Sera ya Kuwawezesha watanzania weusi ni ya lazima?

Kuna tofauti tunaposema uzawa na Watanzania weusi. Uzawa hauna rangi na naomba iyo tofauti tukubaliane
 
Hapa tunazungumzia wazawa weusi..Kwani ni wazawa wapi hao ambao ndiyo wenye shida?
Usijiconfuse mwenyewe Kamundu.
 
Tanzania ni nchi ya pekee kwa kushindwa kwaendeleza wazawa wake katika fani za biashara kwa makusudi.
Nenda nchi yoyote duniani na uta kuta biashara ambazo zina fanywa na wazawa tu.
Lengo ni kupata ajira kwa wazawa wa nchi hizo.Leo tunashangaa kuwa kikitokea kilio kuwa Watanzania lazima tujipendelee katika nchi yetu watu wanaanza kudai kuwa ni ubaguzi.Katika blog hii nimeona malalamiko kuwa wahindi/wapakistan wasio raia wanendesha maduka pale airpot.
Wachina wanauza mpaka bidhaa rejareja kama machinga hapa nchini.
Na hii wala si Africanisation ya miaka ya sitini, ni uwezeshaji wa wazalendo ili wasiishie kuwa machinga katika nchi yao.
Tanzania tuko nyuma sana katika biashara za kimataifa na hata za kitaifa, sababu mojawapo ni watu wake kukazania kuajiriwa aidha serikalini au kwa waasia.
Hii mentality ya kuwa salaried ni mbaya sana na lazima tuondokane nayo.
Bahati mbaya sana ni kuwa hata viongozi wengi serikalini hawana mwamko au inclination ya kuwawezesha watanzania wenzao kuendelea kwenye biashara/miradi ambayo ni kubwa.Yeyote anayejaribu huwa anapigwa vita,Mifano hai ni mingi.Tanzania itaendelezwa na watanzania na si waPakistan, WaHindi waIngereza au waChina
 
Unyonge wa Mwafrika unatokana na nini? Pampja na Nyani kudai ndivyo tulivyo, je inawezekana kuwa tulilazimishwa kuwa ndivyo tulivyo kifikra na kimazingira kwa muda mrefu kiasi kuwa imekuwa ni sehemu ya jinioloji yetu na urithi?

Naomba mpitie barua hii ya Mfalme Leopold wa Ubelgiji. Sijui kama ni kweli iliandikwa lakini ukipima matokeo ya ukoloni na makovu ya ukoloni, yanaonyesha wazi kuwa kuna ukweli ndani yake.

Sasa ukishaisoma, jiulize kama Iddi Simba alikuwa amekosea au laa!



http://www.world-hi.com/KingLeopoldLetter.html
 
Black empowerment for what and on what grounds? Aren't blacks the overwhelming majority in Tanzania? Don't they run pretty much just about everything? So where does this notion of black empowerment come from? I just don't get it!

I think, in my opinion, it us who are holding ourselves back. The buck stops with us, end of story. We need to get up on our butts and start working, start participating responsibly in the electoral process by booting leaders who betray our trust, and intensify the war against mafisadi by hunting them down and making an example out of them (through the justice system). It can be done only if we want to.
 
1.
Wale wanaosema kuna ubaguzi kuhusu uzawa...Then niwaulize na hao wahindi na caste system si ubaguzi? Mapungufu tuliyonayo ni makubwa kiasi cha kwamba tukifanya marekebisho bado tutakuwa fair na si ubaguzi hata chembe.

- Mkuu Mushi heshima mbele sana, Wahindi sio tatizo isipokuwa tatizo ni sisi wenyewe na serikali yetu kushindwa kui-regulate ipasavyo hiyo sysytem ya
Wahindi, tumeshindwa kwualipisha kodi ipasavyo sasa hatuna wa kumlaumu ila ni sisi wenyewe, sasa hivi tumo kwenye siasa za kibepari sio kijamaa jamaa, ni yule tu anayeweza ku-invest ndiye anyeweza kutusaidia taifa, sio anything else!


2.
- Hapa naona kuna ishu nyingi sana, kuanzia ardhi, ubaguzi, weusi, I mean siamini kwamba bongo tuna matatizo kama ya Zimbabwe kuhusu ardhi, ardhi tunayo ila tumeshindwa kuitumuia kwa faida yetu lakini otherwise on ardhi yetu it has nothing to na ubaguzi au wananchi kutokuwa nayo, kwa sababu ardhi tunayo wananchi unless nina-miss something!
 

- Bravo Mkulu mwenzangu Nyani, maana hapa tupo ukurasa mmoja.
 
