Serikali badilisheni pori tengefu la Kibaha liwe eneo la makazi!

Charliemic

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2019
Posts
602
Reaction score
969
Naomba kuishauri serikali kupitia wizara ya Ardhi kuangalia uwezekano kubatilisha matumizi ya pori tengefu lililopo Kibaha mkoa wa pwani liwe eneo la makazi ya watu na matumizi mengineyo! Eneo hili lilihodhiwa na shirika la Elimu Kibaha ambapo kwa sasa shirika hilo limefutwa!

Pori hili likibatilishwa matumizi litapelekea kukua kwa mji wa Kibaha ambapo itasaidia kupunguza msongamano uliopo Dar es salaam
 
Lina ukubwa gani ?? Tupate viwanja hapo.....
 
Huwa najiuliza walio pita wangekuwa na tamaa za fisi kama hizi tungekuwa wapi.. ushauri wangu eneo la kibaha na eneo linalomilikiwa na chuo cha kilimo uyole mbeya yabaki hata miaka 100 mbele hivyo hivyo ndio wagawe maana kizazi hicho watakuwa na shida kuliko sisi
 
Kwani hawajagawana raia huko?

Pwani imejaa mapori
 
Tanzania ardhi ni kubwa siyo mng'ang'anie hapo karibu na Dsm. Kwanini usiende kujenga kwenu? Hilo pori ndio mapafu ya hiyo miji. Hujui umuhimu wa misitu mpaka leo? We mshamba kwenu wapi.
 
Maeneo ya wazo yabaki mfano sahivi dsm hakuna maeneo ya wazi kwa ajili ya mwanachi wa kawaida kwenda kupumzika tukitoa kila eneo itakua nchi ya hovyo sana
 
Maeneo ya wazo yabaki mfano sahivi dsm hakuna maeneo ya wazi kwa ajili ya mwanachi wa kawaida kwenda kupumzika tukitoa kila eneo itakua nchi ya hovyo sana
Nchi nzima iwe kama tandare kweli?????
 
Ndo mleta uzi anavyotaka
Nchi hii inaviongozi warafi sana ukiona panafuka moshi ujue pana moto. Siku wakianzisha hii hoja walala hoi wengi watawatetea wakitumaini kuwa watapewa wao kumbe watapewa vigogo. Nikuombe huu ujinga ukianzishwa tuu nitapinga na uniunge mkono
 
Tanzania ardhi ni kubwa siyo mng'ang'anie hapo karibu na Dsm. Kwanini usiende kujenga kwenu? Hilo pori ndio mapafu ya hiyo miji. Hujui umuhimu wa misitu mpaka leo? We mshamba kwenu wapi.
Hahahaha 😆🤣🤣🤣🤣 umeeleweka mkuu
 
Waacheni majoka kenge na wadudu wengine waishi huji

Ova
 
Hivi shirika la elimu kibaha limefutwa?
 
Mnapenda miji isiyo na free zones kwa ajili ya ku absorb cabondioxed na ku produce Oxygen?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…