π Wapo baadhi ya wanaharakati uchwara waliokuwa wakitarajia kuona Dkt. Samia Suluhu Hassan akitumia lugha kali dhidi ya Marekani katika mahojiano yake ili kuonyesha upande anaouunga mkono.
π Kwa mtazamo wao, walidhani njia bora ya kuimarisha uhusiano na Urusi ni kuikosoa hadharani Marekani.
π Hata hivyo diplomasia ya kisasa haijengwi kwa misingi ya matusi, lawama au mashambulizi ya kisiasa.
π Kiongozi makini hutafuta maslahi ya Taifa lake kwanza kabla ya kutafuta makofi ya kisiasa kutoka kwa upande wowote.
π Tanzania imekuwa na historia ya muda mrefu ya kufuata sera ya kutokuwa upande wa migogoro ya mataifa makubwa.
π Sera hiyo imeiwezesha nchi kudumisha urafiki na mataifa mbalimbali yenye mitazamo tofauti duniani.
π Diplomasia ya kweli ni sanaa ya kujenga madaraja, si kubomoa mahusiano.
π Mara nyingi viongozi wenye uzoefu huchagua maneno yao kwa umakini mkubwa wanapozungumzia masuala ya kimataifa.
π Kauli za jazba zinaweza kufurahisha baadhi ya watu kwa muda mfupi, lakini zikaharibu maslahi ya Taifa kwa miaka mingi.
π Nguvu ya diplomasia ipo katika busara, si katika kufoka.
π Tanzania inanufaika kwa kushirikiana na mataifa mbalimbali katika biashara, uwekezaji, elimu na teknolojia.
π Hivyo si jambo la hekima kufunga milango ya ushirikiano kwa sababu ya tofauti za kisiasa za mataifa mengine.
π Dkt. Samia suluhu Hassan ameonyesha mara kadhaa kuwa anaamini katika mazungumzo na ushirikiano wa kimataifa.
π Njia hiyo imeendelea kuipa Tanzania nafasi ya kuheshimiwa na kusikilizwa katika majukwaa mbalimbali duniani.
π Marafiki wa kweli wa Taifa hawapimwi kwa ukubwa wa maneno makali wanayosema, bali kwa manufaa wanayoleta kwa wananchi.
π Katika diplomasia, busara mara nyingi huwa na nguvu zaidi kuliko kelele.
π Kiongozi anaweza kujenga uhusiano mzuri na Urusi bila kuwa adui wa Marekani.
π Vivyo hivyo anaweza kushirikiana na Marekani bila kuvunja mahusiano na mataifa mengine.
π Hiyo ndiyo falsafa ya diplomasia ya usawa inayozingatia maslahi ya Taifa kwanza.
π Ndiyo maana mafanikio ya diplomasia hupimwa kwa matokeo yake, si kwa ukubwa wa
maneno yanayotamkwa mbele ya kameraβοΈ