Sera ya Vyuo Vikuu kubakiza wahitimu wenye ufaulu wa juu badala ya kuajiri wasomi walio- practice unaathri ubora wa elimu inayotolewa vyuoni

Hiyo experience ya field anaitoa wapi kama mtu kamaliza chuo miaka mitano nyuma first class with hanours na hajapata hata kiofis cha kujitolea
Wwchukuliwe wale wenye uzoefu wapo kibao tu mtaani
 
Jamaa ana point! Hao wanafunzi wenye first class hio practical wanaifanyia wapi ambapo kuna kazi za proffessional zao? Au wataifanyia mtaani kwa kuanza kufanya biashara za ubuyu na kupost nguo mtandaoni?
na wewe ujaelewa kitu,umekurupuka kucoment bila kusoma uzi kama inavyotakiwa: hili ndo tatizo la Wadanganyika wengi🤣 Mtoa mada anashauri Walimu wa Vyuo wawe wale ambao wanatokea mtaani baada ya kufanya kazi kwa miaka kadhaa,Wasichukukiwe wale direct from School ili waweze fundisha kwa umakini na kutumia uzoefu wao na changamoto walizokutana nazo wakiwa kazini kwa new generation,sasa hivi ni kama vile Kipofu kuongoza Kipofu mwenzake.....mtu ajawai mathalani kufunga ata mnara mmoja wa simu,au kufungua/kuasembo engine ata moja ati kwa kuwa amefaulu vyema anakuja kuwa mwalimu wa Automotive engineering au wa Telecom... Mfano Prof Assad kwa sasa yupo pale Muslim Unv Morogoro...Tuna amini wanafunzi walio chini yake watamaliza chuo wakiwa na uelewa mpana sana kwenye taharuma ya Uhasibu kuliko wale wanaofundishwa na Maprofessor ambao awajawai kuajiriwa au kijiajiri kwenye fani walizosomea
 
Na ndio maana kwa sasa serikali inapeleka wahitimu wengi wa kidato cha nne wenye ufaulu wa kati mf. DIV 2 dhaifu na DIV 3 vyuo vya kati kusoma Diploma.
Wakati nakua au tunakuwa tulikuwa tunaaminishwa ya kuwa au kuambiwa ys kuwa vyuo vya ufundi vinawafundisha vijana kazi na wanajua kazi kweli,nikakua mzee mzima nikapita katika baadhi ya vyuo hivyo,nilichokiona ni tofauti na nilichokisikia ni theory tu na ukikuta practical ni zile za zamani na zimeshapitwa na wakati katika ile hali ya vifaa.

Ukitaka kujua kazi kwanza ni kwa juhudi yako na kupenda unachokifanya na kuingia field husika. Hapa nawazungumzia mafundi wenzangu. Mfumo wetu wa elimu hado mbovu sana kuanzia ngazi za chini mpaka huko juu.
Kwa fani za ufundi hasa sisi mafundi,walimu wetu pia wanatakiwa wawe mafundi hasa.

Lakini hata hao wenye uwezo walipofika vyuoni walifeli na wasio na uwezo wengine walifaulu. Haya mambo huwa yanataka kujitambua na mifumo kubadilishwa.

Mimi huwa nawaambia wadau kama ningepata wasaa wa kutoa maoni au kupewa mchongo wa kubadilisha mtaala katika shahada ya uhandisi wa umeme vijana wangepata ladha ya ufundi tangu wapo mwaka wa kwanza. Mfumo wetu unatupotezea muda sana sasa sijui wasomi wetu hawajiamini au shida ni ipi.
 
Uko sahihi kabisa. Ulimwengu huu wa sasa umekuwa na changamoto nyingi sana kuliko zamani,hautati story nyingi zaidi ya kutatua matatizo na kusonga mbele.
 
Maprofesor/ lecturer wanaoongoza Kwa kutoa machapisho mengi Tanzania nafikiri ni SUA . Most prereviewed journal
 
Ujerumani hauwezi kufundisha vyuoni kama hauja pactice ulichosomea kwa angalau miaka 5. Na hii ni hasa upande wa emgineering
 
Upo sahihi sana katika maelezo yako kwamba vyuo vyetu viliona ni nafuu kujenga kuanzia chini (T.A) hadi kutengeneza professor.

Ila kuna tofauti kati ya kufanya kile kilicho nafuu (kilicho ndani ya uwezo wako) na kufanya jambo sahihi lakini linalohitaji maamuzi magumu. Ninachopendekeza ni mabadiliko makubwa katika mfumo wa elimu ya vyuo vikuu utakaohitaji maamuzi magumu yafanyike.

