KERO Responded Sera ya NSSF kuondoa Fao la Kujitoa INAUA NDOTO ZA VIJANA KUJIAJIRI – Irejeshwe

  • Thread starter Thread starter Anonymous (9713)
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakati Serikali ikiendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya kuwakopesha vijana ili kuwawezesha kujiajiri, bado kuna kundi kubwa la vijana waliowahi kufanya kazi katika sekta binafsi ambao wanatamani kujiajiri kwa kutumia mitaji yao binafsi—fedha walizochangia kwa jasho lao kupitia NSSF. Hata hivyo, ndoto hii imeendelea kuzimwa na sera kandamizi ya kuondoa fao la kujitoa, huku NSSF ikiendelea kukaa kimya licha ya kilio cha wananchi wengi wanaodai kurejeshwa kwa fao hilo.

Inatia shaka kuona Serikali ikihangaika kuwatafutia vijana mikopo, ilhali vijana hao hao tayari wana fedha zao wenyewe zilizohifadhiwa NSSF ambazo wangeweza kuzitumia kama mtaji wa kuanzisha biashara. Je, ni mantiki gani Serikali iwakopeshe vijana pesa zao wenyewe—wakati mwingine kwa riba, masharti magumu na urasimu mkubwa?

Mikopo mingi ya Serikali na taasisi za kifedha, ikiwemo ile ya asilimia 10 inayotolewa kupitia Halmashauri bila riba, imejaa urasimu, inachukua muda mrefu, na mara nyingi haiwafikii walengwa stahiki. Zaidi ya hapo, vijana hulazimishwa kujiunga katika vikundi, ilhali si kila kijana ana malengo au mwelekeo unaofanana na wa wengine.

Hali hii imechangia biashara nyingi kushindwa kudumu na mikopo kushindikana kurejeshwa. Si ajabu kuona hata baadhi ya wabunge wakishauri Serikali kuanza kutoa mikopo kwa watu binafsi, kama inavyofanyika kwa watu wenye ulemavu.

Sera ya sasa inayomnyima kijana fao lake la kujitoa, na badala yake kumpatia asilimia 33 ya mshahara wake kwa miezi sita, kisha kumsimamisha kwa miezi 18 akitarajiwa apate ajira nyingine, ni sawa na kushikilia fedha za mtu kwa miezi 24 bila uhakika wowote.

Inaonekana wazi kuwa waliopitisha sera hii hawatambui ugumu uliopo katika kupata ajira mpya nchini. Kama ajira ni rahisi kiasi hicho kupatikana, kwa nini wabunge wenyewe hawako tayari kukaa bungeni kwa muhula mmoja au miwili tu kisha waende kutafuta ajira nyingine?

Kwa kuwa NSSF tayari imeunganishwa na mfumo wa NIDA, ambao pia hutumika katika utoaji wa mikopo kwa vijana na ajira za Serikali kupitia Ajira Portal, Serikali ina uwezo wa kufuatilia na kusimamia wanufaika wake.

Hivyo basi, iwapo inaonekana ni vigumu kurejesha fao la kujitoa bila masharti, angalau kijana apewe uhuru wa kuchukua fedha zake za NSSF ndani ya miezi mitatu baada ya kuachishwa au kuacha kazi kwa hiari yake, kwa sharti la kukubali kutonufaika na mikopo ya vijana wala ajira za Serikali kwa kipindi cha miezi 24.

Inashangaza kuona kijana anayeamua kwa hiari yake kuacha kazi anaambiwa asubiri hadi afikishe umri wa miaka 55 ndipo apewe fedha zake. Je, kuajiriwa ni lazima kwa kila kijana? Vipi kwa yule anayeona ni bora kujiajiri na hata kuajiri vijana wenzake? Kwa nini adhibiwe kwa uamuzi wake wa kimaendeleo?

Mara nyingi sera za hifadhi ya jamii huigwa kutoka nchi za nje ambako mazingira ya ajira na maisha ni tofauti kabisa na ya Tanzania. Kwa nini NSSF isifanye tafiti za ndani, hususan kwa wanachama wake na waajiri wao, ili kuelewa uhalisia wa maisha ya Watanzania na kubuni mifumo ya mafao inayokidhi mahitaji halisi? NSSF imewasababishia vijana wengi msongo mkubwa wa mawazo kwa kujaribu kulinganisha ajira zisizo na uhakika za sekta binafsi na ajira za uhakika za sekta ya umma.

Je, kuna mbunge yeyote au mfanyakazi wa NSSF anayeweza kusimama kwa ujasiri mbele ya vijana wanaohangaika mitaani na kuwaeleza, kwa uhalisia na kwa ushahidi, ni kwa namna gani kuondolewa kwa fao la kujitoa ni kwa manufaa yao?

Natoa wito kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutafakari upya, kwa haraka na kwa maslahi ya Taifa, na kurejesha sera ya fao la kujitoa la NSSF. Hatua hii itawawezesha vijana wengi kujiajiri kwa mitaji yao wenyewe, huku Serikali ikielekeza nguvu zake katika kuwasaidia wale wasio na mitaji kabisa.

Isiwekwe nongwa kwa kijana anayeamua kuacha kazi kwa hiari yake. Vijana wengi wanapitia mazingira magumu kazini na wana ndoto za kujitegemea. Fedha wanazodai si msaada wa Serikali, bali ni jasho lao. Kuendelea kuzishikilia ni kuwaongezea mateso na kukatisha tamaa kizazi kizima cha vijana wanaotaka kujenga Taifa kupitia kujiajiri.

Pia soma ~ Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu: Mwajiriwa akipoteza ajira atapata mafao yake ya jumla ndani ya Siku 90
 
Na Hiyo 33% unaichukua baada ya mwezi au miezi mitatu?
 
Andiko adhimu na la kuelewa sana hili,Serikali kuja sera kabla hawajaleta bungeni tuzifikirie kwanza,hii sera ya fao la kujitoa NSSF iwekewe mkazo kwa sekta ya umma,huku sekta binafsi hususani viwandani kiukweli kuna madhara mengi,kwa hiyo kijana anafanya kazi kwa malengo ya muda mfupi ili kukwepana na hayo madhara,so anakuw anategemea fedha ya nssf ili kujiajiri.
Nipo kiwanda fulani kinazalisha betri naona vijana kadhia wanazopitia,tujali hili kundi la vijana ukiwa front ndiyo unaweza kuwa na uchungu ...NB:Serikali tuweke sera imara na zenye utekelezaji kwa kundi la vijana ambao wapo takribani milioni 13+
 
Back
Top Bottom