Uchaguzi 2020 Sera ya majimbo itaua utaifa na uzalendo

Uchaguzi 2020 Sera ya majimbo itaua utaifa na uzalendo

dndagula

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
1,602
Reaction score
1,650
Nimesikia chama kimoja kinazungumzia nchi kuigawa kwenye majimbo ya kiutawala na uendeshaji. Kwangu mimi kwa nchi ambayo imekuwa kwenye utawala wa mikoa kwa miaka zaidi ya 50 na kwa mfumo wa kugawana mapato kupitia serikali kuu na serikali za mitaa kwa baadhi ya mapato haileti mantiki kubadili mfumo kwenda kwenye majimbo ambayo yanaweza kuua utaifa na kuleta mfarakano. Mfumo wa sasa unaondoa u-mimi na maendeleo ya uchumi yanayopishana- Regional economic imbalances - ambao utaacha baadhi ya maeneo kwenye umasikini mkubwa. Baadhi ya athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na:

1. Maeneo yenye raslimali kidogo kuendelea kuwa maskini na maeneo mengine kuwa tajiri na hivyo kuwa na mchango mdogo wa GDP

2. Ajira ndogo kwenye baadhi ya maeneo yenye raslimali chache na hivyo ongezeko la idadi ya watu kwenye maeneo yenye utajiri wa raslimali

3. kila jimbo kuwa na sheria zake za kiutawala, bunge dogo, polisi nk hali inayoweza kujenga mwelekeo wa kujitenga. Rejea matatizo yakujitenga kwa Biafra Nigeria miaka ya nyuma.

4. Nchi zenye majimbo mf Msumbiji hazina hakikisho la maendeleo endelevu kuzidi ambazo hazina utaratibu huo ie Tanzania

5. Mfumo huo utakuwa na gharama kubwa kuuanzisha

Kimsingi hadi sasa mfumo uliopo hauna shida changamoto kubwa ni kuweka mifumo mizuri ya udhibiti matumizi na mapato ya serikali kwa kuyagawa kwa haki ili kila eneo la serikali liweze kunufaika. Na hususani kuimarisha mfumo wa Halmashauri uweze kukabiliana na changamoto za kiuchumi kwa kila eneo. Iwapo kuna changamoto za mgawanyo sawia basi tupitie upya sera na sheria zetu ndani ya mfumo uliopo tuboreshe.

6. Hata hivyo, Kwa maoni yangu badala ya utawala wa majimbo ni afadhali kuweka kanda za kiuzalishaji ili kuchochea uchumi wa kimaeneo kulingana na mazingira ya kiuchumi na uzalishaji kwa kila eneo.
 
Maadhimio ya AU nchi zote za Africa ziliazimia hakuna nchi kujitenga na yeyote atakayeleta habari ya kujitenga jeshi la AU litamsambaratisha kwa hiyo hoja yako ya tatu umeipresent kwa sababu huna unalolifahamu
 
Uzalendo upi?Huu?[emoji116]
5430210.jpg
 
Ukiangalia kwa makini utaona CCM ndio inatengeneza mazingira ya watu kutaka majimbo.

Rais anasema kama huchagui chama chake hakuna maendeleo. Kuna maana gani kwa wakazi wa Mbeya Mjini kulipa kodi zoooote na wasipate maendeleo badala yake zipelekwe kwa wanaompenda Rais na chama chake?
 
Mkuu umewahi kuwaza kuhusu hii sera ya ukanda? Kanda ya ziwa ni untouchable, ni kipaumbele katika maendeleao na pia mpango wa serikali kwa sasa ninkuifanya iwe kanda ta utalii ili kuinua uchumi

Kuna mikoa ambayo imebarikiwa vivutio vya utalii lakini haijapewa kipaumbele kwa sababu rais hatokei kanda hizo

Acheni upupu muelimisheni mgombea wenu ajifunze kuwapa wananchi wote haki sawa bila kuwabagua kikanda la sivyo ataishia kufokafoka tu majukwaani
 
SWALI NI: JE, MFUMO WA MAJIMBO UTALETA UKABILA NA KUFANYA BAADHI YA SEHEMU TANZANIA KUTOKUWA NA MAENDELEO?

