Serengeti Boys yatwaa ubingwa wa Ferwafa U17 Kigali 2019

Serengeti Boys yatwaa ubingwa wa Ferwafa U17 Kigali 2019

Mathayo Fungo

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2018
Posts
319
Reaction score
511
Timu ya vijana Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys imetwaa ubingwa wa michuano ya vijana iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la Rwanda (FERWAFA) baada ya sare ya mabao 3-3 na wenyeji Nyigu Wadogo mjini Kigali jana Alhamisi. Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na John Edmund mawili dakika (28 na 49) na Edson Mshirakandi dakika ya 89. Vijana wa Rwanda mabao yalifungwa na Rutonesha Henson dakika ya 18, Nsanzimfura Keddy dakika ya 20 na Isingizwe Rodrigue dakika ya 94.
Kwa sare hiyo, Serengeti Boys ilimaliza na pointi nyingi zaidi, nne kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Cameroon kwenye mchezo kwanza Aprili 1. Cameroon imefuatia kwa pointi zake tatu baada ya kuifunga Rwanda 3-1 Machi 29 kwenye mchezo wa kwanza na kwa matokeo hayo wenyeji wameshika mkia kwa kuambulia pointi moja.
Michuano hiyo ilikuwa matayarisho ya mwisho kwa Serengeti Boys kabla ya kuingia kwenye Fainali za Kombe ka Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, (AFCON U17) katikati ya mwezi ambazo wao ndiyo wenyeji.



sere.JPG


Kila la heri vijana wetu Serengeti Boys. . . . #NiZamuTetu bado inaendelea.💪💪💪
 
Kwenye AFCON watatoka hatua ya makundi hawa madogo hawajitumi kabisa kama wale waliopita waongeze juhudi kama wanataka wafuzu kombe la dunia
 
Mwanzo mzuri, Hongera sana vijana wa Serengeti, Kila la kheri kwenye mashindano ya AFCON U17
 
Yule kipa wao wajipange upya....anafungwa magoli ya mbali sana, sijui ni ufupi. Pia awe mtulivu, goli la mwisho la Rwanda ni mpira ulimponyoka mikononi.......nina mashaka nae kama ndio tegemezi lao.
 
Kwenye AFCON watatoka hatua ya makundi hawa madogo hawajitumi kabisa kama wale waliopita waongeze juhudi kama wanataka wafuzu kombe la dunia
Game ya Rwanda uliangalia au umesimuliwa tu?
 
Back
Top Bottom