Elimu yetu ya chuo kikuu haiwezi tena kuhimili vishindo vya karne ya 21, yenye changamoto za ajira, mabadiliko tabia ya nchi, uchumi wa kidigital, magonjwa ya milipuko, n.k. Vyuo vyetu havipaswi tena kuwa teaching universities, lazima viwe strategic think tanks, research and solution oriented universities. Hii dhana inaaply kwenye field zote (kuanzia Kiswahili hadi Atomic Physics). Kwa sasa unaweza kushangaa watoto ngazi ya chuo kikuu wanaingia darasani kufundishwa irabu za Kiswahili na namna ya kuunda sentensi za Kiswahili. Kwa karne ya 21 tunapaswa kuwafundisha watoto namna gani Kiswahili kinaweza kutumika kupenyeza ajenda ya East Africa across the continent kiuchumi, kisiasa na kitamaduni. Kuna maana yake maana katika context ya utandawazi na itahitaji integration ya lugha, uchumi, siasa na usalama wa nchi. Ndio maana watoto wetu wakienda kufanya interviews na waajiri hawawezi kufikiri nje ya box na kulink mambo. Ni kazi ya PIs kuwa strategic thinkers, na kutengeneza wanafunzi strategic thinkers wengine kupitia ufundishaji na usimamizi.

Huu ni mfano tu, lakini unaapply hata kwenye disciplines zingine ikiwemo Sayansi, Kilimo, Biashara, Teknolojia, Uchumi, Ualimu, n.k, na nakwambia haya mambo yanahitaji yapewe kipaumbele na serikali kuangalia namna gania ya kuondoka kwenye traditional educational systems kwenda kwenye innovative educational systems. Kwa muktadha wa namna ambavyo Kikwete alimleta Maximo Maxime kiutoka Brazili akawa anamlipa milion 11 ili aiboost timu ya taifa, ndivyo Serikali inavyopaswa kulipa umuhimu suala la elimu ya chuo kikuu. Ni kosa la kimkakati kuwa na vyuo vikuu lukuki ambavyo huwezi kuvihudumia inavyostahili. Bora kuwa na vyuo vikuu vichache, vya kimkakati, utakavyoweza kupata PIs wenye sifa -- waendeshe vyuo vikuu kwa tija. Vyuo vikuu vinamsemo wa tangu zama za kale eti kazi yao ni Teaching, Research and Consultancy -- ukiwauliza nionyeshe mfano wa hizo consultancy zenu mnazofanya, utashangaa ni upuuzi mtupu maana wengine ndio kama hao akina REDET na siasa zao za huyu sijui anakubalika kwa asilimia ngapi. Hii nchi tayari inapoteza hela nyingi sana kwenye mifumo ya elimu isiyo na tija, na kila mwaka nchi inatenga takribani bilioni 400 kugharamia wanafunzi wanaosoma vitu vitu visivyo na maana na matokeo yake hawaajiriki. Hizi ni hela nyingi sana ukizistrategize zinaweza kubadilisha sana namna elimu yetu inavyoendeshwa. Kuna mambo mengi ya kushauri kuhusu hili lakini niishie hapa kwa sasa.
 
Maprofesor/ lecturer wanaoongoza Kwa kutoa machapisho mengi Tanzania nafikiri ni SUA . Most prereviewed journal
Naam hakuna kama SUA Tanzania, wanafanya na tafiti nyingi sana za kisayansi.
 
Nilimalizia kwa kusema tutahitaji political will and commitment. Tuna mfumo wa sauti moja nchi hii na maamuzi magumu labda yatoke juu vinginevyo funding inakuwa shida. Sasa hivi tuna mass production ya graduates karibu vyuo vyote. Na kama haitoshi hao ma phd ndio kila siku wanachaguliwa serikalini kwa kazi ambazo wenye degfee moja au masters wanazimudu. Hii inashusha quality ya elimu yetu na wahadhiri kutopata muda wa utafiti.
Hadi hapo tutakapo pata mtu wa kuchampion elimu kama mkombozi wetu na kuwa tayari kj invest strategically sioni mwanga. Mfumo wetu wote wa maamuzi unahitaji mabadiliko.
 
Wenye GPA za lower second tunadharaulika sana ila trust me. Nilishindana interview na vipanga wenye firts class nikawachakaza vibaya katika post ya meneja katika idara moja nyeti sana ya Umma mwaka jana October.

Nipo nafanya kazi na watu wakubwa sana hadi namshangaa Mungu.

Hakika usidharau confidence uliyonayo hiyo ni zaidi GPA Class yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…