Kuwawezesha wazawa kwenye nyanja muhimu za kiuchumi ni jambo la muhimu...Imagine mapesa yote yaliyohamishwa nje pamoja na za mafisadi wetu wazawa...Taifa lingekuwa wapi?
We huoni kwamba kuna uozo hapo na kunahitaji mabadiliko makubwa?
Sasa hao mafisadi kwani sio wazawa? Na title inasema weusi, kwa hiyo watu ambao sio weusi lakini wamezaliwa na kukulia Tanzania inakuaje?
 
Ndio maana makanisa ya Marekani siku hizi wanaanza kufundisha kwamba watumishi wa Mungu ni lazima wawe matajiri na kutoa mifano ya watumishi wote wa Mungu katika agano la kale walikuwa na uwezo, hata kama walihangaika mwanzo lakini walikuwa na uwezo na ni haki ya kila anayemuabudu Mungu kuwa na uwezo.
Lakini hii kitu ya kuwawezesha wa-Tanzania weusi ni lazima ifanyike na ndio maendeleo yatapatikana Tanzania, kwa sababu wa-tanzania ndio watakaoijenga Tanzania na wageni hawana uchungu wowote na Tanzania kwa hiyo watafanya kila njia kuiba au kukwepa kodi na bila kujali lolote. Na USA iko hivi ilivyo sasa kwa ajili ya kuwawezesha wa-Marekani, kwa sababu najua zamani ilikuwa ni priority yao ingawa sasa hivi ndio hivyo mambo ya Globalisation, lakini Marekani ilijengwa na wenyewe kwanza na ndio maana ipo hapa ilipo.
 
Kwa nini tusiwe na sera ya kumwezesha mtanzania yeyote asiye na uwezo bila kujali rangi au uzaliwa wake? Hii kutafuta vijisababu vya kibaguzi kwa matatizo yetu hakutatufikisha popote. Babu na bibi zetu walikubali kumwaga damu zao ili wasihukumiwe kutokana na rangi yao. Leo hii hatuwezi kuwaenzi kwa kugeuka na kufanya kilekile walichokataa wao kufanyiwa. Ubaguzi ni ubaguzi hata uurembeshe vipi. Sisi tunatakiwa kuwa wa mwisho kuuendekeza.

Amandla..........
 

I doubt the authenticity of this letter. Ukiangalia lugha ilivyotumika si ya karne tunayoizungumzia. King Leopold was a monster of the vilest and most evil kind to have ever landed in Africa na hatuhitaji blatant forgeries kama hizi kujua hilo.

Amandla........
 
FMES,
Mkuu hivi ktk akili yako unaamini kwamba mashirika haya ya Ford, GM yataondoka na kufa kifo cha nyani bila kupewa msaada!...U must be kidding! Mkuu wangu jaribu kusoma nyakati kwa sababu hizi ni siasa tupu zinatumika sasa hivi lakini by the end of all this, mashirika haya yatapewa kila msaada yaweze kushindana. Focus ya Marekani ni kuiweka nchi yao ktk uwezo wa kushindana na wanaposema nchi yao ni muhimu uelewe kwamba wewe na mimi hatumo!

Kuna mifano mingi ya nyuma ambayo imewahi kutokea, kwa mfano wakati wa depression mwaka 1984 Uingereza waliliacha shirika la Leyland lianguke kwa sababu kulingana na mfumo wa Ubepari kuweka regulations na serikali kuingilia kati ilikuwa aibu tupu..Wakaliacha likafa na toka siku hiyo mashirika ya Uingereza mengi tu yalishindwa kujiendeleza yakaanza kuuza hisa zake kwa mashirika ya nje ikiwa ni pamoja na Marekani.. Jaguar ni moja wapo..na wanajutia kiuchumi kwani kazi nyingi zimehamia nje (cheap labour) ikiwa ni pamoja na viwanda vya kutengeneza vipuri.

Wakati huo huo nchi kama France ambayo walikuwa socialist waliweza kusaidia shirika la Renault ambalo pia lilikuwa mahututi na limeweza kuinuka na kuendelea hadi leo hii, na kwa uhakika France haijauza wala kufikiria kuuza mali zake. Leo hii ni one of the strong company economically na hawategemei parts kutoka nje..
Japan mabingwa wa biashara ya magari wameingia Marekani lakini nafasi ya Marekani huko Japan ni ndogo sana,hhawa pia wameyasaidia mashirka yao kwa sababu wanafahamu nini uzawa, usisikie mkuu wangu..
Kifupi ni mashirika yote ya magari yamesaidiwa na nchi zao isipokuwa Marekani na wanachelewesha tu kutazama Upepo lakini kwa uhakika Obama hawezi kuyaacha hivi hivi isipokjuwa wataweka masharti..

