Serikali tatu ni 'uchuro'...ili tuishi bila kuzozana....kuna njia mbili kuhusu hili:-
...moja..kuwa na serikali moja tu ambayo itaifuta serikari ya Zanziba na itafutilia mbali matumaini ya kurejesha serikali Tanganyika. Tuwe na rais mmoja, bunge moja , jeshi la polisi moja, jeshi la magereza moja, mahakama kuu moja, jaji mkuu, mmoja, waziri mkuu mmoja, spika mmoja nakadhalika na kadhalika.
...mbili...kuwa na serikali mbili ambazo ni serikali huru ya Zanzibar na yenye mamlaka kamili huku ikiwa na kiti cha uwakirishi Umoja wa Mataifa na nyingine Serikali huru ya Tanzania Bara yenye mamlaka kamili huku ikiwa na kiti cha uwakirishi Umoja wa Mataifa
Kinachotakiwa ni kuwaunga mkono wazanzibari wengi ambao hawataki kujiondoa kwenye muungano ila wanalazimishwa na viongozi wachache wasiyouta muungano maslahi wanayoyajua wao. Wazanzibari hawa walio wengi wakiuungwa mkono tutapata Tanzania yenye serikali moja na rais mmoja.