Sera ya Kilimo kwanza nini msingi wake?

Sera ya Kilimo kwanza nini msingi wake?

Nemesis

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2008
Posts
5,517
Reaction score
4,477
Chama cha Mapinduzi (CCM), Serikali yake na watendaji wa umma (civil servants) wanatangaza na kuhamasisha sera/kauli mbiu mpya ya KILIMO KWANZA. Taifa letu limepita katika vipindi mbalimbali vilivyopelekea kutungwa kwa sera/kaulimbiu kadhaa. Mfano Siasa ni kilimo, Kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa nk. Kauli hizo zilikuwa na mwanzilishi, msingi na msukumo wake japo hazikufanikiwa.

Hii kauli ya sasa, imeanza ghafla, ni kama mtu ametoka usingizini na kutoa kauli ndipo Serikali na CCM wakapanga siku ya kuzindua sera hiyo. Nimekuwa nikifuatilia nini chanzo na msingi wa kauli mbiu hii bila mafanikio. Viongozi wamekuwa wagumu kueleza uwazi wa sera hii.

Laghaula, leo nimepata kusikiliza kipindi cha MUVIWATA kupitia Radio Maria Tanzania 89.1FM. Kipindi hicho kimejitahidi kuweka wazi kwa sehemu na kujaribu kujibu baadhi ya maswali ya msingi juu ya kaulimbiu au sera hii.

KILIMO KWANZA ni kauli mbiu iliyoanzishwa na WAFANYABIASHARA ili kutimiza malengo yao ya kibiashara. Kauli hii haikutoka kwa mkulima wala Serikali au viongozi wa kisisa. CCM na Serikali yetu walipoipata hiyo kauli wakaichukua kama kawaida yao, bila hata kuitafakari kwa umakini na kuanza kuihubiri.

Kutokana na msingi huu, Je sera hii itasaidia kuinua kilimo? Ni nini malengo ya KILIMO KWANZA?

Naomba wenye taarifa zaidi watusaidie kuweka wazi chanzo, msingi, malengo ya kauli hii. Binafsi nipo very pessimistic kutokana na sababu nilizozitoa hapo juu.
 
Huu ni usanii mwingine. Haifiki kokote!!! Inahitaji pesa nyingi kutekeleza hizo pillars zao. Je serikali ya awamu ya nne imejiandaa kwa hili??? Kuna programmes nyingi na bado hazijatekelezwa, kwa kukosa funding. Hata development parners were a bit shocked na kuanza kuuliza kama wana acha kutekeleza ASDP (Agricultural Support Development Programme) ambayo wanaifadhili!!! Walitulizwa kuwa KILIMO KWANZA (GREEN REVOLUTION) ni sehemu ya utekelezaji wa ASDP???!! Mimi sijui hapo tena wakuu na mipango ya nchi hii. Hii imeingia kichwakichwa!!! Politics is the dirtiest game ever!!!

2010 is just at the corner!!1 Wapiga kura wengi ni wakulima, viini macho vya kuomba kura!!
 
[COLOR=DarkRed said:
KILIMO KWANZA ni kauli mbiu iliyoanzishwa na WAFANYABIASHARA ili kutimiza malengo yao ya kibiashara. Kauli hii haikutoka kwa mkulima[/COLOR]

Huu ndio msingi wa kilimo kwanza, mkulima original wa Tanzania amewahi kuangaliwa na kujaliwa na mtu yoyote? Kidogo wakati wa Siasa ni Kilimo subsidy ya mbolea na pembejeo mpaka vijijini, kilimo ni uti wa mgongo wa nchi hii pale mkulima alithaminiwa lakini sasa SIJUI LABDA MAAJABU YATOKEE!!!!!!!!!!!
 
