Serikali: Ardhi ya Tanzania ni mali ya Umma siyo ya Kabila moja, Katiba imemkabidhi Rais wa JMT aisimamie

Serikali: Ardhi ya Tanzania ni mali ya Umma siyo ya Kabila moja, Katiba imemkabidhi Rais wa JMT aisimamie

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa Maliasili na Utalii Dr Damas Ndumbaro ametoa kauli ya serikali kuhusiana na mgogoro wa Ngorongoro. Dr Ndumbaro amesema ardhi ni mali ya Umma wa watanzania siyo mali ya kabila fulani na katiba ya JMT imempa Rais madaraka ya kuisimamia, kuiendeleza na kulipa fidia panapohitajika.

Ndumbaro amesema kwa sasa mkuu wa mkoa wa Arusha yuko kwenye majadiliano na mailagwanani wa kabila la Wamasai na akikamilisha ndipo tume ya serikali itakwenda na kuandaa ripoti ambayo itakabidhiwa bungeni.

Chanzo: ITV
 
Naendelea kusema Masai kaeni na serikali angalieni mambo ya msingi kadhaa;

Jadili kiasi Cha fidia kwa wahanga
Jadili ardhi/eneo mnalopelekwa ukubwa wake na upatikanaji wa malisho
Jadili upatikanaji wa huduma muhimu Kama shule , hospital, barabara, maji, usalama nk
Jadili muda ambao mnahisi mtakuwa tayari mmeondoka hapo mbugani.

Kuendelea kubisha kwamba hamtaondoka hautawasaidia hata kidogo tena mshukuru serikali ya awamu hii ya sita angekuwa Magufuli mnayemtaja angewaondoa bila fidia hata shilingi Mia wala kuwasaidia mkakae wapi.

Ulizeni watu wa ubungo-kimara, pamoja walikuwa na amri ya Mahakama wasibomolewe Ila Magufuli alibomoa na hakujali kitu na aliyepiga picha alikuwa anapotezwa ndio maana hata picha hazijaonekana.

Sasa msifanye serikali iamue hayo, ardhi ipo chini ya Rais, whether anapewa mwekezaji au wameona kweli kabisa kuna uharibifu wa mazingira wanaousema hiyo kwa sasa sio mjadala tena, nadhani mjadala wajikite kuangalia wanaondokaje, hili ndio la msingi.

Sheria ya ardhi imetamka wazi kabisa Sasa waendelee kujadili kwamba wanaondolewa anapewa mwekezaji kwani Rais aliamua muondoke aweke mwekezaji Kuna tatizo au ndio mara ya kwanza kusikia hilo? Watu wamepisha ujenzi wa reli, ujenzi wa airport chato, Mara bukoba nk, watu wamepisha uwekezaji Bagamoyo port wameliowa wakaamua kuondoka, yaani ishu ni umasai wenu??? No way kuweni wastaarabu hakuna mwenye ardhi hata Kama una haki Ila haki Ina mipaka.
 
Tigray ilianza hiv hivii,acheni kuwaonea makabila mengine hiyo ni asili yao
Inaanzaga hivi hivi mdogo mdogo halafu inashika mizizi then it'll be permanent major pain in our assses and many generations to come.
 
Wapigwe 200M each kama watabaki hapo,
Zile shida Tu, wakipewa hela lazima wake mjini kutesa
 
Umewaza mbali sana....wataelewa,wataondoka kwa amani bila kupoteza haki zao za msingi
Inaanzaga hivi hivi mdogo mdogo halafu inashika mizizi then it'll be permanent major pain in our assses and many generations to come.
 
Unazungumzia katiba ipi?Ni hii hii ambayo CCM wanaiogopa kuliko wanavyomuogopa Mungu hadi wanaharakati wa kutetea katiba mpya wanaitwa ni magaidi?!
 
Nchi za wenzetu na UN wanatambua na kulinda haki za indiginous na minority groups.....nyie ni kujitia ujuaji na ku apply ubabe eti watu hawana haki na ardhi bali rais ndo anamiliki ardhi nchi nzima, kama kuna watu wanasaka maslahi binafsi kwenye hili lazima liwatokee puani......muda utaongea.
 
Hao Maasai ndiyo a minority group kuanzia lini? Mbona wenzao kule Morogoro wamehamishwa ili kupisha ujenzi wa bwawa la Kidunda, au kuna baadhi wako sawa zaidi kuliko wengine (some are more equal than others - Animal Farm).
 
Morogoro kuna Wamang'ati siyo Wamasai bwashee!
 
Back
Top Bottom