Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Mimi sio mchumi, ila nachokiona ni kuwa, awamu hii inakaamua sana wananchi na hela inayokusanywa sehemu kubwa imeelelekezwa katika miradi michache tena inayoplekea baadhi ya fedha kwenda nje ya nchi(kupitia ununuzi wa malighafi kutoka nje,kulipa wataalamu wa kigeni,n.k) na hivyo inakuwa ni vigumu kwa hela hiyo kurudi kwa wananchi wengi wa kawaida na ambao ndio walipa kodi, na zaidi, miradi hiyo michache ya kuhesabu, iko katika maeneo machache ukilinganisha na ukubwa wa nchi, hivyo kuwezesha wananchi waliko katika maeneo hayo tu kufaidika moja kwa moja na miradi hiyo huku wananchi wengi katika maeneo mengine ya nchi wakibaki watazamaji tu.
Mwananchi huyu mtazamaji na anaelipa kodi ni nani?
Mtumishi wa umma
Huyu si mwingine bali ni yule mtumishi wa umma ambae kwa miaka mitano amesota na mshahara ule ule, na kama mtumishi huyu ni mfaidika wa Bodi ya Mikopo,basi mwisho wa mwezi anakutana na makato ya asilimia 15 ya mshahara usiongezeka kulipia deni lake la mkopo wa Bodi.
Mfanyabiashara
Wote ni mashahidi wa kilio cha wafanyabiashara kuilalamikia TRA katika swala zima la utozaji wa kodi na wote ni mashahidi wa taarifa za biashara nyingi kufungwa kutokana wahusika kushindwa kuziendesha ndani ya hii miaka mitano.
Wakulima,wafugaji na wavuvi
Japo hawa nao ni walipa kodi,lakini ukitaka kujua kodi wanayolipa inawarudiaje kuwasaidia katika sekta au maeneo yanayowahusu,sikiliza kilio cha wabunge,hasa wa upinzani,juu ya bajeti zinazotengwa kwenye sekta hizo na zaidi angalia kiwango halisi cha fedha kinachopelekwa kulinganisha na Bajeti iliyokuwa imepangwa.
Kuhusu wakulima wa korosho na kilimo cha mazao mengine ya biashara na mwenendo mzima wa mazao hayo,nawaachia wasomaji mtafute taarifa zikoje kuhusu mwenendo wa mazao hayo ya biashara na mchango wa mazao haya katika kuingiza fedha za kigeni ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Kwa kifupi, mpaka hapo utaona ni kwa namna gani fedha iliyokusanywa na serikali inamrudia mlipa kodi huyu kupitia nyongeza ya mishahara, kupitia biashara anazofanya,kilimo anachoendesha,uvuvi anaoufanya,n.k alafu jiulize kama purchasing power ya mwananchi huyu inaongezeka au iko matatani kila kukicha.
Hapo usisahau watu kama mafundi ujenzi wa nyumba na vibarua wao,mafundi seremala,dereva wa bodaboda na wengine walioko katika makundi mengine wanaotegemea fedha kutoka kwa mfanyabiashara huyu,mtumishi huyu wa umma,mkulima,n.k.
Binafsi huwa najiuliza: hivi mpaka leo hii hatujui ni zipi zinapaswa kuwa sera zetu na ni sekta zipi tuzipe kipaumbele kwanza ili mchango wake katika uchumi uwe reflected katika maisha ya wananchi walio wengi na ambao hata wakisikia uchumi umepanda,basi walau waweze kuona ina-make sense?