Amani iwe nanyi wadau!

Leo napenda kuwajibu wana CCM wanaosema mfumo wa Majimbo utachochea ukabila na kusababisha baadhi ya maeneo kutokuwa na maendeleo,

Ukweli ni kuwa kamwe mfumo wa majimbo hautaleta ukabila na kamwe hautoleta kudumaa kwa maendeleo kwenye baadhi ya sehemu kama propaganda za CCM zinavyosema! Hii ni kwa sababu zifuatazo;

1. Jimbo la Kati- Mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora na Morogoro.
Mikoa hii ina utajiri mkubwa wa mazao kama Tumbaku, Zabibu, Alizeti, Karanga, Asali na Mtama, Mpunga,Ndizi na Mahindi(vya mkoa wa Morogoro) Haya mazao tukipata viongozi wenye akili sio hawa wa CCM yataendelezwa vizuri na kuingiza mapato makubwa kwenye jimbo hili la kati.

Kuna uhitaji mkubwa sana wa Karanga na Asali kwenye masoko ya Asia na Ulaya. Haya mazao yakiendelezwa kisasa na kibiashara jimbo hili litanyanyuka mno kiuchumi. Hata viwanda vya mvinyo tu Dodoma vikiendelezwa na kutangazwa vizuri na mvinyo ukitengenezwa mzuri mapato

Pia kwenye jimbo hili kuna maliasili mbalimbali za wanyama kutokana na mapori ya akiba kama swagaswaga, manyoni na mapori ya Tabora ambayo pia yana tembo wengi na mbao nyingi. Hivi vitu vikiendelezwa na kutangazwa vizuri vitakuwa source kubwa ya mapato kutokana na uwindaji na utalii. Haya pia ni mapato makubwa sana.

Mkoa wa Morogoro una mbuga za wanyama kama mikumi, udzungwa na nyingine nyingi ambazo pia zitaleta mapato ya utalii.

Pia Kuna madini Kama dhahabu mikoa ya Tabora na Singida na Morogoro ambayo yakiendelezwa vizuri yataketa mapato makubwa sana kwenye maeneo haya. Hapo sijaweka biashara za mifugo, wanyama na viwanda ambavyo navyo vipo na vitakuwepo kwenye jimbo hili.

Kwa hiyo dhana ya Jimbo la Kati kuwa masikini si kweli.

2. Jimbo la Mashariki- Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Pwani
Jimbo hili chanzo kikuu cha Maputo kitakuwa Bandari, Viwanda na Biashara. Kodi nyingi itakusannywa kutoka maeneo haya na kwa kweli itaendeleza kweli jimbo hili.

3. Jimbo la Kusini- Mikoa ya LINDI, Mtwara na Ruvuma
Jimbo hili lina utajiri mkubwa wa gesi na mazao ya korosho na mbaazi bila kusahau viwanda, bandari na uvuvi. - Hili jimbo litakuwa na na mapato makubwa sana ambayo yatajenga shule bora, hospitali, madawa, kujenga barabara nzuri na makazi bora.

Pia jimbo hili litakuwa na mapato ya utalii kutokana na hifadhi ya Selous na mapori ya akiba ya mkoa wa Ruvuma.

4. Jimbo la Nyanda za Juu kusini- Mikoa ya Iringa, Njombe,Songwe na Mbeya
Jimbo hili ndo mzalishaji mkuu wa chakula kinacholisha Tanzania, Afrika ya kati na Afrika mashariki. Kilimo na Biashara ya Chakula kitaingiza mapato makubwa sana kwenye jimbo hili. Biashara pia ya mbao na utalii kutokana na hifadhi za kipengele, Ruaha, Kitulo na Rungwe vitaingiza mapato makubwa sana kwenye jimbo hili.

