Serikali futa matokeo ya Form 4 badala yake tumia matokeo ya Mock, 2012

Serikali futa matokeo ya Form 4 badala yake tumia matokeo ya Mock, 2012

Katika hali ya kawaida haiwezekani asilimia 60% ya watahiniwa wa form 4 wakafeli mtihani. Sote tunajua kwamba wanafunzi hawakufundishwa vizuri kwa sababu mbalimbali lakini kubwa ni mgomo wa kitaifa wa walimu mnamo mwezi wa saba japokuwa pilkapilka zake zilianza mapema kimya kimya bila kufundisha. Hivyo Serikali isipoingilia kati hali hiyo ili kunusuru maisha ya watoto malaika wasio na hatia itakuwa haikuwatendea haki.

Baada ya mgomo kufutwa walimu walienda Sensa, lakini hata waliporudi na shule zikafunguliwa walimu hawakufundisha kuwaandaa vizuri wanafunzi kwa ajili ya mitihani, hususan wale walimu ambao majina yao yaliondolewa kwenye orodha ya kuhesabu sensa dakika za mwisho kwa madai kwamba walikuwa vinara wa mgomo. Je, inawezekana kwamba walimu hao nao walichangia kwa kula njama za kulipiza kisasi katika usahihishaji ili kuikomoa Serikali? Inasikitisha kuona kwamba kuna wanafunzi waliokuwa wamepata Division 2 au 3 katika mock, lakini katika final wakafeli kabisa kwa Div 4 ya 35. Je, inaingia kichwani hiyo kwamba kufeli kwa wanafunzi kama hao ni halali yao?

Sasa ili kutenda haki na kuokoa maisha ya watoto wasio na hatia nashauri serikali ikubali kufuta matokeo ya f4 yaliyotangazwa hivi karibuni, badala yake serikali itumie matokeo ya Mock, 2012. Hapo idadi ya kushindwa itakuwa ya kawaida, isiyotisha. Hatua hiyo ichukuliwe haraka iwezekanavyo ili watoto wachaguliwe kwenda f5.

Achana na mambo ya Tume ya kisiasa ambayo madhumuni yake ni kupoza hasira za wananchi, kwani sababu za kufeli zinafahamika.
Mbona hueleweki ndugu unashngaa kwanini zaidi ya 60% kufeli wakati huo huo unaeleza kuwa walimu hawafundishi kutokana na sababu ulizotaja hapo juu, halafu unataka matokeo ya mock yatumike ili waende form 5 waktai unakiri kuwa hawakufundishwa sasa huko wanakwenda f 5 kufanya nini wakati hataua hii wakufundishwa na kufuzu,
 
Back
Top Bottom