Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,984
Sikimbii hoja. Mimi ni mmoja katika hao ambao wanatakiwa kuwasaidia wenzake kujitoa katika umasikini. Isipokuwa mimi simlaumu mtu mwingine yeyote kwa mapungufu yangu. Naamini kuwa ninapaswa kujirekebisha na si serikali inipendelee dhidi ya mwenzangu tuliotofautiana rangi!
Amandla......
Fundi,
kufanikiwa wewe haimaanishi kuwa wengine wasiofanikiwa hawakujituma au hawajitumi. Kuna mambo mengi ambayo yamewakwaza hadi wakashindwa kufanikiwa.Na sababu kubwa ya watu wengi kushindwa kufanikiwa ni mfumo wetu wa uendeshaji serikali. Mathalani kila siku tunaimbishwa kuwa kilimo ni uti wa mgongo, na ama kwa hakika sekta hiyo imeajiri watanzania zaidi ya asilimia themanini(hapa namaanisha walioajiriwa na kujiajiri wenyewe).Na kwa sehemu kubwa hawa ndio wana matatizo makubwa pamoja na wamachinga ambao pia ni zao la kilimo chetu kukosa tija kwahiyo vijana wameamua kukimbilia mijini na kujiajiri kwa kuendesha maduka ya mikononi.Kwakuwa hupendi kusikia waarabu au wahindi wakitajwa, nakuomba niwatumie hapa kidogo.Je ni wangapi wanaotaabika na hizi shughuli za kilimo kama akina masanja, akina mkude na akina mwakifamba?Ndio maana tukasema hatuna sababu yoyote ya kuwakwamisha wale ambao tayari wamefanikiwa, ingawa miongoni mwa hao watanzania waasia wapo ambao hawajafanikiwa lakini nao bado hawatazuiwa kunufaika na huo uwezeshaji.Isipokuwa ni lazima tutilie mkazo kuwakwamua hawa wamatumbi ambao bado wengi sana ndio wenye hali mbaya.Mwenyewe Umekiri kuwa hawa jamaa wanasaidiana huko jamatini, kwahiyo wengi wao wanapata misaada toka kwa wenzao, je sisi wamatumbi tunawasaidiaje wenzetu?. Ndio sabau tukasema basi ni vizuri serikali yetu iweke utaratibu wa kuwasaidia hawa wamatumbi choka mbaya.