Sera za nchi zinabadilisha maisha ya mtu na kuamua kuhama nchi kama Darius Phillip

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Darius Philip alizaliwa Tanganyika, wazazi wake walivutiwa na utawalawa wa British East Africa Empire na kusikia Tanganyika kuna ardhi kubwa walihamia miaka ya 1940 na kufanya kilimo cha biashara. Philip alisoma Tanganyika na kumalizia elimu ya juu Uingereza alikosomea uchumi wa kilimo. Alirudi Tanganyika, alioa msichana wa Kigiriki na kuanza familia. Aliwatunza wazazi wake katika uzee mpaka wanafariki. Philip alirithi shamba kubwa la mkonge kutoka kwa wazazi wake. Licha ya mkonge Philip alilima chai katika milima ya Usambara na alitoa ajira kwa watu wengi sana.

Azimio la Arusha lilipo tangazwa hela nyingi za Philip benkini zilitaifishwa. Philip alianza kutunza pesa kwenye ndoo za plastic. Alichimba mashimo na kuhifadhi pesa katika foreign currency na kufukia zege katika mashimo yake. Alijenga mashimo ya zege. Mpango ni kuzifukua miaka 10-20 ijayo.

Wakati huu Philip anahangaika na haya, zao la mkonge lilipoteza soko, Cold War na ufumbuzi wa kamba za platic zilizojulikana kama manila ulichangia kuua soko la mkonge. Hata soko la chai lilishuka baada ya nchi za Magharibi kuanza kununua chai Latin America., Sri Lanka na India na kuacha chai yetu.

Wakati Philip anapigana na haya yote, tuliingia katika vita ya Kagera. Biashara za Philip zilikosa matumaini. Aliuza nyumba, mashamba, mashine, matrekta kwa bei ya hasara na kuondoka nchini. Watu wengi walipoteza ajira. Leo mashamba ya Philip ni mapori.
 
Yapo wapi hayo nikawekeze,nataka niyafufue asee
 
Aisee nomaaa sana
 
Back
Top Bottom