Mkuu, hii Sera ni Nzuri Ukiwa katika Jimbo, ama mkoa wenye Resources nyingi na kutoshereza kujiletea maendeleo, swali langu ni kwamba, Kwa kuwa mikoa yenye utajiri wa lasirimali za kutosha huwenda zisifikie hata mikoa 8, hiyo mikoa mingine wataweza kuvumilia umaskini Wao uliopo ktk mikoa Yao ukiwemo mkoa wa Singida anakotokea Raisi wa mitandaoni?
Sera ya majimbo, ni Nzuri Sana mkiwa na eneo kuuubwa la nchi, nchi yetu ni ndogo na inaweza kulinganishwa na Jimbo moja tu la Taxes Maerekani, maana yake Ni kwamba, Jimbo la Taxes, utajiri ulio katika Baadhi ya maeneo yake, huufunika umaskini wa maeneo mengine yasiyokuwa na utajiri wa rasilimali
Je, hapa, mtaigawaje hii nchi ili kwamba, Kwa mikoa hiyo isiyozidi minane iingizwe kwenye hayo majimbo hata yasiyokuwa na kitu ili sasa kuumeza huo umaskini wa mikoa zaidi ya ishirini+
Hata ukasema uigawe kikanda, Naihofia kanda ya Kati, Kwa kuwa mikoa yake ni myeupe na inakuwaga na njaa sana
[/QUSi lazima mapato yote yarudishwe hapo ila aslimja 75 iachwe eneo husika likachangie serikali juu ili wao wagawe kulingana na hitaji la dhati la eneo fulani na kwa vigezo maalumu ama hakika sera ya majimbo ndio Njia pekee ya kurahisisha maendeleo kwa sasa