Nathanaelsumbi
New Member
- Aug 4, 2022
- 1
- 0
SERA YA MFUMO MPYA WA ELIMU.
Binafsi, Kama kijana naumia sana kuona watoto, vijana na watu wengine kwenye jamii zetu wanapoteza uwezo wao wa kipekee walio zaliwa nao eti kisa, MFUMO WA ELIMU ULIOPO SASA.
MFUMO WA ELIMU ULIOPO SASA, Ni Mfumo ambao, haujatengenezwa kwa ajili ya kila mtoto aliyepo kwenye jamii zetu, bali ni Mfumo wa Elimu ambao ni maalumu kwa ajili ya baadhi ya watoto na sio watoto wote, Nasema ivyo kwa sababu, Elimu ambayo inatolewa huko mashuleni (Mfano, Subjects zilizopo huko na namna ambavyo mtoto anaandaliwa), imekaa katika mazingira ya kumtengeneza mtoto kuwa vile ambavyo Mfumo wa Elimu wenyewe unavyotaka na sio vile ambavyo mtoto anataka. Kwa maana nyingine ni kwamba, ni Mfumo Wa Elimu ambao unawahusu Sana watoto wenye ndoto za kuwa wahandisi, madaktari, marubanii, walimu, wanasheria, wafanya biashara na taaluma zingine zinazo endana na izo, na kuwaacha watoto wenye Vipaji, ndoto na kiu kubwa ya kuwa wanamichezo hodarii, wasanii mahirii na talanta nyinginezo.
Moja ya mfano mzuri ambao unaonyesha kuwa Mfumo Wa Elimu uliopo sasa ni changamoto kubwa kwenye jamii zetu ni pale ambapo moja kati ya matajiri wakubwa kama vile Gary Vee alipo ulizwa kwa nini alifeli shule, akajibu “sikushindwa masomo ya shuleni bali mfumo wa shule ulishindwa kutambua uwezo wangu” kwaiyo hii inaendelea kudhiilisha kwamba Mfumo Wa Elimu uliopo sasa, Ni tatizo kubwa sana kwenye jamii zetu.
Na Kama huu Mfumo Wa Elimu utafanyiwa mabadiliko, Kuna uwezekano kabisa wa kupunguza au kuondoa matokeo mabaya huko mashuleni, kwani mwisho wa siku kila mtoto atafanya kitu ambacho anakipenda na kitu ambacho anauwezo nacho katika kukifanya kwa ufasaha na ufanisi mkubwa, hii ni kwa sababu kila mtu ana uwezo wake wa kipeke katika eneo fulani la maisha.
MFUMO MPYA WA ELIMU, Sera ya Mfumo mpya wa Elimu, imejikita katika kuchochea Mfumo wa Elimu ambao, utaleta Elimu itakayo husika moja kwa moja katika kugundua na kuendeleza nguvu ya upekee ambayo mtoto flani amezaliwa nayo. Ni Mfumo wa Elimu ambao utamsaidia mtoto aweze kujitambua yeye ni nani haswa na nini anacho paswa kukifanya kwenye jamii yake, lakini pia umsaidie aweze kufikia kilele cha Malengo yake. Unatakiwa uwe ni Mfumo wa Elimu ambao utalenga Kumfungulia mtoto Dunia na kuhakikisha huyo mtoto anaishi katika Ndoto anayo itaka. Elimu ambayo itatoa Haki sawa kwa kila Mwanadamu au kila Mtoto anaye zawaliwa katika ardhii hii ya Tanzania na hata Dunia kwa ujumla, Namaanisha kwamba kama mtoto akitaka kuwa Daktari sawa, pia kama Mtoto akitaka kuwa Mwanamichezo hodari basi isiwe shida pia.
Natamani kuona Mfumo Wa Elimu ambao utaleta Elimu ambayo itamsaidia mtoto kuweza kujua ni nini maana ya halisi ya Maisha, ili aweze kuishi na jamii yake katika Hekima na Maarifa na pia aweze kutatua changamoto zilizopo katika jamii.
