Sera ya Kuwawezesha watanzania weusi ni ya lazima?

hahahahaaaaa, ukiona mtu kaanza kwenda personal kuna kitu behind the scenes. Kama unataka asante omba nitakuwekea kwa kujilazimisha huku nikiangalia pembeni lol!

Hivi wee mama, ikifika wakati wa SHEREHE, na jirani yako kuna masikini, je huyo pia huwa unamnunulia SUTI au nguo kama unazowanunulia wanao ingawa wanao wako katika hali nzuri? Kukitanganzwa msaada wa nguo kutoka kiwanda cha ADIDAS basi na wewe unapeleka wanao wakafaidi vitu MADE IN GERMAN, unaona hilo ni sawa? Mie nafikiri hata Wahindi wenyewe kama akina SHIVJI kama wakiona Mpango kama huo watasema ".. Ni mpango mzuri acha na Mipingo nao waanze kuinuka maana wako chini sana kibiashara.".
Nimeshindwa kujua ulichowekea asante ni nini ndiyo maana nikakuweka kundi moja. VInginevyo kama ungeliandika mawazo yako katika hilo ningeliangalia msimamo wako na hapo kukuchanganya au kutokukuchanganya. Sina shida na asante na wala sina tatizo kuzitoa (nimekupa hapo juu Thanx) ... 🙂
 

Kama sijamtendea haki huyo binti wa kiNorway, samahani. Simjui na inabidi niamini kile unachokieleza juu yake. Kwangu mimi ni premature kuanza kumpigia debe kwa kusema tu kuwa ana nia ya kurudisha passport ya Norway. Mimi hata asipoirudisha na kuamua kwenda kujitolea Tanzania kama raia wa Norway atastahili pongezi. Lakini sitamsifia au kumshukuru hadi hapo atakapofanya hivyo.

Naam, hautakuwa wa kwanza kuniita VERY MUONGO. Kuweko mmoja au wawili hakubadilishi ukweli ( nionavyo mimi na nilivyoshuhudia) kuwa wahindi wengi ( sikutaja wasomali au wamalawi) walitiliwa ngumu kupata scholarship kwa dhana ya kuwa watakimbia nchi. Pengine siku hizi ambapo scholarship imekuwa biashara basi wanazipata kwa kupenyeza rupia. Wengine hata hivyo pengine wanapata kwa sababu tu ya utanzania wao maana si watendaji wote ambao ni wabaguzi au wapenda rushwa. Ubaguzi ninaouzungumzia mimi haukuwa kwenye sera bali ilikuwa ni maamuzi binafsi ya maafisa husika ambao wengi wao kama sio wote walikuwa hao tunaowaita wazawa. Kwani wakina Profesa Issa Shivji walitokea wapi?



Mbona unaji-contradict? Sasa huyo mwaarabu wa UDSM hana kwao? Kama wako wanaorudi basi kwa nini mnawatia wote kwenye kundi la huyo Mhindi wa Mohammed Enterprise?

Hapa tunajadiliana wala hatutakiwi kugombana. Sasa wewe kumwingiza Mama ati kwa sabau ametoa Thanks ndiyo unataka kugeuza haya yawe malumbano. Mbona hukumuona wengine kama Gamba la Nyoka bali unamwandama Mama? Asante haina maana ya kuwa aliyeitoa anaunga mkono kilichoandikwa. Asante ni kushukuru kwa kubandika kitu kilicho muhimu hata kama haukubaliana nacho.

Kutofautiana si lazima iwe kugombana. Naona mwenzangu unataka kunipeleka huko.

Kwa hali hiyo, naona heri tuishie hapa. Kama nilivyosema awali. Tukubali kutofautiana.

Nakutakia heri na mafanikio katika mwaka mpya wa 2009.

Amandla......
 
MJJ tuweke elimu ubaguzi hausaidii hasa ukizingatia Tanzania ni nchi masikini Solution ya Tanzania ni Elimu siyo biashara. Elimu italeta biashara lakini biashara pekee haisaidii nchi.

Nakubaliana na wewe Kamudu elimu ndiyo ufunguo wa maisha bila ya elimu hakuna maisha, Hata hivyo wazawa wengi wameweza kujikomboa katika biashara, miaka ya nyuma tulizoea kuwaona wa asia pekee katika biashara hasa hizi za maduka, lakini hivi sasa wazawa wengi ndiyo wafanya biashara tena wakubwa na wadogo hilo halina ubishi.
 
