Serikali fanyeni hata hivi basi

Serikali fanyeni hata hivi basi

Mechanic 97

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2021
Posts
854
Reaction score
1,296
Serikali ya CCM chini raisi Samia Suluhu Hassan. Naomba sisi vijana tulio soma iwe kuanzia form four(aliyefaulu) or Veta(NVC 3) na kuendelea kwenye hiyo miradi na huku mitaani na mtuwekee kipaombele/ au mazingira wezeshi Yaani Kwa mfano haya makampuni ya kichina yanayo jenga miradi ya serikali na yenye viwanda hapa tanzania ya pewe udhibiti wa aina ya wafanyakazi ambao itatakiwa kua ajiri sio kuajiri Kila mtu kitu kinacho sababisha rushwa iwe juu. Kwahiyo haki ya vijana Wenye weledi inapotezwa.

Na huku mitaani jaribuni kuwawekea mazingira wezeshi Hao walio soma Kwa kuwabana Kwa sheria ambao walikimbia shule. Kwa mfano ni vizuri kumlinda fundi simu Alieishia form six labda PCM kwa kuwa ataweza kwendana na mabadiliko ya sci-tech na ataweza kucopy tech mpya kuliko kuendelea kuwakumbatia wajinga ( unakuta fundi redio capacitor anaita Kitenki). Kupitaa hivi utawafanya wasomi wapate faida na kufikiria kufika mbali zaidi na kuwa ajiri hao walio kimbia shule
 
Tatizo kubwa la sisi vijana wa kitanzania ni uvivu, kazi kidogo tunataka maslahi makubwa, yaani ule uchapakazi wa kujituma hatuna tunaona kama tunamfaidisha boss
 
Tatizo kubwa la sisi vijana wa kitanzania ni uvivu, kazi kidogo tunataka maslahi makubwa, yaani ule uchapakazi wa kujituma hatuna tunaona kama tunamfaidisha boss
Sema Kwa hii mkuu ni Kwa wote. Na sana sana Kwa Hawa wasio na elimu huwa Wanamuibia sana mchina Kwa vile hata umuhimu wa miradi wanakua hawautambui
 
Sema Kwa hii mkuu ni Kwa wote. Na sana sana Kwa Hawa wasio na elimu huwa Wanamuibia sana mchina Kwa vile hata umuhimu wa miradi wanakua hawautambui
vijana wa kitanzania huwa wanawaza kupiga(kuiba tu) na sio kuendeleza taasisi ndo maana unaona taasisi akipewa mtanzania lazima ife, hatuna ile kufanya kazi kwa bidii ili nijiongezee ujuzi katika eneo langu
 
Mbona mlivyofaulu darasa la saba hatukuwaombea mabaya....iweje Leo mtuombee njaa[emoji3061][emoji3061][emoji3061]
Mkuu nyinyi mlio soma kabla ya shule za kata nyinyi ni form four leaver Kwa kulinganisha na form four ya Sasa. Kwa maana baada ya shule za kata swala la sekondari lilikua ni Kila mmoja hivyo nyinyi hamuhusiki na hii kwanza wengi wenu sio vijana
 
Acha ushindani uwepo
Yaaani uchanganye kijiko kimoja Cha sukari kwenye ndoo ya maji na utegemee ikolee yaani hata sukari itakuwa maji. Yaaani ushindanishe msomi mmoja kwenye kata na wajinga kumi kwenye kata yaan hata msomi mjinga na anaweza hata kuhama ndio maana wasomi wanabaki kugagania mjini Wanajua jamii inavyo wahakumu huku nje eti utakuta wanasema " nae anafanya Vitu ambavyo hata wasio soma nao wanafanya"
 
Ahahaha 🤣 🤣 🤣
Mwajiri ndiye ana haki nambari 1 kuchagua aina ya mtumishi ampendaye.

Kama rushwa anayekula ni Mtanganyika mwenzako wala usimbebeshe mzigo Mchina.

Kosa ni la wazazi na ndugu zako wanaosema CCM ni kama baba yao.

CCM imeshindwa kutumia rasilimali lukuki.

Nchi inayoongoza kwa rasilimali ina vijana jobless, hatari sana
 
Ahahaha [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
Mwajiri ndiye ana haki nambari 1 kuchagua aina ya mtumishi ampendaye.
Kama rushwa anayekula ni Mtanganyika mwenzako wala usimbebeshe mzigo Mchina.
Kosa ni la wazazi na ndugu zako wanaosema CCM ni kama baba yao.
CCM imeshindwa kutumia rasilimali lukuki .
Nchi inayoongoza kwa rasilimali ina vijana jobless, hatari sana
Hata hao wachina japo kuwa hawakagui vyeti ila wanapenda watu Wenye uwelewa wa hali ya juu yaani ambao wanaweza wakaelewa kazi Kwa mdaa mchache kuna site nilienda kuna Jamaa ana degree ya art lakini alijifunza kusoma mchoro plus kuongee kingereza vichina vikamuongeza 1000 Kwa siku na ndio nilimkuta kama msemaj wa watingaji.
 
Ahahaha [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
Mwajiri ndiye ana haki nambari 1 kuchagua aina ya mtumishi ampendaye.
Kama rushwa anayekula ni Mtanganyika mwenzako wala usimbebeshe mzigo Mchina.
Kosa ni la wazazi na ndugu zako wanaosema CCM ni kama baba yao.
CCM imeshindwa kutumia rasilimali lukuki .
Nchi inayoongoza kwa rasilimali ina vijana jobless, hatari sana
Japo ni kweli CCM inazingua
Vijana walio jitolea kupenda elimu na wazazi wali jitolea kusomesha watoto wao CCM inawakosea sana
 
Back
Top Bottom