mkuu acha tu... yaani Power ni moja ya series ambazo nazisubiri kwa hamu sana!
Tukija suala la Executive Producers, hii inategemeana sana na scale of production lakini kimsing, EP ndie boss katika utenegenezaji wa mzigo husika. Huyu ndie mtoa pesa ku-cover gharama zote za utengenezaji filamu or series. Kwa Hollywood, EPs wengi wanakuwa ni wawakilishi wa Production Studios or sometime Distribution Company. Kwa mfano, ukichukulia Power, option ya kwanza inaweza kuwa ama Studio X or Distribution Company Y inatoa pesa kwa ajili ya utengenezaji wa Power na kumteua 50 Cents kama msimamizi wa Project mzima katika kuhakikisha mzigo unatengenezwa kutokana na standard zinazokubalika na suala zima la malipo kwa kila hatua. Kwahiyo, atakachofanya 50 ni kutafuta Producer na kumtengenezea bajeti kisha yeye 50 kufanikisha bajeti husika on behalf of ama hiyo studio au kampuni ya usamabazaji.
Option ya pili, na hii ndiyo naipa uzito zaidi kwa case ya 50 Cent ni kwamba inawezekana ni 50 Cent mwenyewe ndie anafanikisha bajeti ya utengenezwaji wa Power... kwamba anatumia pesa yake mwenyewe badala ya kuiwakilisha kampuni nyingine. Hii ni sawa sawa na hapa Bongo wewe
Innocizy unaweza kuwa na idea au script tayari na pesa ya kutosha na kwamba unataka kutengeneza fialmu. Utakachofanya ni kuongea mathalani na Mtitu ambae atafanya kazi kama Producer na wewe utagharamia kila kitu... katika mazingira kama hayo, Mtitu atabaki kuwa Producer (unless kama atachukua na roles zingine) na wewe utakuwa ndie Executive Producer. Lakini hapo hapo kwa mfano wa Mtitu... inawezekana badala ya wewe kuchangia 100% ya gharama, kinyume chake Mtitu nae anaweza kuchangia sehemu ya gharama. Inapotokea hivyo, wewe utakuwa Executive Producer kama kawaida na Mtitu atakuwa Producer and at the same time Executive Producer.