FAIDA ZA MFUMO MPYA WA ELIMU.
Moja kati ya Faida kubwa na Muhimu za mfumo mpya wa Elimu katika jamii zetu, ni kwamba watu wataishi ndani ndoto zao, na hii itapelekea watu kuishi MAISHA WANAYO YAPENDA NA WATAYAPENDA MAISHA WANAYO ISHI NA FURAHA ITA TAWALA MAISHANI. Kawaida, mtu akiishi maisha anayo yapenda au akijishughulisha na kitu anacho kipenda, ni dhahiri kwamba, bidiii, kujituma, ufanisi na ufasaha katika kazi utaongezeka, ambapo nalo hilo pia litapelekea mtu kuleta MAENDELEO MAKUBWA KWENYE JAMII HUSIKA.
MAPENDEKEZO YANGU YA NINI KIFANYIKE ILI TUWEZE KUINGIA KWENYE MFUMO MPYA WA ELIMU.
Katika mchakato wa kuhakikisha tunaingia kwenye Mfumo mpya wa Elimu, SERIKALI inatakiwa kubeba hili jukumu kwa asilimia kubwa. Kama ilivyo pambana katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na shule nyingi tulizo nazo leo hii, basi vivyo hivyo ipambane katika kuhakikisha TANZANIA INAPATA SHULE MAALUMU NA ZENYE UWEZO WA KUMSAIDIA MTOTO KATIKA KUGUNDUA, KUKUZA NA KUENDELEZA UWEZO WAKE WA KIPEKE ALIO ZALIWA NAO. Kwa maana nyingine ni kwamba izo shule zinatakiwa ziwe na MITAALA MAALUMU KULINGANA NA UWEZO WA KIPEKEE NA KIPAJI ALICHO NACHO MTOTO. Hapa namaanisha kwamba kama mtoto anataka awe Mwanamichezo, basi apewe ELIMU AU MTAALA MAALUMU UTAKAO ENDANA NA TALANTA YAKE ILI AWEZE KUFIKIA KILELE CHA MALENGO YAKE. Na vivyo hivyo wafanyiwe watoto wenye talanta nyinginezo.
Pia katika kuhakikisha hilo lina enda sawa, basi Serikali inavyo utambulisha huo MFUMO MPYA WA ELIMU, inatakiwa waambatanishe na MAELEZO MAALUMU yanayo fafanua na kueleza umuhimu na maana ya Mfumo huo mpya wa Elimu,na hayo maelezo ni kwa ajili ya kukomboa fikra za watu waliopo kwenye jamii zetu ili mtoto atakapo onyesha nia ya kuwa chochote anacho taka, basi familia iheshimu mawazo yake. Kwani miaka hii ya sasa, asilimia kubwa ya watu kwenye jamii zetu wanacho jua tu ni kwamba mtoto anatakiwa awe daktari au mhandisi au rubani au taaluma nyinginezo zinazo tokana na kwenda huko shuleni hasa zilizopo kwenye Mfumo wa Elimu wa sasa, kitu ambacho kina athiri na kuumiza sana watu wengine.
Mabadiliko ya Mfumo wa Elimu wa sasa ninayo yazungumzia hapa sio kwa ajili ya kuusema vibaya Mfumo wa Elimu wa sasa, wala sio kwa ajili ya kuwatenga watu wanao taka kuwa madaktari, wahandisi, marubani, wanasheria, au Taaluma yoyote inayotokana na Mfumo wa Elimu wa sasa, BALI mabadiliko ninayo yazungumzia hapa ni kwa ajili ya kila mtoto aneye zaliwa kwenye ardhi hii ya Tanzania na hata Dunia kwa ujumla , pia ni kwa ajili ya kujenga Taifa lililo bora, Taifa lenye watu ambao wana talanta mbali mbali zinazo saidia kutatua changamoto kwenye jamii zetu, watu ambao wanaishi ndoto zao ambazo zinawapa FURAHA MAISHANI MWAO.
ASANTE.
AUTHOR:NATHANAELI SUMBI.
Upvote
1