Mipaka ya Zambia na Malawi pia itaingiza mapato makubwa kutokana na biashara bila kusahau viwanda na kilimo cha mashamba makubwa ya mpunga, maparachichi, nyanya, chai na miti.

5. Jimbo la Magharibi- Mikoa ya Katavi, Rukwa, Kigoma na Kagera- Mikoa hii ina utajili wa kilimo hasa cha mazao ya mahindi, tumbaku, mawese, miwa pamoja na miti pia. Pia ina uvuvi wa maziwa ya Tanganyika na Victoria.

Mikoa hii pia ina utalii wa mbuga za wanyama kama hifadhi za Gombe, Kimisi, Katavi, Mto Maragarasi pamoja na biashara kubwa na kodi katika mipaka ya nchi za Congo( Bandari) , Burundi, Rwanda na Uganda! Itoshe tu kusema kuwa jimbo hili pia litakuwa na mapato mengi sana ambayo yataboresha miondombinu ya barabara, hospitali , mashule na huduma za Maji safi na salama!!

6. Jimbo la Kaskazini- Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Mara.
Jimbo hili litakuwa na na chanjo kikuu cha mapato ambacho ni utalii na pia madini ya mikoa ya Arusha, Manyara na Mara. Utalii wa mbuga za kilimanjaro, Ngorongoro, Serengeti na Manyara utaingiza pesa nyingi sana za kuboresha miondombinu na huduma za msingi

Biashara pia na kodi kwenye mipaka ya Kenya kwa sehemu za holili,Silali na Arusha italeta mapato mengi Sana. Na hapa hujaweka kilimo cha ndizi, tangawizi na mifugo bila kusahau viwanda.

7. Jimbo la Kanda ya Ziwa (Victoria)- Mikoa ya Simiyu, Geita, Shinyanga na Mwanza.
Jimbo hili ndo kitovu cha madini Tanzania. Pia lina mbuga na mapori ya akiba mengi bila kusahau viwanda na biashara ambavyo vitaingiza napata mengi sana na kuleta impact kubwa sana kwenye uchumi. Uvuvi pia utaleta mapato mengi sana.

Dhana ya ukabila haiwezi kupata nguvu kwenye mfumo huu kwa sababu Kuna mchanganyo mkubwa wa makabila kwenye majimbo haya!

Pia chini ya mfumo huu kila mwananchi atawajibika kufanya kazi halali na kujituma kwa sababu atajua bila kufanya kazi hawezi endelea na sehemu yake haiwezi kufanya vizuri katika huduma za msingi.

Chini ya mfumo huu pia hakutakuwa na unyanyasaji wa wananchi kwa sababu wananchi watakuwa wanajua kuwa Mapato yao ndio yatakayowaletea maendeleo!

Viongozi pia watawajibika moja kwa moja kwa wananchi na kamwe hawatofuja mali kwa wananchi wala kuwagawa kwa misingi ya kikabila au kichama kwenye maendeleo.
 
Salamu kwako Tundu Antiphas Lissu, Shalom,

Leo napenda kukwambia rasmi kuwa , Kura yangu iko kwako! Na hii ndo sababu yangu kuu ya kukupa kura!

Katika maisha yangu nimekuwa nikifanya utafiti sana juu ya dhana ya umasikini wa watanzania na Tanzania kwa ujumla, Moja ya sababu ambayo niligundua kwenye utafiti wangu ni kuwa Tanzania tuna mfumo mbovu sana wa utawala ambao vyovyote vile hatuwezi kuendelea kwa mfumo huu!