Unaposema kuwawezesha wananchi ni lazima ulitazame swala hili in a broader way kwa sababu haikatazwi kwa mgeni kushindana wala kupata mikopo isipokuwa nafasi ya kwanza anapewa mzawa.

Mkuu hata ajira ya kazi nchi zote zilizoendelea zinamtazama kwanza mzawa. Mimi nimekuja huko kwenu mwaka 1987, tena makao makuu ya uhamiaji Baltimore, unajua walinambia nini?.. Kazi unayoitaka ni lazima iwe kwanza hakuna Mmarekani anayeweza kuifanya na pili hata kama hakuna bado shirika husika linatakiwa kukuombea kibali cha kufanya kazi..sikutaka kuishi chini ya meza wala kubeba box nikarudi home!

Sasa naweza kuisema hawa wazungu sio sawa na sisi kwa sababu wana wasomi wengi ndani ya nchi tofauti nasi, lakini tunachoomba sisi kuwawezesha wananchi ama niseme wazawa ni kuwepo na utaratibu kama huu toka uhamiaji..Sio swala la shirika kutoa ajira kwa mtu yeyote wanayemtaka toka nje.

Pili ukitazama mikopo, mkulima mzawa mwenye shamba la hekta 10 hawezi kupata mkopo bila kumtumia Patel ambaye hana shamba. Na kibaya zaidi ni kwamba viongozi wetu wana feel confortable ku deal na mhindi kuliko mtu mweusi.. Sasa usije nielewe vibaya kuwa mhindi sio mzawa.. Wapo wazawa lakini tofauti ni kwamba wao wana uraia wa nchi mbili na hakuna utaratibu wowote nchini wa kuwanasa wale wenye kutumia jina la Utanzania kwa kuficha asili na royal yao kwa nchi.
Wapo wahindi walio give a lot to our nation kama kina Rajan, Virani, Kugi's, na wengine wengi sana tu nao kama wazawa wanahitaji kupewa nafasi lakini nao pia wamekutana na mengi ya kuwakwamisha na hata kuhoji Uzalendo wao. Hata waarabu wapo wengi sana wazawa hawa wote ni kundi moja nasi kwa sababu tumesota wote..

Binafsi sina tatizo la rangi hata kidogo na wala siwezi kusema mtu mweusi ana haki zaidi kwa nchi yetu kuliko mhindi, mwarabu ama Mzungu laa hasha! wapo wazawa toka kila rangi na tukianza kutazam watu kwa rangi zao basi itafikia mahala tutaanza kutazama watu kwa asili ya makabila yao kwani rangi ni moja ya alama za asili ya mtu (kabila)...
 
Kwa vile hii ishu ina umuhimu mkubwa, inabidi kuanza kwa kuchanganua msamiati wake.

Mzawa wa Tanzanai ni mzaliwa wa Tanzania. Kuwezesha wazawa ni kuwapa wazaliwa fursa ya kujiinua kiuchumi.

Mzawa ni raia, lakini wako raia ambao sio wazawa. Je, raia wote wanastahili haki sawa? Ndio. Je, kuwapa wazawa fursa ya kujiinua kiuchumi kunakiuka huu msingi wa haki sawa kwa raia wote? Not necessarily.

Affirmative action is sometimes the way to address historical injustices. And there are many historical injustices here. For instance, the colonial government spent several times more on the education of each white or Indian child than it did on the education of "an African" child.

Hatua ya kwanza na ambayo inawezekana tu vizuri ya kuwawezesha wazawa ni kuwarudishia ardhi yao. Ardhi hii ilichukuliwa kuwa mali ya taifa (?) mara baada ya UHURU. (i.e. Independence led to a massive loss of property for wazawa).

Kila mzawa anayetoka sehemu zenye ardhi basi amilikishwe ekari 50 – 100 kutoka katika ardhi inayozunguka kwao. Hiyo pekee itakuwa ni sawa na kumwekea yeye na uzao wake akiba ya VIJISENTI (yaani kama shilingi bilioni moja). Hii ni haki, sio ubaguzi (inambagua nani?) na inawezekana. Ni kuwarudishia wazawa mali zao.

Sasa akija huyu mtu anayeitwa mwekezaji, na akatamani madini yaliyoko kwenye ardhi ya hawa wazawa, itabidi aweke mkataba nao wa kuwamilikisha hisa (sio ruzuku) za kutosha. Serikali itahusika kuhakiki hiyo mikataba.

Labda utauliza fedha za kupimia ardhi zote hizo zitatoka wapi? Zitatoka ARDHI. Kama serikali itaacha utani na kuanza kutoa hati miliki kwa viwanja vilivyopo mijini, na kukusanya kodi za viwanja hivyo, basi MAJISENTI chungu nzima (billions and billions of shillings) yatapatikana.
 

