Uchaguzi 2020 Sera ya Majimbo ndio mkombozi wa Taifa

Truth!
 
Salamu kwako Tundu Antiphas Lissu, Shalom,

Leo napenda kukwambia rasmi kuwa , Kura yangu iko kwako! Na hii ndo sababu yangu kuu ya kukupa kura!

Katika maisha yangu nimekuwa nikifanya utafiti sana juu ya dhana ya umasikini wa watanzania na Tanzania kwa ujumla, Moja ya sababu ambayo niligundua kwenye utafiti wangu ni kuwa Tanzania tuna mfumo mbovu sana wa utawala ambao vyovyote vile hatuwezi kuendelea kwa mfumo huu!

Mfumo huu ninaousema ni mfumo kuwa fedha zote za watanzania zinakusanywa na kuwekwa chini ya mtu mmoja( raisi ambayo yeye ndo anayeamua kuwa hizo fedha zigawanywe kivipi)

Madhara ya mfumo huu ni kuwa umeondoa uwajibikaji kwa wananchi na viongozi, umeondoa ubunifu kwa wananchi na viongozi na mwisho umepelekea tabia ya ombaomba na unafiki kwa wananchi na viongozi

Mfumo huu pia umechochea ufisadi wa kiwango kikubwa sana kwa wananchi na viongozi na kama Kuna mtu anabisha Leo hii aniambie maisha ya ukwasi wanayoishi maraisi wastaafu yametokana na nini???

Hapa Tanzania hakuna raisi mstaafu mwenye maisha ya utajiri wa kuwaida. Wengi wana utajiri mkubwa wa real estate, kilimo kikubwa na hata pia makampuni makubwa ya uzalishaji. Na kibaya ni kuwa vyote hivi huwa wanavipata wakiwa maraisi. Sababu ya haya yote ni kuwa tumekuwa na mfumo wa kuziweka fedha zote za nchi chini ya mtu mmoja.

Leo hii raisi ni kama Mungu hapa Tanzania. Kila aendapo watu ni kulia shida, awafanyie hiki na awaletee hiki, haya yote ni kwa sababu ya mfumo mbovu tulionao ambao umeondoa uwajibikaji na ubunifu kwa watanzania na viongozi wetu

Kwa nini Mfumo wa Majimbo ndo suluhisho wa haya yote?
1. Mfumo wa majimbo utafanya hela zote zinazokusanywa kwenye sehemu husika zitumike kwa matakwa ya wananchi wa sehemu husika mf. Kujenga barabara , hospitali, shule bora na huduma bora za Maji na umeme!! Hili litafanya wananchi wasiwe wajinga kwa viongozi wao na kamwe was iwe ombaomba na watu wa kujipendekeza kwa viongozi wao.

2. Mfumo wa majimbo utachochea ubunifu kwa wananchi kufanya shughuli mbalimbali bora za uzalishaji ili majimbo yao yakusanye fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo yao.

Kama jimbo husika linategemea kilimo basi wananchi wa hilo jimbo watafanya kilimo bora na watakifanya cha biashara ili wapate mapato mazuri ya kuendeleza jimbo lao kimiundombinu na Pia kimaendeleo. Hakuna sehemu watu watalala au kuwa wazembe na watakuwa wakali kwa viongozi wao kuwahamasisha wawe agressive kwenye kubuni miradi bora ya maendeleo kwa maendeleo yao.

Mfumo huu utatengeneza wananchi wanaojiamini na Kuwajibika kweli katika kutunza rasilimali zao ili ziwasaidie wao na uzao wao. Wananchi hawatakuwa wazembe na watawawajibisha kweli viongozi wasio wabunifu kwenye kutengeneza vyanzo vya mapato kwa sababu watakuwa wanajua bila vyanzo vya mapato bora na vya uhakika kwenye maeneo yao basi watakuwa nyuma kimaendeleo na hawataweza kunsurvive.

Mfumo wa majimbo utafanya kama sehemu Kuna mbuga za wanyama basi wananchi wa maeneo husika wazitunze rasilimali kweli kwa sababu watajua kweli bila mbuga hizo utalii utakufa na hawatapata mapato ya kulipa mishahara wafanyakazi wao, kujenga barabara na mitaa bora, kuhudumia Bima za afya na madawa hospitali. Kwa iyo Kama jimbo litategemea utalii basi watautunza na kuuthamini kweli utalii.

Kama jimbo linategemea viwanda au biashara basi jimbo hilo litatunga Sera bora ili kuhamasisha uwekezaji mkubwa wa viwanda na biashara kwa sababu wananchi wa sehemu husika watajua bila hivyo basi hawawezi pata mapato ya kununulia dawa, kupata Maji safi na salama na kujenga barabara nzuri!

