Serikali haipo kwa maslahi yetu bali kufanikisha upigaji wao

Serikali haipo kwa maslahi yetu bali kufanikisha upigaji wao

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Haiko hivi katika nchi zingine. NIsiache kumkumbuka yoga, kwetu ni kampuni la watu na familia zao.

Mifano ni mingi hata hivyo tuanzie na elimu ya juu, tuelewe ya loan board. Elimu ya juu rasmi ni private education isiyokuwa na ruzuku popote. Wanafunzi wanalipa malipo yote in full. Tuition fees, accommodation, vitabu, stationeries na vingine vyote.

Kwa hali hiyo budget ya wizara ya elimu kwa elimu ya juu ni kwa kazi gani?

Tuje hospitali ambako mazaga zaga yote ni ya kulipiwa. Kumwona daktari, operesheni, dawa, kulazwa, mortuary nk kote ni private services zinazolipiwa na wahanga wenyewe directly au indirectly kupitia bima.

Tujiulize tena bajeti za matrilioni wizara ya afya kwa ajili ya dawa mahospitalini ni kwa ajili ya nini?

Huku kunako mabehewa ya treni, umeme wa mgawo, maji nk ni mwendelezo wa upigaji ule ule ambapo kimsingi pana wao wenye kampuni na sisi tulio wateja, bidhaa na hata masoko.

Kodi, tozo, ada, faini mbalimbali, zinazoishia serikalini zina maslahi kwa nani? Polisi au mamlaka ipi Iko kusimamia maslahi ya nani?

Enyi mnaojiita wajumbe wa bodi na mameneja matawi wa hili kampuni lenu Mola anawaona.

Kwamba hamtaki hata tuhoji lolote linalotuhusu huku nyie mkiendelea kulambishana asali?

Endeleeni kujidanganya kuwa hatuwaoni na kwamba eti hatutakaa tuchukue hatua.
 
Wakisoma hili bandiko lako hapa utawakuta wanakuangalia kwa style hii hapa; 🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄
 
Haiko hivi katika nchi zingine. NIsiache kumkumbuka yoga kwetu ni kampuni la watu na familia zao.

Mifano ni mingi hata hivyo tuanzie na elimu ya juu tuelewe ya loan board. Elimu ya juu rasmi ni private education isiyokuwa na ruzuku popote...
Ngoja watetezi akina baptist na wenzake waje!!
 
Ni kweli ulichoandika, jamaa wapo kwa ajili ya kufanikisha mambo yao kupitia migongo yetu, na kwa sababu bahati mbaya sisi tumelala, basi wataendelea kututafuna kwa muda mrefu sana ujao.

Sisi watanzania ni watu wa ajabu sana, tumeridhika kufelishwa na hawa jamaa na tunaendelea tu kuwaacha waendelee kutufanyia majaribio yao, ni kama vile wametugeuza midoli yao, sasa wanatuchezesha wanavyotaka.
 
Wakisoma hili bandiko lako hapa utawakuta wanakuangalia kwa style hii hapa; 🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄

Ukweli wa wazi:

1. Elimu ya juu ni fully private education. Wanafunzi wanalipa Kila kitu. Wanaopata mkopo wanailipia elimu hiyo na riba juu.

2. Hospitali Kila kitu kinalIpiwa Hadi mortuary. Zote ni private hospitals.

3. Wananchi wanakamuliwa kodi, tozo, faini, rushwa nk kote.

4. Polisi barabarani, upelekezi, rumande na kwenye anga zao nani ana Cha kujivunia?

6. Nk nk.

Mwendelezo ule ule ambao wananchi wanakuwa hawana furaha katika nchi zao.

Kama vile haitoshi bajeti ma trillion Kila mwaka yanatolewa kwenda huko kunakolipiwa na watu.

Hayo macho na waangalie nayo tu. Hawa si wa kunyamazia.
 
Kibuyu Cha Asali Msikipasue

Elimu ya juu kupitia loan board wanafunzi wanailipia in full na riba juu ila bajeti pia inatolewa Kila mwaka kwa jukumu hili hili. Hiki kibuyu na kipasuliwe tu!
 
Ukweli wa wazi:

1. Elimu ya juu ni fully private education. Wanafunzi wanalipa Kila kitu. Wanaopata mkopo wanailipia elimu hiyo na riba juu.

