Sera ya Vyuo Vikuu kubakiza wahitimu wenye ufaulu wa juu badala ya kuajiri wasomi walio- practice unaathri ubora wa elimu inayotolewa vyuoni

Mkuu rejea kwenye msingi wa vyuo vikuu. Kazi ya vyuo vikuu sio kuandaa practioners bali critical thinkers! Haya ya practical yako vyuo vya kati.

mkuu mwisho wa siku elimu inatakiwa kuendana na mahitaji ya soko husika na hapa ndipo alipolenga mleta mada

kada kama za biashara haziitaji tu mtu ambaye ni critical thinker ila anaeweza pia kuwa impactful kwa area yake,
na hiyo impact kwa kiasi kikubwa itachangiwa na experience ya mtoa elimu kwanza

Not necessary awe amekaa ofisini lakini at least awe familiar na vitu vinavyoendelea katika field yake kupitia work shops, "Research" , practice binafsi au hata online course

sasa kama lecturer hafit zaidi ya kukaririsha watu notes bhasi hakuna haja ya kulalamikia graduates kuwa weupe kichwani wakikabidhiwa maeneo ya kazi
 
Lakini mbona Ajira hutangazwa kwa uwazi! Au huwa hauoni? Isije kuwa unamaoni lakini hukuyaweka sawa? Kwa walimu mashuleni huwa wamepractice wapi mzee?
 
Mkuu Eyce, mleta mada anaamini kwamba kuwabakiza wanafunzi wenye ufaulu wa juu ni makosa. Sasa nashindwa kumuelewa kwasababu huu utaratibu uko dunia nzima, pia mtu huwezi kutoka kuwa Tutorial Assistant/Tutor na kupanda juu kuwa Assistant Lecturer hadi Lecturer bila kufanya tafiti na kuwa na uzoefu.

Pili, huwezi kufundisha wanafunzi wa shahada kama wewe bado una shahada. Utasaidia tu kazi chache-chache na ukipata shahada ya pili ndipo utaingia darasani. Lakini kubwa TCU imetoa utaratibu kwamba kila muhadhiri ni lazima aandike machapisho kadhaa ndani ya muda fulani.

Ukienda UDSM shule ya sheria waalimu karibia wote ni mawakili wazoefu na wameandika machapisho mengi na kufanya tafiti kubwa sana pengine kuliko vyuo vingine nchini Tanzania, sasa sifahamu alikuwa anazungumzia uzoefu upi labda.....
 
Hahaha labda mawakili maboya mfano wa Dr mwakyembe na Prof kabudi wazee wa theories
 
Hoja yako ina ukweli. Mfumo unasabisha uduni wa mawazo.Elimu ya TZ ni kutafuta GPA kubwa siyo maarifa.Sasa tuangalie practice pia
 
Hahaha labda mawakili maboya mfano wa Dr mwakyembe na Prof kabudi wazee wa theories
Prof Kabudi ni wakili ambaye hajawahi kufanya shughuli za uwakili, lakini Dr Mwakyembe amefanya sana shughuli za uwakili miaka ya 90's hadi 2000's mwanzoni: Hawa wote wawili ni wanasheria wazuri sana.

Tatizo kubwa ambalo linaikumba nchi yetu ni tabia ya kuchanganya utaalamu na siasa za kujikomba kwa watawala (Intellectual Sycophancy) ambalo limewakumba wanazuoni wetu wengi. Tukifanikiwa kutenganisha siasa na utaalamu naamini tutafika mbali sana...
 

Nimekuelewa brother

ndio maana hata kwenye comment yangu sikusisitiza tu hawa tutorial assistants au wenye vyeo vyovyote lazma wapitie actual field lakini at least wawe aware na vitu vinavyoendelea huko. Vinginevyo elimu watakayoitoa itakuwa less relevant

bhasi hata kama wataendelea na mfumo huu au kutangaza ili kupata watu wanaostahili zaidi (inafanyika pia).
bhasi kuwe na system ya kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa, watu wanaoitoa na soko linalopokea, virandane

nadhani hii ndio main concern ya mleta mada
 
Nakubaliana kabisa na wewe kaka, kwamba ni lazima elimu yetu iendane na mazingira husika ya dunia tunayoishi. Hili sasa ni suala la kisera zaidi ambapo sisi kama taifa tunatakiwa tukae na kuamua tunafanya nini ili kulifanikisha, kuanzia kwenye ngazi ya mitaala (Hapa ndipo pana changamoto kubwa).