Mfumo huu ninaousema ni mfumo kuwa fedha zote za watanzania zinakusanywa na kuwekwa chini ya mtu mmoja( raisi ambayo yeye ndo anayeamua kuwa hizo fedha zigawanywe kivipi)

Madhara ya mfumo huu ni kuwa umeondoa uwajibikaji kwa wananchi na viongozi, umeondoa ubunifu kwa wananchi na viongozi na mwisho umepelekea tabia ya ombaomba na unafiki kwa wananchi na viongozi

Mfumo huu pia umechochea ufisadi wa kiwango kikubwa sana kwa wananchi na viongozi na kama Kuna mtu anabisha Leo hii aniambie maisha ya ukwasi wanayoishi maraisi wastaafu yametokana na nini???

Hapa Tanzania hakuna raisi mstaafu mwenye maisha ya utajiri wa kuwaida. Wengi wana utajiri mkubwa wa real estate, kilimo kikubwa na hata pia makampuni makubwa ya uzalishaji. Na kibaya ni kuwa vyote hivi huwa wanavipata wakiwa maraisi. Sababu ya haya yote ni kuwa tumekuwa na mfumo wa kuziweka fedha zote za nchi chini ya mtu mmoja.

Leo hii raisi ni kama Mungu hapa Tanzania. Kila aendapo watu ni kulia shida, awafanyie hiki na awaletee hiki, haya yote ni kwa sababu ya mfumo mbovu tulionao ambao umeondoa uwajibikaji na ubunifu kwa watanzania na viongozi wetu

Kwa nini Mfumo wa Majimbo ndo suluhisho wa haya yote?
1. Mfumo wa majimbo utafanya hela zote zinazokusanywa kwenye sehemu husika zitumike kwa matakwa ya wananchi wa sehemu husika mf. Kujenga barabara , hospitali, shule bora na huduma bora za Maji na umeme!! Hili litafanya wananchi wasiwe wajinga kwa viongozi wao na kamwe was iwe ombaomba na watu wa kujipendekeza kwa viongozi wao.

2. Mfumo wa majimbo utachochea ubunifu kwa wananchi kufanya shughuli mbalimbali bora za uzalishaji ili majimbo yao yakusanye fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo yao.

Kama jimbo husika linategemea kilimo basi wananchi wa hilo jimbo watafanya kilimo bora na watakifanya cha biashara ili wapate mapato mazuri ya kuendeleza jimbo lao kimiundombinu na Pia kimaendeleo. Hakuna sehemu watu watalala au kuwa wazembe na watakuwa wakali kwa viongozi wao kuwahamasisha wawe agressive kwenye kubuni miradi bora ya maendeleo kwa maendeleo yao.

Mfumo huu utatengeneza wananchi wanaojiamini na Kuwajibika kweli katika kutunza rasilimali zao ili ziwasaidie wao na uzao wao. Wananchi hawatakuwa wazembe na watawawajibisha kweli viongozi wasio wabunifu kwenye kutengeneza vyanzo vya mapato kwa sababu watakuwa wanajua bila vyanzo vya mapato bora na vya uhakika kwenye maeneo yao basi watakuwa nyuma kimaendeleo na hawataweza kunsurvive.

Mfumo wa majimbo utafanya kama sehemu Kuna mbuga za wanyama basi wananchi wa maeneo husika wazitunze rasilimali kweli kwa sababu watajua kweli bila mbuga hizo utalii utakufa na hawatapata mapato ya kulipa mishahara wafanyakazi wao, kujenga barabara na mitaa bora, kuhudumia Bima za afya na madawa hospitali. Kwa iyo Kama jimbo litategemea utalii basi watautunza na kuuthamini kweli utalii.

Kama jimbo linategemea viwanda au biashara basi jimbo hilo litatunga Sera bora ili kuhamasisha uwekezaji mkubwa wa viwanda na biashara kwa sababu wananchi wa sehemu husika watajua bila hivyo basi hawawezi pata mapato ya kununulia dawa, kupata Maji safi na salama na kujenga barabara nzuri!