Huu ni usanii mwingine. Haifiki kokote!!! Inahitaji pesa nyingi kutekeleza hizo pillars zao. Je serikali ya awamu ya nne imejiandaa kwa hili??? Kuna programmes nyingi na bado hazijatekelezwa, kwa kukosa funding. Hata development parners were a bit shocked na kuanza kuuliza kama wana acha kutekeleza ASDP (Agricultural Support Development Programme) ambayo wanaifadhili!!! Walitulizwa kuwa KILIMO KWANZA (GREEN REVOLUTION) ni sehemu ya utekelezaji wa ASDP???!! Mimi sijui hapo tena wakuu na mipango ya nchi hii. Hii imeingia kichwakichwa!!! Politics is the dirtiest game ever!!!

2010 is just at the corner!!1 Wapiga kura wengi ni wakulima, viini macho vya kuomba kura!!

Ndo hao ya kukurupuka, sera hii imetangazwa kama wiki moja baada ya bajeti kutangazwa. Wangekuwa wameipata mapema maybe wangeweza kuiingiza kwenye bajeti.

ASDP inafanya vizuri, tena ukaguzi wake unafanywa na LOcal Government Support Program au Local Government Development Grant (LGSP au LGDG) hawa jamaa hawana mchezo. Endapo Serikali ingeongeza mchango wake hapo yaani kuongezea ktk kile wanachotoa wafadhili tungeweza kufanya vema zaidi.

Hii ya kuanzisha sera kwa lengo la kupata kura, itashia kushindwa kama zilivyoshindwa vibaya kauli mbiu za maisha bora kwa kila Mtanzania na ile ya kasi mpya.
 
Huu ndio msingi wa kilimo kwanza, mkulima original wa Tanzania amewahi kuangaliwa na kujaliwa na mtu yoyote? Kidogo wakati wa Siasa ni Kilimo subsidy ya mbolea na pembejeo mpaka vijijini, kilimo ni uti wa mgongo wa nchi hii pale mkulima alithaminiwa lakini sasa SIJUI LABDA MAAJABU YATOKEE!!!!!!!!!!!

Ulimwengu sasa unafuata nadharia ya 'bottom up'. Tena wakulima wanaibiwa na kunyonywa sana na wafanyabiashara. Wafanyabiashara ndiyo wanaopanga bei ya mazao, ndio wanaoamua vipo na lopesa. Kweli leo wanaweza kuanzisha kitu chema kwa mkulima?
 
Serikali hii ni ya kupiga kelele tu za majukwaani, walipiga marufuku wakulima kulazimishwa kuuza mazao kwenye magunia kwa mtindo wa lumbesa lakini walishindwa kusimamia. Makelele mengi sana.
 
Ni kweli kwamba kukosekana kwa vipimo ni tatizo pia na ni moja ya vyanzo wa kuibiwa kwa wakulima hata kile kidogo wanachokipata kwa shida. Nchi zilizoendelea mkulima hauzi kitu bila mizani (beam balance), hata nyanya, viazi, mboga za majani, vitunguu swaumu (galic), matunda nk vinapimwa kwenye mizani.

Ni vema idara ya vipimo, wizara ya kilimo, TCCIA nk kutafuta vipimo vya mazao. Itakuwa rahisi hata kufuatilia kodi.
 
Hii ni misemo tu ya CCM hakuna lolote, mbona kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya imefulia siku nyingi na hakuna anyeitaja hadharani hata kikwete mwenyewe. Hii ya kilimo kwanza hata january haifiki.
 
Chama cha Mapinduzi (CCM), Serikali yake na watendaji wa umma (civil servants) wanatangaza na kuhamasisha sera/kauli mbiu mpya ya KILIMO KWANZA. Taifa letu limepita katika vipindi mbalimbali vilivyopelekea kutungwa kwa sera/kaulimbiu kadhaa. Mfano Siasa ni kilimo, Kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa nk. Kauli hizo zilikuwa na mwanzilishi, msingi na msukumo wake japo hazikufanikiwa.

