Series (Special thread)

Wakuu natafuta hii TV Show inaitwa Journey to the West. Ni series moja popular kwa kizazi cha miaka ya 90s.

Nikipewa direct download link yenye English subscribe itakuwa poa sana.
Vincenzo Jr msaada wako unahitajika hapa.
 
Jack Ryan wamefeli kwenye kuonesha kwamba USA wana akili sana huku mataifa mengine hata makubwa ya Ulaya hayana kitu. Hapo tu wamezingua
Sasa mkuu wewe ulitaka waoneshe mataifa mengine kuwa ni bora? Hizi muvi tunazo angalia zimebeba ajenda nyingi ndani yake.
1. Kutukuza teknolojia ya nchi husika
2. Kutukuza vyombo vya usalama vya nchi husika kwa lengo la kuwatisha wengine
3. ushoga
4. Kula muda wa mtqzamaji asiwaze mambo mengine ya msingi.
5. Kudhoofisha industries nyingine za uigizaji kwenye nchi masikini kama tanzania. Leo mtu upo tayari kuunguza GB za kutosha ukitafuta muvi za zamani kama predator au deadly prey lakini hauko tayari kuchoma GB ili udownload muvi inaitwa shamba kubwa au misukosuko.

Upo tayari kuangalia spiderman ila sio nsyuka au muvi nyingine za musa banzi n.k

HIVYO USIFHANI WAMEZINGUA KWA BAHATI MBAYA BALI NI MAKUSUDI

NB: UPO TAYARI KU SUBSCRIBE NETFLIX, HULU, APPLE TV, AMAZON NA NYINGINE NYINGI ILA SIO KULIPIA KIFURUSHI KWENYE DECODER ILI UFUATILIE MZANI WA MAPENZI N.K
 
Point yangu ni simple sana, ATLEAST MOVIE/SERIES IAKISI UHALISIA ULIOPO. Utakuta series kama Strike Back waingereza watatu tu wanaua maelfu ya majasusi na makomando wa Kirusi...sasa unajiuliza kama Russia Federation anaweza kuyakalisha mataifa zaidi ya 50 pale Ukraine vipi Hawa askari watatu tu.

Ila mkuu nimekuelewa katika point zako ninachozungumzia mimi ni wajipendelee ila wasizidishe sana, Mataifa ya dunia ya kwanza hayatofautiani sana katka mambo ya kiusalama tofauti ni idadi ya wanausalama na rasilimali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…