Nemesis
JF-Expert Member
- Feb 13, 2008
- 5,517
- 4,477
Chama cha Mapinduzi (CCM), Serikali yake na watendaji wa umma (civil servants) wanatangaza na kuhamasisha sera/kauli mbiu mpya ya KILIMO KWANZA. Taifa letu limepita katika vipindi mbalimbali vilivyopelekea kutungwa kwa sera/kaulimbiu kadhaa. Mfano Siasa ni kilimo, Kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa nk. Kauli hizo zilikuwa na mwanzilishi, msingi na msukumo wake japo hazikufanikiwa.
Hii kauli ya sasa, imeanza ghafla, ni kama mtu ametoka usingizini na kutoa kauli ndipo Serikali na CCM wakapanga siku ya kuzindua sera hiyo. Nimekuwa nikifuatilia nini chanzo na msingi wa kauli mbiu hii bila mafanikio. Viongozi wamekuwa wagumu kueleza uwazi wa sera hii.
Laghaula, leo nimepata kusikiliza kipindi cha MUVIWATA kupitia Radio Maria Tanzania 89.1FM. Kipindi hicho kimejitahidi kuweka wazi kwa sehemu na kujaribu kujibu baadhi ya maswali ya msingi juu ya kaulimbiu au sera hii.
KILIMO KWANZA ni kauli mbiu iliyoanzishwa na WAFANYABIASHARA ili kutimiza malengo yao ya kibiashara. Kauli hii haikutoka kwa mkulima wala Serikali au viongozi wa kisisa. CCM na Serikali yetu walipoipata hiyo kauli wakaichukua kama kawaida yao, bila hata kuitafakari kwa umakini na kuanza kuihubiri.
Kutokana na msingi huu, Je sera hii itasaidia kuinua kilimo? Ni nini malengo ya KILIMO KWANZA?
Naomba wenye taarifa zaidi watusaidie kuweka wazi chanzo, msingi, malengo ya kauli hii. Binafsi nipo very pessimistic kutokana na sababu nilizozitoa hapo juu.