Serikali chukueni hatua za haraka dhidi ya vodacom

Serikali chukueni hatua za haraka dhidi ya vodacom

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Hamjambo wote Wanahisa wa Vodacom. Nakumbuka Serikali yetu pendwa ilituhamasisha tuwekeze kwenye Kampuni ya Vodacom. Kiuhalisia Vodacom inafanya biashara sana na inapata faida kubwa.

Kwa kweli haiingii akilini kuwa Vodacom inatoa faida ya Tshs.10 kwa kila hisa ukichukua biashara kubwa inayofanya. Kama NMB inatoa wastani wa Tshs.100 kwa hisa iweje Vodacom inatoa Tshs.10 tu.

Ninaishauri Serikali kama bado wanaendelea na utaratibu huu wa kuwaonea Wanahisa basi ni vema wakafunga virago vyao na tupate Kampuni nyingine kama mbadala. Tunaiomba Serikali itusaidie sisi Wanahisa.
 
Hoja yako ina mantiki, na ni swali ambalo wanahisa wengi wa Vodacom Tanzania wanaweza kuwa nalo—kwanini mgawo wa faida (dividends) ni mdogo licha ya kampuni kuwa na biashara kubwa?
 
Tatizo nyie mnataka gawio la maana wakati mna hisa kiduchu labda kuanzia hisa 500-1000..wakati kuna watu humo voda wana hisa mpaka million kwa mamilioni level za kina rostam azizi hao ndio kidogo wanapata gawio zuri.. ww si ushawahi sikia rostam anauza hisa zake huko voda au tigo mpaka bilion 200 unadhani mchezo..ila nyie wenye vihisa uchwara sijui 200 hadi 1000 mkihurumiwa sana mnapewa 1000 tu
 
Hamjambo wote Wanahisa wa Vodacom. Nakumbuka Serikali yetu pendwa ilituhamasisha tuwekeze kwenye Kampuni ya Vodacom. Kiuhalisia Vodacom inafanya biashara sana na inapata faida kubwa.

Kwa kweli haiingii akilini kuwa Vodacom inatoa faida ya Tshs.10 kwa kila hisa ukichukua biashara kubwa inayofanya. Kama NMB inatoa wastani wa Tshs.100 kwa hisa iweje Vodacom inatoa Tshs.10 tu.

Ninaishauri Serikali kama bado wanaendelea na utaratibu huu wa kuwaonea Wanahisa basi ni vema wakafunga virago vyao na tupate Kampuni nyingine kama mbadala. Tunaiomba Serikali itusaidie sisi Wanahisa.
Kuwekeza kwenye hisa bongo ni pigo kubwa, Ila ukiwa ni preferential shareholder, ahhh mashallah, umeula
 
Ungeweka bei ya hisa hapo ingekua rahisi kujua kama divident ni nzuri au vipi.
Kwa kanuni za haraka haraka kama umepata sawa au zaidi ya faida benki zinazotoa kwa fixed deposit basi ni OK.
Kumbuka haya makampuni makubwa yanafanya audit kikamilifu na kuwakilisha hesabu zao serikalini TRA Ili walipe Kodi Kisha ndio divident
 
Back
Top Bottom