Serikali andaeni mfumo wa kudhibiti wizi wa pikipiki

Serikali andaeni mfumo wa kudhibiti wizi wa pikipiki

Ntunzima

Senior Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
136
Reaction score
145
Waasalamu Wakuu.

Kumetokea wimbi la wizi wa pikipiki za vijana wetu ambao wamechagua hiyo kazi kujiingizia kipato.
Hali inazidi kuwa mbaya maeneo mbalimbali mpaka inaonekana kuendesha boda boda ni kazi ya hatari.
Lakini wizi huu umetokana na serikali kushindwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa hivyo vyombo.
Nashauri waandae mfumo ambao utawezesha askari wetu wa baraban kuzifanyia ukaguzi hizo pikipiki na kuziwekea stika kwa zile ambazo zimeshakaguliwa kila baada ya muda fulani. Na pia washirikishe ulinzi shirikishi baina ya jeshi la polisi na vyama vya boda boda mahali husika.
Ina huzunisha mtoto wa masikini anapoteza kitega uchumi chake afu hakuna kichofanyika ili kukwamisha biashara za pikipiki za wizi.
 
Hapo mkiambiwa mtoe hela mtaanza kulalamika Tanzania kila kitu watu wanalalamika hilo zoezi sio bure kuvaa helment askari wamejitahidi mpaka basi bila mafanikio yaani kiufupi boda boda ni wajeuri pambaneni na hali yenu
 
Kawaida ukinunua chombo unafunga gps system na unakua unaweza kufuatilia chombo na jambo lingine bodaboda hawana muda wa kuuliza mtu anaenda wapi na usalama wa eneo hilo.

Naongea hivi kwakua nimeshajihusisha na boda boda kwa miaka kadhaa nyuma nikiwa najitafuta na hata leo nikiwa na ka tvs kangu nikipata abiria lazima nihoji wapi aendako na mazingira yapoje.
Kweli boda boda imekua kazi ngumu sana ila umakini uwepo.

Kikubwa ni kuweka system ya ulinzi na kupaki sehemu yenye ulinzi wengine wanalala na pikipiki ndani inahatarisha sana maisha na inakua rahisi kuja kuibiwa.
 
Umeongea point Mkuu. Bodaboda hawana Muda wa kuhoji abiria au kumkatalia abiria. Tamaa ya kipato ndo inayowaua. Saa 2 usiku unakodiwa kumpeleka Mtu umbali wa km 30 tena maporini unakubali kisa umeahidiwa 10,000?
 
Hapo ndipo tatizo linapoanza. Ugumu wa kazi nao umechangia mtu anaangalia pesa kabla ya usalama
 
Back
Top Bottom