Fm,
Nimeandika kuwa WENGI WAO na SI WOTE (Wahindi, Waarabu).
Juu ya Mama ni kuwa nilitaka kumchokoza tu. Ndiyo maana nikamuandika. Kama umegundua hata mwenyewe anacheka...... ni katika kumalizia mwaka huu.
Usije ukaniita mbaguzi, HAPANA. Ila sema ni mtu ninayetaka USAWA. Mengineyo ni katika kueleweshana tu. Hamna CHOCHOTE zaidi ya hicho. Kama nilivyosema na umeandika ni kuwa "... hivi vitu huwa ni sera za siri za nchi. Utakuta zinafanywa na hutakuta zimeandikwa popote pale kama ile issue ya Ogondieki. Siwezi kupinga au kukubali juu ya wahindi kukataliwa kwenda kusoma,," Hivyo mie na wewe hatuna uwezo wa kubadili wala kuleta kitu kama hiki zaidi ya kusema "mimi muono wangu ni huu". Kama swala la elimu basi "kubagua Wahindi au Waarabu leo ningelipinga kwani Mipingo wengi wamesoma sana..." Tatizo langu ni kwenye BIASHARA TU.
Mwisho na mimi Fundi Mchundo mwenzio nikuombee Kila la kheri na fanaka katika mwaka ujao. Ukawe na Afya njema wewe a familia yako. Huko Sikonge twasema "Mwaka 2008 uwe mwaka mbaya kwako kuliko mwaka 2009".

Kwa Member wengine wachangiaji wa hii habari nasema HERI YA MWAKA MPYA 2009.
God Bless and check next year.
 

Ni ukweli usiopingika kuwa Watanzania wenye asili ya Asia wameanza kupitwa na wale Natives katika biashara kubwa.Hapa Mwanza Wachagga,Wanyantuzu Wakurya,Wahaya,Wasukuma wasio na asili ya Bariadi,Wajaluo wanatawala katika biashara kubwa za mahoteli,viwanda,maduka ya vipuri n.k.kitu ambacho miaka 40 iliyopita ilikuwa ndoto!

Kitu kizuri zaidi ni kuwa hawa weusi wanaheshimiana na wahindi na kujiona wapo katika lile tabaka la juu la wenye nazo.Wanawasiliana.wanafanya biashara na kjumuka katika sherehe mbalimbali wakijialika wenyewe kwa wenyewe kwa kuwa wanajiona tofauti na watu wengine.

Sasa wale wanounga mkono sera ya uzawa wanachokitaka ni kipi?Wanataka kuupiga vita umasikini kwa kutumia tu neno "uzawa".Hili neno litakuwa na maana ya kuwabagua aina ya watu wengine.

Neno uzawa lingeondoka na kutumika neno jingine lisilokuwa na chembechembe za ubaguzi.
 

Fundi pamoja na wachangiaji wote wa thread hii, kila mmoja ana mtazamo wake jinsi anavyodhani inafaa katika kuboresha maisha ya wamatumbi wenzake.Na kilichojitokeza hapa ni kuwa wengi wetu kama sio wote tunakubaliana kuwa kuna umuhimu wa kuwawezesha hawa wamatumbi, isipokuwa tunapishana ni kwa namna gani, kwa njia gani hawa wamatumbi wawezeshwe?nadhani pia hata tukiendelea kuelezea mawazo yetu hapa hatutafika mahali tukawa na common say.
Kwahiyo basi ni vizuri, kama ulivyosema TUKUBALIANE KUTOKUBALIANA au tukubaliane KUTOFAUTIANA. Lakini pia labda tujipe break kidogo ili kila mmoja aendelee kuyatafakari mawazo ya mwenzake na hata kuutafakari msimamao wake na pengine tunaweza kufika mahali TUKAKUBALIANA KUKUBALIANA.

Nimalizie kwa kuwatakia heri ya mwaka ujao(mpya?) wa 2009. Tumuombe sana Mungu atuwezeshe kuwa na bidii zaidi, nguvu zaidi,hekima na busara ili tuweze kukabiliana vilivyo na mazonge ya maisha, bila kusahau kuwa mwaka 2009 tunahitaji kusimama kidete kuhakikisha kwamba ufisadi ni agenda ya kudumu ili tuweze kuukomesha kabisa nchini mwetu.
"ENOKWI EGONGWE"
 

Mkuu FM nafikiri suala ni kuwawezesha wazawa na si kuwabagua wengine.MZAWA maana yake ni yule alizaliwa Tanzania na kutambuliwa kuwa ni mwananchi wa nchi hii.Ndio maana nika-argue kuwa kama kuna mzawa asiye mweusi, basi kupewa kipaumbele katika kuwezeshwa vile vile ni jambo la haki na msingi.
Just read my argument carefully.
Mkuu FM kwa taarifa yako Jeshi letu ni la WAZAWA TU kwa definition ya hapo juu.Kwa hiyo kama wewe ni Mpunjabi, Mmmanga, Mwarabu ,Mkuria,Mdengereko au Muha bado ni mzawa tu kama umezaliwa na kutambuliwa kuwa mwananchi wa nchi hii.
 

