Serengeti Boys yatinga Fainali ya AFCONU17 2026, baada ya kumuondoa Misri kwa mikwaju ya penati

Serengeti Boys yatinga Fainali ya AFCONU17 2026, baada ya kumuondoa Misri kwa mikwaju ya penati

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Serengeti Boys wameandika historia kwa kutinga Fainali ya AFCON U17 baada ya kuiondosha Misri kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 za mchezo mkali uliochezwa usiku huu.

Serengeti Boys wanamsubiri mshindi kati Senegal vs Morocco ambaye ndiye watakutana katika fainali

Hakika wanastaili pongezi nyingi sana. Hakika kocha Elieneza Nsanganzelu kazi kubwa umeifanya, vijana wanapiga mpira haswa na ni watulivu.

Sasa TFF vijana hawa wasipotee kabisa tunataka kuwaona kwenye AFCON 2027

Screenshot 2026-05-28 212843.png
 
Tanzania U 17 vs Misiri U 17 head to head

13/10/ 2012 Tanzania U 17 3-0 Egypt U 17
27/10/ 2012 Egypt U 17 0 vs 3 Tanzania U 17
17/3/2025 Egypt U 17 0-1 Tanzania U17
Leo 28/5/2026 Egypt U 17 0-1 Tanzania U 17
Hawa vijana wasiposifiwa na kupambwa na media, na zile hamasa mara nyingi tunafanikiwa.
Sasa kesho Manara au Makonda akishaamka nao tu watafungwa.
Ile serengeti ya kina Kelvin John ilianza vizuri mno kwenye zile friendlies.
walipoimbwa tu tulifungwa mechi zote chini ya Oscar Mirambo.
 
Serengeti Boys wameandika historia kwa kutinga Fainali ya AFCON U17 baada ya kuiondosha Misri kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 za mchezo mkali uliochezwa usiku huu.

Hakika wanastaili pongezi nyingi sana. Hakika kocha Elieneza Nsanganzelu kazi kubwa umeifanya, vijana wanapiga mpira haswa na ni watulivu.

Sasa TFF vijana hawa wasipotee kabisa tunataka kuwaona kwenye AFCON 2027

well done Serengeti Boys 👊🔥
 
Yohana nkomola, alipotelea wapi.
Alikuwa na wenzie kina kibabage, Ramadan kabwili, Ally Ngazi, Kelvin Nashon, Ally Msengi, Israel mwenda, Jobs nk.....Serengeti boys ya 2017...walitakiwa watoe droo tu, wakafungwa na Niger, wakafeli kufuzu world cup ya vijana....
Yohana Nkomola baada ya kuachana na yanga alitimkia wapi?
 
kwa kweli hawa majamaa hawana dalili zakuwa na miaka 17, wengine sura zimeshakomaa kabisa, Hata aibu tunakosa.
Inasikitisha sana
 
Hawa madogo wanafanya vizuri huu ndio muda wa wale wanaojiita mawakala na mameneja kuchukua wachezaji, kuinvest kwao na kuwatafutia timu zitakazo wakuza. Sio timu zinawachukua ,dogo akionekana na potential ndipo mnaanza kujipachika umeneja/uwakala, baadae timu zilizo wakuza wakianza kudai hela ndefu mnaanza kutafuta huruma kwa jamii.
 
Jitihada kubwa zimefanywa na vijana pamoja na benchi la ufundi, ila tayari wanasiasa wameshaanza kujitafutia ujiko.
 
Baada ya fainali kuisha tutabaki tunasimulia kuwa Angalau tumefika fainali.
U-17 Morocco.
 
Back
Top Bottom