Kama ningewashauri serikali namna ya kuleta mageuzi katika elimu ya vyuo vikuu ningewaambia wafate model inayofanyika huko kwa vyuo vikuu vilivyotangulia. Kwenye hivyo vyuo vikuu waalimu wa vyuo vikuu hawaajiriwi kama njugu. Mwalimu wa Chuo Kikuu anapaswa awe mtu mkubwa sana, ili aitendee haki ile nafasi yake.
Wenzetu wanafanya hivi: kwa mfumo wa Western Universities na hata Easten huko Uchina, Japan, South Korea, Singapore, Indonesia, waalimu wa vyuo vikuu wanaitwa PIs (Principal Investigators). Principal Investigators ndio viini vya taaluma za vyuoni. Wanawajibika katika kuanzisha research agenda, kutengeneza research teams, kuattract research funding, kuhire research assistants kama postdocs na tecnicians, kurecruit PhD na Master students. Na kwa vile hawa watu watahitaji budget kubwa pale vyuo vinapotaka kuwaajiri hawaajiriwi kama njugu. Ni lazima itengwe initial budget ya kutosha kuajiri PI (wao wanaita seed funding) ili baadaye aweze kukiingizia chuo fedha zaidi kupitia grants atakazoattract. Department moja ya kitaaluma inaweza kuwa na PI 12 tu, halafu staff waliobaki ndani ya department wanafanya kazi chini ya hao PIs kwenye supporting roles. Ni ka mfumo ka ubepari vyuoni, lakini kako effective.
Hapa kwetu tunafanya tofauti. Mtu anaajiriwa kuanzia tutorial assistant (degree moja) hadi PhD. Wote hawa wanaajiriwa kupitia mfumo wa kawaida wa ajira serikalini. Akifika pale chuoni kama mwajiriwa mpya atapewa ofisi tu na courses atakazofundisha. Huyu mtu anatofauti gani na mwalimu wa sekondari? Wale tutorial assistants wataambiwa waende shule kwanza wapate masters. Ni utoto yaani, maana katika hiyo model hauwezi kupata excellence. Kama tunataka mabadiliko katika vyuo vyetu vikuu ni lazima mapinduzi yafanyike katika namna chuo kinavyoajiri wanataaluma wake. Lazima waajiriwe wanataaluma wachache wenye sifa na ubora wa juu kulingana na malengo ya chuo, lakini watakaowezeshwa vya kutosha ili wakiletee chuo tija katika malengo ya uwepo wa chuo hicho. Wenye sifa hizo wanaweza kupatikana kupitia uzoefu wao ndani na hata nje ya nchi.
P