Serikali Awamu ya Sita zuieni matukio ya utekaji wa wanaoikosoa Serikali, haileti picha nzuri

Serikali Awamu ya Sita zuieni matukio ya utekaji wa wanaoikosoa Serikali, haileti picha nzuri

Kama umegundua utekaji kwa 2024 umeshika kasi baada ya mkuu wa mkoa mmoja wa kaskazini aliyekuwa kipindi cha Magu kuingia madarakani.Nimeanza kuamini yeye anaendelezq Yale na ameingizwa kimkakati .Kwa serikali hii wasipoangalia wanachafuliwa na wananchi.huku chini wanaelewa
 
Rais Samia tunakupenda, tunakuheshimu, wewe ndio Dereva unayeendesha gari la Tanzania, sijui kama kweli hujui hila zinazoendelea ndani ya Serikali yako.

Wakati wa Magufuli makumi ya watu wametoweka na hadi sasa hawajulikani walipo akiwemo Ben Saanane, na wote waliotoweka walikuwa wakosoaji wakubwa wa Serikali.

Uliposhika usukani tulidhani tumepona kumbe ndo kwanza mambo yameanza upya Tena.

Watu wote wanaokosoa Serikali wanaendelea kupotea kwa kutekwa, na Ushahidi unaonesha kuwa Serikali inahusika vizuri mno, mfano ni kijana Sativa aliyetekwa na kupakiwa Karakana ya Oysterbay, mwingine ni Kombo Mbwana ambaye Tarehe 15/June/2024 alifuatwa nyumbani kwake na Police wakiambatana na mwenyekiti wa mtaa. Tangu wakati huo, Police wote wamekana kumshikilia Mbwana, yaani katika utawala wako tu, wamepotea wakosoaji zaidi ya 30.

Ndio sababu wasaidizi wako wakakushauri Twitter (currently X) ifungiwe eti inatukana viongozi, hakuna kiongozi yoyote aliyetukanwa Twitter, huko kumejaa wakosoaji tu.

Na kama kuna msaidizi wako alikushauri hilo lifanyike basi hakupendi hata kidogo.

Rais Samia, Duniani tunapita tu, it's just a blink of an eye, kisha Tunakufa na kusimama mbele ya Hukumu as according to our deeds.

Damu zisizo na hatia ni laana kubwa kwa Taifa, Damu huwa inalia mbele za Mungu ikidai kisasi, hakuna Damu inayomwagika bure bila kulipwa. Mwanzo 4:9-12.

Kukosoana tu ndio kupelekee Damu za watu kumwagika?

Rais Samia, usitoe sadaka yoyote kwenye madhabahu ya Mungu kama unajijua moyo wako si safi mbele ya Mungu.

Afrika imekuwa maskini kwa sababu ya laana za matendo yetu wenyewe!
CCM huwa hawafi ila wakosoaji tu.
 
Mi naamini Taifa la Tanzania 🇹🇿 ni Mungu tu anasaidia ila jitihada za kiongozi na viongozi sioni kama wapo taifa linajiendea tu!
 
Back
Top Bottom