Serikali haijaruhusu Kilimo cha bangi

Serikali haijaruhusu Kilimo cha bangi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Christina Rweshabura, ameyasema hayo leo mbele ya Wahariri wa vyimbo vya habari jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo ya mpango kazi kwa ajili ya kutambua mchango wa wanahabari katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu kuzuia na kipambana na dawa za kulevya.

Amesema Mwandishi wa Habari aliyesema Serikali kuruhusu Bangi, alimnukuu Vibaya. Amesema Duniani utafikti unaonesha kwamba bangi faida zake ni nyingi kuliko hasara zake. Hivyo amesema Sheria ya Madawa ya kulevya kifungu namba 12, kimepelekwa bungeni kufanyiwa marekebisho ili kama ikitokea Bangi imependekezwa kutumika, iwe kwaajili ya matumizi ya matibabu na Mkurugenzi Mkuu wa Madawa ya kulevya ndo atakuwa nanaidhinisha kwa Matumizi ya dawa na utafiti

=====
Christina Rweshabura: Ni mazao haramu lakini ikigundulika mazao hayo yanaweza kutumika kwenye tiba basi Sheria itabidi irekebishwe iandikwe kwamba bangi labda na mirungi na mazao mengine haramu yatalimwa kwa sababu maalum ya tiba na tafiti za kisayansi.

Sasa nashangaa kichwa cha habari kinasema kwamba Serikali yaruhusu kilimo cha bangi , Serikali itaruhusu kilimo cha bangi.

Peter Patrick Mfisi: Unajua tumetafsiri vibaya Mimi kwa mtazamo wangu hata uandishi sidhani kama kuna utata wowote kama ulivyosema jana kwamba tutabadilisha kifungu kwa sababu kifungu kilikuwa hakijaongelea kwamba kilikuwa kimesema tu kifungu cha 12 kwamba Kamishna Jenerali anaweza akaruhusu kilimo cha mazao



Capture 1.jpg
 

Attachments

Zile green house zangu nitaweka nusu bangi nibangue na nusu naweka nyanya ninyanyue.
 
Ukiona Bunge linadai ^Kenya wanafanya hivi^ ^Uganda mbona wamefanya vile^ ujue the so-called viongozi, uwezo wao wa kufikiri umegota mwambani. People are unsure whether we are going or coming back!?
 
Ukiona Bunge linadai ^Kenya wanafanya hivi^ ^Uganda mbona wamefanya vile^ ujue the so-called viongozi, uwezo wao wa kufikiri umegota mwambani. People are unsure whether we are going or coming back!???
Bunge la kijani
 
Back
Top Bottom