Serikali acheni kuwafunga Waethiopia/Wasomali, wana-hustle tu kama sisi

Utaratibu huwa wanarudishwa kwao, au utaratibu umebadilika maana hata Watz miaka ya 90 wamefanya sana safari za namna hii achilia mbali za kudandia meli na kutoswa baharini! Wengi walikuwa wanarudishwa kwa ndege na walikuwa wanapigwa faini 10,000
mpaka kesho inafanyika bado ila siku hizi ukifika unapigwa miezi sita
 
Nimewaza hili long time, hawa watu adhabu kubwa warudishe walikotoka, vinginevyo tuwaache tu na hustle zao wanaenda mbali hawa na huko wakifika neema hii hapa wanapewa.
 
Hivi wanawezaje kupita katikati ya nchi ya Kenya kwa mamia halafu waje kukamatiwa Tz?

Ni kwamba Kenya hawana sheria inayohitaji vibali kuingia kwao au idara za usalama ndiyo ziko hoi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…