Kama jimbo husika linategemea kilimo na migodi basi wananchi wa viongozi wa maeneo husika wataumiza kichwa kuweka Sera bora katika hayo maeneo ili kuhakikisha zinawapatia mapato makubwa ya kufanya miradi ya maendeleo. Watu watajiona kweli kuwa wao ni sehemu sahihi ya maendeleo husika.

Imefika wakati watanzania lazima tuseme kuwa mfumo wa utawala wa Chama cha mapinduzi, umechochea sana ufisadi, umasikini, kujipendekeza, uzembe, ubabaishaji na kutowajibika kweli kwa Watanzania!!!

Mfumo huu wa sasa umefanya watanzania tudharauliwe na viongozi na kuendeshwa Kama watoto wadogo kuwa tusipowachagua watu wao basi tusahau maendeleo kwa sababu wao ndo wanaamua hela zetu wazigawe vipi!! Hii sio sawa kabisa

Mfumo huu wa sasa umesababisha watu kuwa ombaomba na watumwa kwenye nchi yao kuwa kila wakimuona Raisi basi wamnyenyekee kama Mungu n kumuomba hiki na kile. Kama Raisi tunaomba Maji, barabara, umeme na shule bora

Kwa maendeleo ya kweli ni lazima Watanzania tuamue kwenye uchaguzi huu kumchagua Tundu Antiphas Lissu ili atubadirishie mfumo.

Hamasisha watu wengi zaidi kumchagua Lissu na Chadema kwa maendeleo ya kweli ya Tanzania na Watanzania!

Sambaza kwa watu wengi zaidi waelimike pia!!

Asanteni!
Lord denning.
 
Maadhimio ya AU nchi zote za Africa ziliazimia hakuna nchi kujitenga na yeyote atakayeleta habari ya kujitenga jeshi la AU litamsambaratisha kwa hiyo hoja yako ya tatu umeipresent kwa sababu huna unalolifahamu
AU ina jeshi? Lini na wapi hata kulinda amani tu hapa Africa uliona AU wamefanya bila msaada mkubwa wa UN na US? Anzia Congo, Mali Somalia, Africa ya kati n.k. kila panapohitajika jeshi la kulinda amani kila kitu iwe logistics, gharama nk huwa ni aidha UN au US na mataifa ya magharibi.
 
AU ina jeshi? Lini na wapi hata kulinda amani tu hapa Africa uliona AU wamefanya bila msaada mkubwa wa UN na US? Anzia Congo, Mali Somalia, Africa ya kati n.k. kila panapohitajika jeshi la kulinda amani kila kitu iwe logistics, gharama nk huwa ni aidha UN au US na mataifa ya magharibi.
Acha kubisha kitu usichokifahamu mkuu tafuta habari ziko mtandaoni, AU haina jeshi rasmi, ila ukitokea mzozo wa kundi fulani kugawa nchi, kila mwanachama wa AU atatoa wanajeshi wake kwenda kupambana na kundi la uasi!
 
Kwa hiyo nchi zilizoendelea hawana utaifa na uzalendo?

Mnataka hii nchi iwe pale pale isiendelee ili muendelee kupiga pesa.
Yaani wewe kwa akili yako unajiamini kabisa kuwa nchi haijaendelea, kama WB na IMF wameiweka tanzania kufika uchumi wa kati wewe nani useme haijapata maendeleo.

Uthibitisho wa ubovu wa sera yenu ya MAJIMBO mtauona kuanzia tarehe 28/octoba ndiyo utawajua watanzania kuwa ni wapenda utaifa na uzalendo. kufikia tarehe 30 octoba, Lissu atakuwa amekimbia nchi kwa aibu, lakini kwa kuwa anahitajika kujibu hoja pale mtaa wa bibi titi atashuhudia aibu yake akiwa hapahapa.
 
Back
Top Bottom