Kama jimbo husika linategemea kilimo na migodi basi wananchi wa viongozi wa maeneo husika wataumiza kichwa kuweka Sera bora katika hayo maeneo ili kuhakikisha zinawapatia mapato makubwa ya kufanya miradi ya maendeleo. Watu watajiona kweli kuwa wao ni sehemu sahihi ya maendeleo husika.

Imefika wakati watanzania lazima tuseme kuwa mfumo wa utawala wa Chama cha mapinduzi, umechochea sana ufisadi, umasikini, kujipendekeza, uzembe, ubabaishaji na kutowajibika kweli kwa Watanzania!!!

Mfumo huu wa sasa umefanya watanzania tudharauliwe na viongozi na kuendeshwa Kama watoto wadogo kuwa tusipowachagua watu wao basi tusahau maendeleo kwa sababu wao ndo wanaamua hela zetu wazigawe vipi!! Hii sio sawa kabisa

Mfumo huu wa sasa umesababisha watu kuwa ombaomba na watumwa kwenye nchi yao kuwa kila wakimuona Raisi basi wamnyenyekee kama Mungu n kumuomba hiki na kile. Kama Raisi tunaomba Maji, barabara, umeme na shule bora

Kwa maendeleo ya kweli ni lazima Watanzania tuamue kwenye uchaguzi huu kumchagua Tundu Antiphas Lissu ili atubadirishie mfumo.

Hamasisha watu wengi zaidi kumchagua Lissu na Chadema kwa maendeleo ya kweli ya Tanzania na Watanzania!

Sambaza kwa watu wengi zaidi waelimike pia!!

Asanteni!
Lord denning.
 
Mkuu, umeongea madini Sana,

Nchi yetu INA Baadhi tu ya mikoa michache sana iliyo na utajiri wa rasilimali

Ukisha igawa kimajimbo, tayari umebariki utajiri wa Gesi usivuke kwenda mikoa mingine ispokuwa kibiashara, madini Nayo vilevile, mbuga za wanyama nazo hivyohivyo ziwanufaishe wa hukohuko, vivyo hivyo mapato yatokanayo na bandari zetu, sasa jiulize, Mapato yatokanayo na bandari Kwa mjibu wa Rais wa Lwanda, yanatosha kuendeshea nchi yake na ya Tanzania, utajiri huo wote uwe Tu mikoa ya Pwani pekee

Madini kule Geita, Kwa mjibu wa takwimu za Mapato ya Serikali 2019 yamevunja rekodi ya Mapato yote ya utalii Kwa miaka yote

Utajiri huo uwe Geita pekee, hawaoni kwamba, nchi yetu itawalazimisha watu wengi kukuingiza kwenye magenge ya kiharifu wakitafuta kitu
 
Mkuu hawa watu wamezidiwa na ushabiki,Sasa chochote atakachosema Yule Rais wa manyumbu, wao watasapoti na kutafuta namna ya kujifanya kionekane kizuri hata Kama sio. Wanafanya hivyo eti kuikomoa CCM😂😂.Kwahiyo mkuu wala usihangaike na Hawa jamaa.Msanii mmoja, simkumbuki jina, aliwahi kuimba "kumuelimisha chizi utajipa kazi" 🚶
 
Well Said ..Watanzania Tusijidanganye kuna wa kutuvusha zaidi ya Sisi wenyewe kuungana na kusupport juhudi za dhati za Viongozi wetu kama alivyo Dr.Magufuli
Hawa nyumbu wa Chadema,hawawezi kukuelewa ndugu yangu.
 
tupe na pointi za kusapotu hoja yako
 
S
 
Lugha yetu imeshatuunganisha tayari, Suala la majimbo limebeba na historia za maisha ya wakenya hapo nyuma, Usiogopr Ney waambie wenzako Majimbo ndio habari
Ndoto za Asubuhi....Kenya wameishia kutengeneza Matabaka ya walionacho na wasionacho
nxa
 
Sana, Yaani Lisu mmoja ni sawa na CCM wote nchi nzima. We hushangai wote wanajibu hoja za Lisu tu ndo ujue amewazidi sana kwa akili
Oh! Kumbe ndio maana unashabikia sera za majimbo.

Ni mfuasi wa mt fulani fulani au unaweza ukawa wewe mwenyewe ila jina ndio ANONYMOUS.
 
Kuna mtu anatoka kifua mbele anasema singida ina rasilimali ya Alizeti...are sunflowers a natural resources?kweliiiii kabisaaaa...
 
Umenena vyema mkuu.....Kura ni kwa Lisu
 
Unazungumzia wananchi wapi? Labda wewe na jiwe
 
Umeongea utumbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…