Serikali: Aliyedai mtoto kageuka jiwe alidanganya. Alijifungua mtoto 1 wa kike na alikuwa kaweka ahadi ya mtoto wa kuime

Serikali: Aliyedai mtoto kageuka jiwe alidanganya. Alijifungua mtoto 1 wa kike na alikuwa kaweka ahadi ya mtoto wa kuime

Kila siku tunaimba humu kuwa haluna uchawi wala mchawi. Ila maigizo na stori stori na habari za kutunga tu.

Achaneni na hizi imani za ushirikina, uchawi na waganga wa kienyeji zinarudisha nyuma sana maendeleo yetu.
Wacha kabisa, bado mtoto wewe huijui dunia.
 
Wale mashabiki wa uchawi njooni tena uzi wenu huu!

Kutoka 7:22-25​

Lakini wachawi wa Misri kwa kutumia uchawi wao wakafanya vivyo hivyo. Kwa hiyo moyo wa Farao ukabaki kuwa mgumu, naye
 
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt.Khalfany Haule amesema taarifa ya uchunguzi iliyofanywa kuhusu sakata la Mtoto kugeuka jiwe Musoma imethibitisha bila shaka kuwa hakuna aliyezaa jiwe wala hakuna Mtoto aliyegeuka jiwe bali Amina Abdallah aliyemuahidi kumzalia Hamis Mtoto wa kiume kisha akamzalia wa kike aliamua kuokota jiwe na kulipeleka kwa Wakwe na kuzusha alizaa Mapacha lakini Mtoto wa kiume amegeuka jiwe huku akitaka lizikwe haraka kuondoa mikosi.

DC Haule amesema “Amina Mkazi wa Katoro Chato alihamia kijiji cha Mwabuki Bariadi akiuza pombe za kienyeji, kuhudumia vinywaji Bar na uhudumu wa Gesti, tarehe 27/3/2023 alijifungua Mtoto wa kike Zahanati ya Mwabuki akiwa ni Mtoto wake wa tatu aliozaa na wanaume tofauti (Kila Mtoto na Baba yake), Mtoto huyu alizaa na Hamisi mwenye Makazi yake Mungaranjabo, Buhare hapa Musoma, Amina alimuahidi kumzalia Mtoto wa kiume Hamisi lakini kwa bahati mbaya Mtoto aliyezaliwa alikuwa wa kike”

“Hamisi yupo Dar na alituma nauli ili Watoto wapelekwe kwa Bibi yao Buhare Musoma, Amina alianza safari April 13,2023 akapanda basi akiwa na jiwe alilolichukua kwenye mawe ya ujenzi wa nyumba ya Mzee Mirembe wa Mwabuki alikokuwa anaishi, alifika Musoma saa 3 usiku na kupokelewa na Wenyeji wake na kuzusha Mtoto wake pacha aitwaye Amiri ameguka jiwe na kutaka azikwe usiku huohuo ili kuondoa mikosi”

“Kamati imejiridhisha kuwa Amina alikuwa na makubaliano na Hamisi ya kumzalia Mtoto wa kiume tangu mwanzo wa mahusiano yao hivyo Hamisi akaendelea kulea mimba akitarajia Mtoto wa kiume, baada ya kujifungua Mtoto wa kike, Amina aliendelea kumwaminisha Hamisi kuwa amejifungua pacha wa kike na kiume, pia hali duni ya maisha ya Amina kuhudumia Familia ya Watoto watatu ilichangia kusema uongo huo, hakuna Mtoto aliyegeuka jiwe, Wananchi msiamini miujiza”


Pia soma: Musoma: Mtoto afariki na kugeuka jiwe

Hiyo atakuwa mtanzania halisi. Ujuaji mwingi. Apache vipi kupiga nyungu huyo?
 
Hivi Bi Amina anatuonaje? Kutulia denge sisi na jiwe lake la kuokota.
 
Angalau sikupoteza muda kusoma hiyo thread nilijua tu ni uzushi
 
Wacha kabisa, bado mtoto wewe huijui dunia.
Bora nisikue tu, maana kama kukua ndio huko kwa akili timamu kabisa serious unaamini binadamu mwanamke anaweza akazaa jiwe. Kama serikali kukanusha hizo stori na tungo za huyo mwanamke kuzaa jiwe zilikuwa zishaaminiwa na wajinga na kuzisambaza.

Hakuna cha wacha kabisa ushirikina uchawi na wachawi ni stori, tungo na habari zinazoaminiwa na wajinga tu.
 
Back
Top Bottom