Mkuu kama wewe ni Mtanzania na unajua mwaka huu na ujao kuna nini, utajua kwanini Kilimo Kwanza sasa hivi. Tatizo jamaa wameshtuka mmekuwa wajanja mno mnachokonoa kila mahali mara Richmond, mara BOT mara Kiwira. Sasa wanawatwanga dozi kwenye mshipa, waone jeuri yenu
 
Date::10/1/2009Serikali yatangaza Sh58bilioni kila wilaya za ‘Kilimo Kwanza’
Na Gedius Rwiza
SERIKALI imetenga Sh 58 bilioni kwa kila wilaya kwa ajili ya kuboresha mazingira ya maofisa ugani ili waweze kutekeleza vema mkakati wa Kilimo kwanza.

Fedha hizo zitatumika kununulia magari, pikipiki na baiskeli zitakazotumika katika utendaji wa kazi za maofisa hao mashambani.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, jijini Dar es Salaam juzi, Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Dk David Mathayo, alisema kuwa serikali imetenga fedha hizo za kila wilaya kwa ajili ya kuhakikisha kila ofisa ugani anapata usafiri wakati wa kutoa huduma za kilimo.

Dk Mathayo alisema kutokana asilimia 90 ya watanzania kutegemea chakula kinachotoka hapa nchini, serikali imeona haina budi kuboresha mazingira ya kilimo ili kutimiza kauli mbiu ya kilimo kwanza.

“Serikali imejiandaa kuhakikisha kila wilaya inapata magari na wale wa ngazi ya kata kila mmoja atapewa pikipiki na wale wanaofanya kazi ngazi ya vijiji watapewa baiskeli pamoja na kujengewa nyumba ili wawe na moyo wa kutoa huduma za kilimo kwa wakulima,”alisema Dk.Mathayo.

Kuhusu watalaamu wa kilimo, alisema serikali inatarajia ifikapo mwaka 2011 kutakuwa na uhakika wa kupata wahitimu wa fani za kilimo takribani 15,000 na kwamba kwa sasa wana uhakika wa kupata wahitimu zaidi ya 2,500 kila mwaka wanaomaliza katika vyuo mbalimbali vinavyotoa mafunzo ya kilimo.

Alitoa wito kwa vijana kujitokeza kusoma fani za kilimo bila kujali kwamba watapata ajira bali ni faida hata kwa maisha yao mahali popote na kwamba mtu mwenye utaalamu wa kilimo anaweza kujiajiri mwenyewe.

“Mtu mwenye ujuzi wa kilimo sio tu kwamba ajiriwe bali anaweza kuishi mahali popote na akaweza kuanzisha mashamba yake binafsi bila kumtegemea mtu, kwahiyo napenda kutoa wito kwa vijana wote kupenda kusomea masuala ya kilimo,”alieleza Dk.Mathayo.

Naibu waziri huyo pia alisema serikali imetenga Sh 118 bilioni kwa ajili ya ruzuku, mbolea, mbegu na dawa ya mazao na kwamba serikali inathamini sana wakulima ambao wanajihusisha na masuala ya kilimo na imepanga kuwawezesha kuwapa ruzuku ili wafanikishe kuendeleza kilimo.

Kuhusu maandalizi ya kilimo, Dk Mathayo aliwataka wananchi kutunza vyanzo vya maji na kutunza mazingira ili kupata sehemu za kupanda mazao mbalimbali.
Hii ndiyo kilimo kwanza. Maswali ya kujiuliza je, matatizo ya kilimo chetu ni nini? vipaumbele ni vipi?
well, kwa hapa inaonekana matatizo ni magari, pikipiki, baiskeli na nyumba. Je, hii ni kweli?
Sera ya Serikali ktk kilimo kwanza inaonekana kuto mlenga mkulima moja kwa moja. Je, itafanikiwa kuleta mapinduzi ya kilimo?

