Upo sahihi sana katika maelezo yako kwamba vyuo vyetu viliona ni nafuu kujenga kuanzia chini (T.A) hadi kutengeneza professor.
Ila kuna tofauti kati ya kufanya kile kilicho nafuu (kilicho ndani ya uwezo wako) na kufanya jambo sahihi lakini linalohitaji maamuzi magumu. Ninachopendekeza ni mabadiliko makubwa katika mfumo wa elimu ya vyuo vikuu utakaohitaji maamuzi magumu yafanyike.
Elimu yetu ya chuo kikuu haiwezi tena kuhimili vishindo vya karne ya 21, yenye changamoto za ajira, mabadiliko tabia ya nchi, uchumi wa kidigital, magonjwa ya milipuko, n.k. Vyuo vyetu havipaswi tena kuwa teaching universities, lazima viwe strategic think tanks, research and solution oriented universities. Hii dhana inaaply kwenye field zote (kuanzia Kiswahili hadi Atomic Physics). Kwa sasa unaweza kushangaa watoto ngazi ya chuo kikuu wanaingia darasani kufundishwa irabu za Kiswahili na namna ya kuunda sentensi za Kiswahili. Kwa karne ya 21 tunapaswa kuwafundisha watoto namna gani Kiswahili kinaweza kutumika kupenyeza ajenda ya East Africa across the continent kiuchumi, kisiasa na kitamaduni. Kuna maana yake maana katika context ya utandawazi na itahitaji integration ya lugha, uchumi, siasa na usalama wa nchi. Ndio maana watoto wetu wakienda kufanya interviews na waajiri hawawezi kufikiri nje ya box na kulink mambo. Ni kazi ya PIs kuwa strategic thinkers, na kutengeneza wanafunzi strategic thinkers wengine kupitia ufundishaji na usimamizi.
Huu ni mfano tu, lakini unaapply hata kwenye disciplines zingine ikiwemo Sayansi, Kilimo, Biashara, Teknolojia, Uchumi, Ualimu, n.k, na nakwambia haya mambo yanahitaji yapewe kipaumbele na serikali kuangalia namna gania ya kuondoka kwenye traditional educational systems kwenda kwenye innovative educational systems. Kwa muktadha wa namna ambavyo Kikwete alimleta Maximo Maxime kiutoka Brazili akawa anamlipa milion 11 ili aiboost timu ya taifa, ndivyo Serikali inavyopaswa kulipa umuhimu suala la elimu ya chuo kikuu. Ni kosa la kimkakati kuwa na vyuo vikuu lukuki ambavyo huwezi kuvihudumia inavyostahili. Bora kuwa na vyuo vikuu vichache, vya kimkakati, utakavyoweza kupata PIs wenye sifa -- waendeshe vyuo vikuu kwa tija. Vyuo vikuu vinamsemo wa tangu zama za kale eti kazi yao ni Teaching, Research and Consultancy -- ukiwauliza nionyeshe mfano wa hizo consultancy zenu mnazofanya, utashangaa ni upuuzi mtupu maana wengine ndio kama hao akina REDET na siasa zao za huyu sijui anakubalika kwa asilimia ngapi. Hii nchi tayari inapoteza hela nyingi sana kwenye mifumo ya elimu isiyo na tija, na kila mwaka nchi inatenga takribani bilioni 400 kugharamia wanafunzi wanaosoma vitu vitu visivyo na maana na matokeo yake hawaajiriki. Hizi ni hela nyingi sana ukizistrategize zinaweza kubadilisha sana namna elimu yetu inavyoendeshwa. Kuna mambo mengi ya kushauri kuhusu hili lakini niishie hapa kwa sasa.