Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Vipaumbele vya wagombea uongozi wote wa CCM, vinaelezwa kwa ufasaha, umakini na kwa mpangilio mzuri sana na unaeleweka kirahisi kwa wapiga kura.
Hii imechochea hamasa kubwa mno kwa wapiga kura wengi zaidi, tena wa vyama vyote vya siasa kujitokeza na kuwasikiliza wagombea vijana wasomi wa CCM, wanavynadi ilani na kufafanua sera na mipango yao ya maendeleo kwa mustakabali wa maeneo ya uongozi wanayoomba.
Kwakua vyama vingine vingi vya siasa inasikitisha sana. Havina ilani, wala havina agenda. Na kwa bahati mbaya sana wameishia kuporomosha dhihaka, kejeli, matusi na kujaribu kujipambanua kwa wananchi jinsi wasivyo wastaarabu na wasivyo na heshima kwa viongozi wa kitaifa nchini. Kwa hakika watapata kura sifuri.
Ni furaha kubwa kwa wananchi wazalendo nchi nzima, kuanza kuwapuuza na kukwepa kuhudhuria mikutano yao na kusikiliza matusi yao.
Soma Pia: Wapiga kura wengi zaidi Tanzania wana imani kubwa mno na wagombea uongozi wa CCM pekee
Uamuzi wa CCM kupendekeza na kuwapa fursa vijana wahitimu wa vyuo vikuu, kama ndiyo wagombea uongozi wake, kwa sehemu kubwa nchini, imeamsha ari mpya ya kazi na siasa, Lakini pia kumebadili kabisa taswira na uelekeo wa siasa za Tanzania na kuchochea hamasa na pumzi mpya, kwa ustawi wa demokrasia bora zaidi, ndani ya CCM na Taifa kwa ujumla.
Imani ya waTanzania wote kwa CCM ni thabiti. Na ushindi wa kishindo kwa CCM ni wa uhakika na ni Lazima 🐒
Mungu Ibariki Tanzania