My opinion, Serikali ingeweka mikakati na mipango ya kuongeza uzalishaji na tija (productivity) ktk kilimo. Baada ya kufanikiwa ktk hilo ndipo tatizo la watalaam kukosa usafiri lingejitokeza kutokana na uwingi wa uhitaji wa huduma yao. Anyway I'm done
 
CHANZO CHA HIZO KELELE ZA KILIMO KWANZA NI KUWA SIKU MOJA
MJINGA MMOJA ALIKUWA ANATAZAMA TV YA MLIMANI AKAONA

WAMEANDIKA ELIMU KWANZA......
NA yeye akaamua kujifanya mbunifu na kuja
na huo upuuzi wa KILIMO KWANZA...
HIII NCHI HAMNA KITU KABISA...
 
badala ya hata kufikiria kumwaga pesa kwenye matrekta,mbolea yakayosaidia wakulima moja kwa moja wao wanaongea kununua magari na pikipiki za maofisa kilimo!
 
Koba, tumesalitiwa mkuu, yaani hii ni aibu kubwa. Huu ni ufujagi wa fedha za umma. Fikiria kuna Wilaya ngapi, kata ngapi na vijiji vingapi ndo utajua kuwa hiyo pesa ni nyingi sana.

Kwanini wasichague maeneo machache wakazalisha chakula cha kutosha hasa kwa kuanzia? Let say wakaamua kuanzisha mashamba ya umwagiliaji bonde la Rufiji, Ruaha na Kilombero. Wakazalisha chakula kingi na kukisambaza nchi nzima.
 
Hii ndiyo kilimo kwanza. Maswali ya kujiuliza je, matatizo ya kilimo chetu ni nini? vipaumbele ni vipi?
well, kwa hapa inaonekana matatizo ni magari, pikipiki, baiskeli na nyumba. Je, hii ni kweli?
Sera ya Serikali ktk kilimo kwanza inaonekana kuto mlenga mkulima moja kwa moja. Je, itafanikiwa kuleta mapinduzi ya kilimo?

My opinion, Serikali ingeweka mikakati na mipango ya kuongeza uzalishaji na tija (productivity) ktk kilimo. Baada ya kufanikiwa ktk hilo ndipo tatizo la watalaam kukosa usafiri lingejitokeza kutokana na uwingi wa uhitaji wa huduma yao. Anyway I'm done

Hivi unapoongelea mikakati na mipango ya kuongeza uzalishaji hili la vitendea kazi kwa maafisa ugani sio moja kati ya hiyo mikakati unayoongelea ya kuongeza uzalishaji?
 
Hivi unapoongelea mikakati na mipango ya kuongeza uzalishaji hili la vitendea kazi kwa maafisa ugani sio moja kati ya hiyo mikakati unayoongelea ya kuongeza uzalishaji?

Mkuu ngoja nikuambie a simple logic: Kunapokuwa na upanuzi wa kilimo, uzalishaji na shughuli ndipo kunakuwa na uhitaji wa mkubwa wa watalaam. Hapo ni kunakuwa na tatizo la watalaam kushindwa kufika maeneo yanayotakiwa kwa wakati, ndipo uhitaji wa magari, pikipiki na baiskeli unapotokea. But not fro nothing!

Mkuu mimi nahoji: Kilimo kwnza inataka kuleta mapinduzi ya kilimo sasa Je, matatizo ya sasa ktk kilimo ni yapi?

Kwani huwezi kuleta mapinduzi ya kilimo bila kujua hali halisi ya sasa (situational analysis). Huwezi kupanga kupanga na kutekeleza mikakati bila kujua tatizo (undesirable situation) ni nini? Huwezi kufikia lengo bila kujua unataka kuvuna nini (goal/desirable situation).

Serikali imekurupuka tu na kutenga mabillioni ya walipa kodi kununulia magari, pikipiki, baiskeli na kujenga nyumba bila kupitia mchakato stahili.

Kimey, nadhani unatakiwa kuwa na huruma japo kidogo kwa nchi yako. This is a false start of 'Kilimo Kwanza'.
 
Kilimo kwanza ni idea ya best yake mkuu wa kaya, dunstan mrutu, the executive secretary of tanzania national business council (tnbc). aliibuni na akaipropose katika local investors roundtable ndipo watu wa serikali wakaiadopt, haina kubwa jipya ukilinganisha na mipango kama hiyo iliyokwisha kufanywa huko nyuma. in other words its is new wine in an old bottle
 
Back
Top Bottom