Sera za kuwabeba "masikini" zinaua miji

Sera za kuwabeba "masikini" zinaua miji

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
1614586431575.png


Sasa hivi kuna sera zisizo rasmi za kuwabeba ati watu "masikini".

Nawawekea mfungo hao "masikini" maana hata definition yao katika jamii hawajulinani.

Humo kuna mama lishe, machinga na wengine wengi.

Kundi hili kwa sasa, hasa jiji la DSM, limeendekeza uchafuzi wa mazingira mkubwa sana.

Tatizo la hao "masikini" wamepewa open cheque ya kufanya lolote wanalotaka Jijini.

Wanaweza fungua biashara popote
Wanaweza kwenda haja popote
Wanaziba mitaro ya maji ya mvua
Hawazoi taka zao
Hawalipi kodi yoyote
Hawataki kudhibitiwa kwa aina yoyote ile kiutaratibu.

Walijengewa Machinga Complex kule Ilala lakini wako wanang'ang'ania barabarani

Kiujumla hawa "masikini" wanaweza kuwa mtaji wa kisiasa lakini ni kero kubwa kwa watendaji Jijini.

Hili sasa limesha kuwa tatizo la kisiasa.


MFANO HAI: MBEZI LUIS JANA
Gazeti la Guardian na Nipashe leo 2/03/2021

Kituo kipya ha mabasi ya kwenda mikoani.
Pics Pg 1 Machi 02.jpg
 
Hakuna machinga au mama lishe aliye epuka umasikini... Biashara zao zinawafanya masikini siku nenda rudi.

Kuna wamama tangu nasoma chekechea mpk leo bado wanauza vitumbua na maisha yao yako Vilevile.

Serikali haina mbinu za kuondoa umasikini
 
Ndo nikuulize wewe unaewapondea masikini
Basi inaelekea mada yenyewe wala huielewi na soma vizuri hizo commas za "masikini".

Tanzania tuna tatizo la kukurupuka kupata quick-fix solutions wakati source ya tatizo hatulielewi.

Mis-guided sympathy, ati kuwaonea huruma "masikini" ndio kuna attrack matatizo mengi zaidi badala ya kudeal na tatizo lenyewe la kuondoa umasikini.
 
Unaongea ukweli,nenda stand mpya ya mbezi after a week utaniambia. Pita maeneo ya posta sasa hivi uone jinsi mambo yanavyoenda hobela hobela ..
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wahusika wamesikia na kuelewa, watafanyia kazi suala hilo kwa weledi.
Mkuu hili sasa hivi ni tatizo kubwa sana hasa jijini Dar.

Machinga anauza nguo mbele ya duka lako , wewe unalipa kodi zote yeye halipi hata senti tano.

Na mama lishe pembeni kaweka jiko la mkaa au kuni anapika , thubutu umguse.
Wote wana chafua mazingira , hakuna wa kuwachukulia hatua.

Tunaingia sasa katika Jiji la magonjwa, uchafu, na kutoelewn kibiashara.
 
Basi inaelekea mada yenyewe wala huielewi na soma vizuri hizo commas za "masikini".

Tanzania tuna tatizo la kukurupuka kupata quick-fix solutions wakati source ya tatizo hatulielewi.
Mis-guided sympathy, ati kuwaonea huruma "masikini" ndio kuna attrack matatizo mengi zaidi badala ya kudeal na tatizo lenyewe la kuondoa umasikini.
🙏 🙏 🙏
 
Back
Top Bottom