Serikali chunguzeni unyanyasaji, dhuluma na udhalilishaji unaofanywa na Mkuu wa Shule ya St. Margaret Maria Alokok, Igunga, Tabora

Serikali chunguzeni unyanyasaji, dhuluma na udhalilishaji unaofanywa na Mkuu wa Shule ya St. Margaret Maria Alokok, Igunga, Tabora

Mpangala2020

Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
8
Reaction score
14
Kimsingi sisi wazazi ndio waendeshaji wakuu wa shule hii kutokana na ada pamoja na michango mingine tunayolipa, pamoja na mambo mengine wazazi hatufurahishwi na vitendo vya udhalilishaji na dhulma anazofanya mkuu wa taasisi hii ambaye ni mtawa wa kanisa katoliki, kanisa lenye reputation ya kipekee nchini na duniani kwa ujumla,

1. Mtawa huyu amekua na Tabia za muda mrefu za kutukana na kutudhalilisha sisi wazazi bila ya kuangalia heshima na nafasi tulizonazo serikalini na katika jamii kwa ujumla, mkuu wa shule ambaye ukimpigia simu hapokei na akipokea amejawa viburi, matusi na dharau, suala hili ofisi ya elimu wilaya hata mkoa wanalifahamu pia jimboni na kwenye bodi ya shule tushapeleka malalamiko lakini ni mwaka wa pili hakuna suluhisho.

2. Watoto wetu hasa madarasa ya mitihani wanapoenda January kuwaona tena ni desemba, hili si sawa hata kidogo nao pia wanahitaji mapumziko ya kimwili na kiakili.

3. Kuna vikao vya wazazi kila mwaka lakini kinachofanyika ni kuwaandaa wazazi Fulani kuweza kuzungumzia masuala anayotaka yeye, sisi wenye mawazo mbadala hatupewi nafasi, tuna group la whatssapp la wazazi lakini ukionekana unahoji masuala yenye maslahi mapana kwa watoto wetu na walimu pamoja na wafanyakazi wote wa taasisi kwa ujumla basi unafutwa kwenye hilo group.

4. Serikali imezungumzia suala la kubakiza wanafunzi nyakati za likizo kwamba masomo ya ziada hayaruhusuwi watoto wapumzike, lakini yeye bado ametulazimisha kulipa Tsh 150,000/= kama gharama ya kila mwanafunzi wa kidato cha nne na cha pili mwezi wa sita achilia mbali Tsh.150,000/= gharama zingine za kulipia tour.

5. Suala la mkuu wa shule kutomfikisha mbele ya sheria mfanyakazi sekta ya upishi aliyempa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu mwaka Jana kimetuhuzunisha sana, badala yake anaamua kumfukuza mwanafunzi pekee hatulikubali abadani, pamoja na juhudi zote alizofanya mzazi kutafuta haki lakini vyote vilizimwa ili kumlinda swahiba wake kwa kuhonga pesa.

6. Watumishi wa taasisi hii ambao kimsingi ndio walezi wa watoto wetu na ndio wanaotumia muda mwingi kuwalea kuliko sisi wanafanya kazi katika mazingira magumu sana na hali hii ikiendelea itaathiri maendeleo ya watoto wetu kitaalamu, mf. kuwatukana mbele ya mwanafunzi wao haijengi picha nzuri ktk ustawi wa vijana wetu, pili wanafanya kazi bila ya mikataba ya ajira hili ni kosa kubwa na tunaomba waziri wa kazi atume jopo la wataalam idara ya kazi wafike baraka kulichunguza, mfanyakazi anapewa mkataba ajaze kisha anaambiwa apeleke kuna sehemu ambazo anatakiwa yeye ajaze akishapekeka ndio imetoka harudishiwi nakala ya mkataba kwa kisingizio kwamba zitapelekwa kwa mwanasheria wa jimbo kwa ajili ya muhuri Tabora, lakini imepita miaka zaidi ya miwili hakuna mfanyakazi mwenye nakala ya mkataba, wanafanya hivi makusudi ili iwe rahisi kwake kumfukuza mfanyakazi atakapojiskia na pia kumnyima stahiki zake pindi anafukuzwa kwa kuwa mkataba yote amezifungia kabatini kwake na hakuna mahali utaipata.

7. Kutokana na kutokua na nakala ya mikataba imepelekea wafanyakazi waliomaliza mikataba yao kunyimwa kiinua mgongo kadri ya mikataba yao na karibu 3/4 ya wafantakazi wanastahiki hayo malipo.

8. Kipindi ambacho shule zilifungwa kutokana na janga la covid19, wazazi tulilipa michango yetu kama kawaida ikiwemo ada, lakini cha kushangaza zaidi ni kwamba kwa kiburi na jeuri aliyonayo hakuwalipa wafantakazi wote mishahara yao kwa kipindi cha miezi miwili na hii ndo shule pekee ambayo haikulipa mishahara ya miezi miwili miongoni mwa shule zote za jimbo katoliki Tabora huu ni uonevu na ukandamizaji kwani mishahara ya wafantakazi tunatoa sisi kwa nini wasilipwe? Hali hii imepelekea ufaulu kushuka kwa kasi kwani awali enzi za mtangulizi wake mtawa consolata shule hii ilikua inashika nafasi ya kwanza kiwilaya na ya NNE kimkoa lakini Leo hii tumeanza hata kuhamisha watoto wetu kutokana na ufaulu kushuka na uongozi mbovu na dharau
Mwisho kabisa mkuu huyu hana mahusiano mema na uongozi wa elimu wilaya na hata mkoa kiburi na dharau kinapelekea adhindwe kutoa ushirikiano mzuri kwa wasimamizi wa elimu, lakini pamoja na hayo tunaomba kutoa pongezi kwa viongozi wa elimu wilaya kwa juhudi kubwa wanazofanya ktk kusimamia elimu.