Mimi nimesuuzika na jinsi hoja hii ilivyokuwa hot na jinsi wachangiaji walivyojitahidi kutetea hoja zao.kikubwa nilichojifunza ni kwamba wote tulikuwa na haja ya kuona kuwa wanyonge nao wanapewa fursa ya kujiendeleza.

Kwangu mimi maskini ni maskini tu akiwa mweusi au mweupe au wa njano.Ili kumwezesha kiuchumi Serikali na vyombo vya fedha inabidi vitafute sera ya uwezeshaji wa Watanzania maskini.

Nawatakia kila la kheri kwa mwaka 2009! happy New Year!!!
 

kwa hiyo Watanzania waliozaliwa nje ya mipaka ya Tanzania,mfano wale waliozaliwa pindi wazazi wao wakiwa nje ya nchi kutafuta maisha wasiwezeshwe?, maana kwa jinsi ulivyosema hapo unamaanisha mzawa ni Mtazania yule aliyezaliwa Tanzania tu!
 
kwa hiyo Watanzania waliozaliwa nje ya mipaka ya Tanzania,mfano wale waliozaliwa pindi wazazi wao wakiwa nje ya nchi kutafuta maisha wasiwezeshwe?, maana kwa jinsi ulivyosema hapo unamaanisha mzawa ni Mtazania yule aliyezaliwa Tanzania tu!

Kila wakijaribu ku-spin inabaki pale pale. Kama watanzania wote ni wazawa kuna haja gani ya kutumia neno mzawa? Kama kuzaliwa Tanzania ndiyo criteria, je wale waliozaliwa nje kama Mkuu Gamba la Nyoka alivyouliza?

Hata tuipake parfyum vipi, sera inabaki kunuka ubaguzi!

Amandla.....
 
kwa hiyo Watanzania waliozaliwa nje ya mipaka ya Tanzania,mfano wale waliozaliwa pindi wazazi wao wakiwa nje ya nchi kutafuta maisha wasiwezeshwe?, maana kwa jinsi ulivyosema hapo unamaanisha mzawa ni Mtazania yule aliyezaliwa Tanzania tu!

Sasa hili ni suala la immigration na uraia,kwa utaratibu wa kawaida kabisa aliyezaliwa nje hata kama wazazi wake ni waTanzania anakuwa na uraia tata kidogo.Mi si mtaalam wa uhamiaji lakini ninavyofahamu kidogo ni kuwa mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania anaweza kuwa aidha ni raia wa Tanzania au raia wa nchi alimo zaliwa. Hapo suala ni uchaguzi wa mzaliwaji(kwa kawaida akifikisha miaka 18)
Ukizaliwa nje ya Tanzania si automatic kuwa ni mzawa kuna kautaratibu hapo,hata hivyo kwa mwana JF anaye fahamu kwa undani masuala ya uhamiaji, msaada tutani.
 

Ndio maana sisi tukaja na hoja inclusive, "SERA YA KUMWEZESHA MTANZANIA". au tukicheza na maneno kidogo tunaweza kuita "SERA YA KUMWEZESHA RAIA WA TANZANIA". sera hii ina manufaa mengi zaidi, kwanza siyo ya kibaguzi, haijali rangi ya mtu, dini wala kabila, maadamu awe Mtanzania mwenye kuhitaji kuwezeshwa atawezeshwa tu, hakuna atakaye lalamika kusema kwamba Mimi ni mtanzania lakini sijawezeshwa kwa sababu mimi ni Mtanzania mwenye asili ya Kihindi, au sijawezeshwa kwa sababu nasubiri wawezeshwe Watanzania weusi kwanza ndo na mimi nifikiriwe.

Tukifuata sera ya uzawa itawagawa Watanzania katika kundi la wazawa na wasio wazawa, japo wazawa ndo wengi, itakuwa siyo sera yenye mlengo wa kitaifa ambalo kila siku tunahangaika kulijenga, taifa linalojengwa na wazawa na wasio wazawa lakini wote under one nation TANZANIA. sipingi wazawa kuwezeshwa, nataka Watanzania wote wanaohitaji kuwezeshwa wawezeshwe.

kwa hiyo naconclude kwa kusema "tufuate sera ya kumwezesha Mtanzania".
kutunga sera ukaiita "sera ya kumwezesha mzawa", halafu ukaamini hiyo ni sera ya kumwezesha Mtanzania ni kujidanganya, kwa sababu si kila Mtanzania amezaliwa Tanzania"
 

Quite agree on the substance , disagreement yetu ilikuwa just semantics, GOOD DAY AND HAPPY NEW YEAR 2009!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…