Serikali fikirini kimkakati kuhusu reli ya Dar es salaam - Moshi-Arusha

Serikali fikirini kimkakati kuhusu reli ya Dar es salaam - Moshi-Arusha

Upekuzi101

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
221
Reaction score
542
Habari wana jf.
Leo napenda kuwasilisha wazo la kimkakati linaloweza kuharakisha maendeleo ukihusisha miundo mbinu ya reli hasa Kanda ya kaskazini. Ili kuboresha biashara hasa na washirika wetu wa Afrika Mashariki tunatakiwa kuwa na reli ya SGR ukanda huu. Arusha na Moshi ni eneo la karibu kabisa na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na njia ya moja kwa moja kuelekea hadi Congo. Kungekuwa na reli itakayotembea at least kilometers hizi 500 kwa at least saa 4 au 5 kutoka Arusha kwenda Dar es salaam basi miji ya Kanda ya kaskazini ingekua zaidi kibiashara maana ingekuwa rahisi kwa mfanyabiashara kutoka Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na hata Congo kufika Arusha day 1 akalala hotel kesho yake Asubuhi anapanda treni labda saa 12 asubuhi saa 4 yupo Dar es salaam anafanya shopping ya mzigo labda for 3 hours then labda kwenye saa 8 au saa 9 treni inatoka Dar es salaam then saa 12 au hata saa 2 usiku mtu anakuwa amerudi Arusha au Moshi, kesho yake asubuhi mteja anapanda basi lake anarudi kwenye biashara zake uko Kenya, Uganda, Burundi hata Congo pia. Kwa kufanya hivi biashara za mahoteli na lodges itakua na inapokuwa biashara iyo automatic migahawa ya kuuza vyakula itakua zaidi, biashara ya vinywaji pia itakuwa na hata biashara nyingine ambazo zitaongeza ajira na vipato kwa watanzania. Mama Samia naomba wazo hili likikufikia naomba ulifanyie kazi kama itafaa, Kanda ya kaskazini Ina mchango mkubwa sana kwenye uchumi wa Tanzania kwaiyo itumike ni full potential kwa maendeleo ya nchi.

Wakosoaji na waboreshaji wa wazo hili mnakaribishwa kuchangia mawazi.
 
Mimi ningeshauri labda tungekuwa na Luxury Train kama za wenzetu duniani ambapo ni za kitalii zaidi

Yaani train ingekuwa inapita hata baadhi ya mbuga kwa mwendo mdogo huku watalii wakijionea wanyama

Nilipanda Orient Express na sasa natamani Maharaja
Wenzetu huko wanafaidi Dunia kwa kweli na watu wanapanda sana maana ukiangalia ndani unatamani usishuke
Baadhi ni hizi unaweza kuziangalia hata kwa picha

Maharaja Express (India)

Orient Express [emoji636]

Golden Chariot India

Ravos Rail proud of Africa (SA)

Hii ya South Africa inaenda mpaka Cairo
Na sisi tuwe na ya kwetu
 
Sgr ikiunganishwa kutoka Dodoma hadi Arusha. Arusha hadi Nairobi itakuwa poa sana
 
Mradi ufike Mwanza kwanza alafu kwa upande wa Arusha najua mradi uko mbioni kuanza. Hili ni swala la muda tu.
 
Back
Top Bottom