Kuna sehemu kama taifa tulijikwaa, mitaala yetu ya elimu imekaa kizamani sana. Mambo mengi ambayo tumeyaiga Uingereza na Uchina tayari wenzetu wameisha achana nayo. Jingine ni kwamba sisi hata kama tunaandika, hatuandiki katika kiwango kinachotakiwa kama ambavyo wenzetu wa Kenya, Nigeria na Afrika-Kusini wanafanya.

Ukiingia Maktaba ya University of Lagos au Univeristy of Pretoria sehemu kubwa ya vitabu na machapisho utakayokuta ni vimeandikwa na wazawa: Kikubwa zaidi siyo vya zamani sana. Sisi pale UDSM utakuta Profesa mmoja ameandika vitabu viwili tu maisha yake yote. AU Daktari anaandika maandiko matano tu kutokana na kubanwa na TCU.

Lakini changamoto kubwa zaidi ni serikali kutowekeza fungu la kutosha kwenye tafiti zinazofanywa na vyuo vikuu. Hili mbona wakina ndugu Salary Slip hawalisemi ambalo ndilo muhimu kabisa !!! Ili elimu yetu itoke hapa ilipo ni lazia gharama zitumike, lakini serikali yetu imewekeza kwenye siasa na ujasusi dhidi ya raia wake.

Hilo la bwana Salary Slip kupinga wanafunzi wenye ufauli wa juu kubakizwa vyuoni nadhani halina mashiko na limekaa kisiasa zaidi. Huu utaratibu ndiyo uko duniani nzima, ambapo ni lazima nchi iandae wahadhiri wake wa baadae....
 
Sasa kama mtaala wa elimu ni kukaririshana unategemea nini?

Ndio maana mwisho wa siku akina Msukuma wanatukana hao maDr na maProf kule bungeni..

Mtu unaacha kumpa Kimei wizara ya Biashara na Viwanda, a man who single handedly raise CRDB from no where to one of the largest banks in East Africa unampa Mkumbo mwalimu wa Socialogy sijui na mpiga ramli za siasa kisa tu ni Prof..
 
Huwamtaki waliobaki chuoni ambao wamepata First Class, sasa hawa wenye uzoefu wawe wali pata ufaulu gani?
 
Mleta mada ameleta hoja ya msingi hasa.

Ukitizama professors wa nchi nyijngine ukawalingamisha na wa kwetu, tofauti ni kubwa sana.

Hata papers zinazoandikwa na maprofesa wetu, zimejaa nukuu za kazi za wengine, kiasi cha kuchosa hata kusoma. Wale wa vyuo vya nje, hasa Ulaya, America yote ja Australia, hata kama hakufanya kazi baada ya shahada yake ya mwanzo, bado wanakuwa wameshiriki kwenye researches mbalimbali, technical/professional visits za maeneno mbalimbali ya kazi, makongano ya kitaalam, n.k. Hayo yote yanawajengea uelewa mpana sana kwenye fields zao. Na wakati wote wanakuwa kwenye Ulimwengu wa sasa wa fields zao. Siyo kama wa hapa kwetu. Angalia kama Kabudi - wakati wote ni nukuu za historia, mambo ya kale, inaonekana hajui yanayotokea sasa. Aliyoyajua akiwa tutorial assistant, ndiyo aliyobakia nayo mpaka leo, hakuna anachoongeza.
 
