yetu na hawa ni watoto wetu. Rais hatafikia malengo bila ushirikiano wetu. Nimeandika si kwamba nimetumwa, nimeandika kwa sababu nina watoto na hawa watoto ni wajamii nzima ambayo jamii ni sisi wenyewe.
Yawezekana sisi umri wetu tayari hatuwezi kufikia malengo ya kiuchumi na mengine basi tujenge nchi ambayo watoto wetu wataishi kama Watanzania na si watumwa ndani ya nchi yao wenyewe.