Hivyo ni matumaini yetu kwamba serikali ya awamu ya sits chini ya Mama yetu na jemedari mkuu watafuatilia kwa ukaribu malalamiko yetu, nawasalimu ktk jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Mkuu, tafuta shule nyingine uhamishe mwanao... Usipoteze muda wako kulalama!!
Mkuu hii issue tumeiadress kwa serikali ww wala haikuhusu, na kuhamisha mtoto haitokuwa suluhu ya tatizo so waachie wahusika wafanye ufuatiliaji
 
Acha watusumbue na pesa zao sas M'babe wao ameshafariki.
Vyombo husika fuatilieni hili, leo kwake kesho kwako
 
Sometimes unatumia akili.

Yeye anataka mtoto abaki wewe unataka mtoto arudi.

Ila ili abaki inabidi ulipie 150,000. Sasa si haulipi hiyo pesa ili mtoto arudishwe nyumbani kwa kukosa ada?

Hata hivyo nahisi kuna zingine ni chumvi siamini kama mkuu wa shule anaweza kua na nguvu na mamlaka kiasi hicho hata nje ya shule.
 
Acha watusumbue na pesa zao sas M'babe wao ameshafariki.
Vyombo husika fuatilieni hili, leo kwake kesho kwako
Mtu anakuambia hayo mambo ni ya muda mrefu wewe umefocus kuelezea umaskini wako.

Umaskini siyo sifa.
 
Huyu sio mzazi, ni mfanyakazi wa hiyo shule hayo mengine kaongezea kuficha utambulisho
 
Mambo mengine rahisi sana mhamishe mtoto
 
Mtu anakuambia hayo mambo ni ya muda mrefu wewe umefocus kuelezea umaskini wako.

Umaskini siyo sifa.
Shule za binafsi zina taratibu zake. Shule za kanisa ukitaka kutatua matatizo yake hasa ya kiutawala na nidhamu peleka malalamiko yako kwa wenye shule (kanisa/askofu). Serkalini peleka malalamiko ya kukiuka syllabus.
 
Duu kwani lazima asomee hapo. Yaani nawaza namna ya mwanangu kusoma huru pasipo kupangiwa kusoma twisheni Kama walimu hao wanaosisitiza twisheni why wao hawakusoma ili wafaulu zaidi wakaishia kupata alama ndogo wakaenda kusoma kazi za hela ndogo. Kusoma twisheni sio solution am sure.
 
Duu kwani lazima asomee hapo. Yaani nawaza namna ya mwanangu kusoma huru pasipo kupangiwa kusoma twisheni Kama walimu hao wanaosisitiza twisheni why wao hawakusoma ili wafaulu zaidi wakaishia kupata alama ndogo wakaenda kusoma kazi za hela ndogo. Kusoma twisheni sio solution am sure.
Utamaduni tuliozoea Tanzania ndiyo unasababishia matatizo zaidi. Kama kweli hiyo shule ina matatizo kama huyu jamaa anavyosema dawa ni wazazi kuji-organize na kuhakikishia matatizo yameondoka. Kama kikwazo ni huyo mkuu wa shule basi aondolewe. Ukihamisha mtoto wako hujatatua tatizo na ni ubinafsi kwani ataendelea kutesa watoto wengine. Hii nchi mimi inashingaza sana sana. Watu waoga na wanafiki kupitiliza. Yaani mkuu wa shule afanye uhuni kama huo na wazazi badala ya kuchuwa hatua wanakuja kuandika malalamiko yao hapa?
 
Utamaduni tuliozoea Tanzania ndiyo unasababishia matatizo zaidi. Kama kweli hiyo shule ina matatizo kama huyu jamaa anavyosema dawa ni wazazi kuji-organize na kuhakikishia matatizo yameondoka. Kama kikwazo ni huyo mkuu wa shule basi aondolewe. Ukihamisha mtoto wako hujatatua tatizo na ni ubinafsi kwani ataendelea kutesa watoto wengine. Hii nchi mimi inashingaza sana sana. Watu waoga na wanafiki kupitiliza. Yaani mkuu wa shule afanye uhuni kama huo na wazazi badala ya kuchuwa hatua wanakuja kuandika malalamiko yao hapa?
Hili suala kwa Kilimanjaro nadhani halipo kusema ukweli,yaani elimu inasaidia sio upole mnajidai kuwa Ni haki na watu kudhulumiwa haki zao ama kunyanyaswa. Na Ntarime sidhani Kama mkurya anakubali kunyanyaswa Mana Ni fasta mmemalizana naye.


Ukweli umeongea Ile watu wanamaindi kwa pamoja yaani wazazi wanasimama kidete. Yaani uninyanyasie mwanangu na huku nakulipa na sio kuwa unanipa mtaji ndipo utakapojua keisangora Ni Nani.


Binafsi mfumo wa elimu ulivyo napingana nao mno yaani mno jamani mpaka nawaza niwe na independent school like Elon musk. Napenda shule ambao Ina incourage Innovation yaani sitaki mwanangu apate A Ila aweze jua how to solve the problem katika jamii yake.
 
Back
Top Bottom