Ingawa wengi wetu hatupendi kuonekana wabaguzi, maneno yetu ndiyo yanayotufunga!Kwani watanzania weusi hawana uraia wa nchi mbili? Mtu anayejiita Patel bado tunasema anaficha asili yake! Natumaini ulimaanisha loyalty na sio royal. Mtu loyalty na patriotism yake haionekani kwa maneno tu. Kwani hao wanaotufilisi wenye rangi kama za kwetu, tutawaita patriots kwa sababu tu wote tumepigwa kiwi? Hauwezi kuepuka kumhukumu Rajan kwa rangi yake kama ulifanya hivyo kwa Patel! Patel ahukumiwe kama Patel kama vile tunavyofanya kwa weusi wenzetu. Rangi isiingizwe kwa namna yeyote ile.

Amandla.....
 
Fundi mchundo,
Mkuu nimetumia jina la Patel kuonyesha mtu ambaye sii mzawa. Nigetumia hata neno Ogah bado ungetafuta sababu lakini kwa maelezo marefu nimeweza kutenganisha yote unayojaribu kunibambikia.. yes, nilikuwa na maana ya royalty lakini sikuwa na maana ya Patroit wala sikusema hakuna mtu mweusi ambaye hana uchungu na nchi yetu...wapo na wengi tu..Kutomwezesha mzawa ni moja ya kuonyesha huna uchungu na nchi yako kwani nchi sio ardhi peke yake bali ni watu wanaoishi ktk ardhi hiyo.
 

Hizo ekari 50-100 kwa kila mchaga uchagani zitatoka wapi? Na kwa mtaji huu, huyo mchaga hataruhusiwa kwenda kuziomba Mahenge maana zitakuwa zimeishatengwa kwa wazawa wa kule! Na jee, huyo mzawa mwenye hizo ekari, akitaka kumkatia mtu wa kutoka nje ya sehemu ile, ataruhusiwa? Akiruhusiwa na baada ya muda mfupi tukikuta wageni kutoka sehemu nyingine ya nchi wanahodhi sehemu kubwa ya hiyo ardhi, tutawanyang'anya?

Tukumbuke tulinyang'anya maghorofa yote ya uhindini, tukaanzisha msajili wa majumba, tukagawiana wenyewe na leo yako wapi? Si wote tumewauzia wahindi na kwenda kubanana Kimara? Sharif Shamba nako tumeuza. Kariakoo tumeuza. Sasa walionunua wameendeleza tunalia wivu na kudai wanyang'anywe, tupewe ili tuwauzie tena!

Kwa mtaji huu, hatutafika.

Amandla.....
 

Mkuu, ungesema Ogah wala nisingekuandama. Ulitumia Patel kwa kumaanisha mhindi na ndiyo maana baadae ukaunganisha wahindi wengine wakina Rajan, Kugis na kadhalika. Hii uliiweka wazi ulipozungumzia kuwa viongozi wetu wako comfortable zaidi ku deal na MHINDI kwa masikitiko. Ungemweka Ogah kwenye mfano wako, usingeweza kusema hivi!

Ninavyoelewa mimi, patriot ni mtu mwenye loyalty na nchi yake. Hauwezi ukawa patriot bila ya kuwa loyal.

Tatizo linakuja tunapotumia neno mzawa kumaanisha mweusi. Si weusi wote wanaohitaji kuwezeshwa kama vile si watanzania wote wasio na rangi nyeusi wenye uwezo. Kwa nini tunang'ang'ania neno mzawa badala ya mtanzania kama hatumaanishi rangi? Ukweli ni kuwa wengi wetu ni wabaguzi ingawa hatutaki tuonekane hivyo!

Amandla.....
 
Hivi kwa nini lakini kuwe na upendeleo? Kwa nini kusiwe na fursa sawa kwa wote nikiwa na maana kila mtu awe na nafasi inayolingana na mwingine katika kufanikiwa kimaisha na akishindwa basi hana mwingine wa kumlaumu isipokuwa yeye mwenyewe....

Kwa maoni yangu mimi naona cha muhimu hapa ni kuwa au kujenga nidhamu ya kufuata utawala wa sheria na utungaji wa sheria nzuri zisizo za kibaguzi zitakazoenda sambamba na utawala huo. Tutakapoliweza hilo naamini kabisa tutakuwa tumejenga misingi ya usawa wa fursa kwa wote bila kuangalia uzaliwa, rangi, dini, jinsia ya mtu na mambo mengine kama hayo.

Does that make sense, common sense that is?
 

Way to go Rush! A conservative thinking...!
 
Way to go Rush! A conservative thinking...!

Are you trying to be funny or what..?

But seriously, doesn't it make sense to you or you think it's just pure hogwash? I don't know about you but it sure does make a whole lot of sense to me....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…