Jamaa ana point! Hao wanafunzi wenye first class hio practical wanaifanyia wapi ambapo kuna kazi za proffessional zao? Au wataifanyia mtaani kwa kuanza kufanya biashara za ubuyu na kupost nguo mtandaoni?
We pia una point nzuri...ila alichomaanisha muandishi n kwamba kwa mfano mtu kapata first class kwenye mambo sociology then anachukuliwa kupiga mzigo wa huo chuon while watu watu walospecialize kwenye kuwafundisha watu wasocialogy, nafr hio ndo ilkuwa point yake
 
Jamani, jamani, jamani!!!! Hebu tuweni wakweli hata kidogo basi. Mkuu hivi unaweza kuandika chochote kile kwenye ulimwengu huu wa taaluma bila kufanya rejea na nukuu kutoka kwa wanazuoni wengine ??? Hata wanazuoni wakubwa duniani kama Prof Noam Chomsky na Michael Focault ambao wanaongoza kwa kufanyiwa rejea (Most Cited Intellectual) hawawezi kuandika bila kufanya rejea.....

Unaposema nukuu zinakuchosha kusoma hao wa Ulaya na Australia umewasoma na kukuta hawajafanya nukuu hata kama wamehusika na tafiti mbalimbali. Kaaazi kwelikweli......
 
..kama TAs hawana practical experience wanaweza kupelekwa kufanya kazi ktk miradi / projects mbalimbali inayotekelezwa hapa nchini.

..kwa mfano, ni mategemeo yangu kwamba udsm imepeleka vijana wake kadhaa kwenye miradi kama sgr, stieglers, kigongo-busisi, etc ili wapate uzoefu na kurejesha uzoefu huo chuoni.

..hata waliofanya PhD wanaweza kutumwa nje ya nchi kufanya kazi kama Post Doctoral researchers ktk taasisi mbalimbali tulizo na urafiki nazo.

Cc Salary Slip , MALCOM LUMUMBA
 
Hata hivyo pia waliowengi wanabakishwa kwa kujuana
Wengine matokeo hayakutokana na juhudi au uwezo wao bali walipewa kama zawadi,rushwa au hongo.
Naishia hapo maana......naelekea kutoa mfano
 
Jamaa ana point! Hao wanafunzi wenye first class hio practical wanaifanyia wapi ambapo kuna kazi za proffessional zao? Au wataifanyia mtaani kwa kuanza kufanya biashara za ubuyu na kupost nguo mtandaoni?
Mbona kuna ofisi nyingi watu wanajitolea kufanya kazi ili kujiongezea umahili wa vitendo.Shida kama mnawaza kupiga pesa haraka haraka mtashindwa kupractise.
 
Mkuu JokaKuu mimi nakubaliana na wewe kwenye mambo mengi na nikimaliza kazi ntarudi kuchangia kuhusu hili. Nachokikataa mimi ni hili la wanasiasa kama bwana Salary Slip ambao hawajawahi kuwa wahadhiri wa Chuo Kikuu kusema vyuo viache kubakiza wanafunzi wake wenye ufaulu wa juu na viajiri watu wazoefu tu.

Namheshimu sana bwana Salary Slip, lakini kwangu hii ni siasa ya bei ndogo kwasababu haijafanyiwa utafiti wa kutosha. Duniani kote utaratibu uko hivi, kuna marafiki zangu wa nje ya nchi walipakizwa kuwa tutors kwenye vyuo vikubwa tu. Utaratibu kuhusu nini kifanyike unatolewa na TCU, changamoto ni kwamba vyuo vingi havifuati hizo utaratibu (Hili ni tatizo jingine kabisa) ambalo halihusiani kabisa na kubakiza wahitimu wenye ufaulu wa juu.
 
Hahahahah ndio maana wanajitaftia experience pale pale ya kuwa makatili na kuanza kunyanyasa wenzao kupitia courseworks!

Hilo ndilo nalofahamu atleast for now!
Kwa hiyo kumbe tatizo siyo uzoefu bali isipokuwa mnataka mpewe alama za bure za cousework!

Pia hata ukisema unawahitaji wenye uzoefu ina maana wanaomaliza vyuoni hawatapata ajira na badala yake walewale wenye uzoefu wataendelea kuchukua nafasi za wapya. Kwani hao wenye uzoefu wangepata wapi huo uzoefu kama wasingeajiriwa walipomaliza masomo yao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…