2. Hospitali Kila kitu kinalIpiwa Hadi mortuary. Zote ni private hospitals.

3. Wananchi wanakamuliwa kodi, tozo, faini, rushwa nk kote.

4. Polisi barabarani, upelekezi, rumande na kwenye anga zao nani ana Cha kujivunia?

6. Nk nk.

Mwendelezo ule ule ambao wananchi wanakuwa hawana furaha katika nchi zao.

Kama vile haitoshi bajeti ma trillion Kila mwaka yanatolewa kwenda huko kunakolipiwa na watu.

Hayo macho na waangalie nayo tu. Hawa si wa kunyamazia.
Tanzania tumejaaliwa vitu vingi, na kunyimwa vichache muhimu;
mfano:-
-Ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo✔️
-Raslimali za kila aina i.e madini, mito, maziwa,nk.✔️
-Watu wa kutosha kwa ajili ya uzalishaji✔️
-Siasa safi ✖️
-Uongozi Bora✖️
-Uzalendo✖️
 
Haiko hivi katika nchi zingine. NIsiache kumkumbuka yoga, kwetu ni kampuni la watu na familia zao.

Mifano ni mingi hata hivyo tuanzie na elimu ya juu, tuelewe ya loan board. Elimu ya juu rasmi ni private education isiyokuwa na ruzuku popote...
Halafu kuna wakomaza Shingo utawasikia Magufuli alikuwa Dikteta!

Sasa wacha akili zitukae sawa,ili wenye kujitambua wasiurudie ujinga ifikapo 2025

#Kataawaguni
 
Ukweli wa wazi:

1. Elimu ya juu ni fully private education. Wanafunzi wanalipa Kila kitu. Wanaopata mkopo wanailipia elimu hiyo na riba juu.

2. Hospitali Kila kitu kinalIpiwa Hadi mortuary. Zote ni private hospitals...
Nakumbuka kauli ya juzi tu aliyoitoa Rais, Dr. Samia, alisema watanzania tulizoea vya bure, sasa tuanze kuvilipia.

Lakini kwa kuangalia hivyo ulivyoorodhesha hapo juu, sioni ni kitu gani watanzania walikuwa wanapata cha bure, sasa kama anataka tuanze kuvilipia, naona hali yetu ndio itakuwa mbaya zaidi.

Hapa ni kujiandaa kufunga mikanda tu, na ajabu zaidi ni pale tunapolazimika kujifunga mikanda, sehemu ambazo zilishatengewa bajeti!.
 
Ni kweli ulichoandika, jamaa wapo kwa ajili ya kufanikisha mambo yao kupitia migongo yetu, na kwa sababu bahati mbaya sisi tumelala, basi wataendelea kututafuna kwa muda mrefu sana ujao...
Kupambana na watu hawa inabidi kuunganisha wote wenye usongo nao bila kujali kwanini wana usongo nao. Hatuwezi kumwacha awaye yote mwenye usongo nje.
 
Waendelee hvyo hvyo,mpaka akili zitatukaa sawa tu
 
Nakumbuka kauli ya juzi tu aliyoitoa Rais, Dr. Samia, alisema watanzania tulizoea vya bure, sasa tuanze kuvilipia.

Lakini kwa kuangalia hivyo ulivyoorodhesha hapo juu, sioni ni kitu gani watanzania walikuwa wanapata cha bure, sasa kama anataka tuanze kuvilipia, naona hali yetu ndio itakuwa mbaya zaidi, ni kujiandaa kufunga mikanda tu, na ajabu zaidi ni pale tunapolazimika kujifunga mikanda, sehemu ambazo zilishatengewa bajeti!.

Hakipo tunachopata bure. Ni kuwa wanatukamua na kwa ukimya wetu
Wanaona kumbe wanaweza kutukamua hata zaidi.

Hivi ada mashuleni na huku vyuo vikuu nani anapanga au hata ku regulate tu?

Hivi Ile tume ya haki za mteja haina cha kufanya kama dhulumati ni serikali?

Wametugeuza kuwa viumbe wa kuwazalishia mali. Sisi na punda hatuna tofauti.

Bila shaka huku ndiko uliko ule msingi wao wa kulinda siri za serikali au baraza la mawaziri au zile atakazozigundua yeyote kwenye utendaji wake.
 
Waendelee hvyo hvyo,mpaka akili zitatukaa sawa tu
Kauli kama hizi zenye kuendelea kuwapa mianya ya kulamba asali wanazipenda sana. Hawachoki kutamka hadharani, kazi na iendelee.
 
Back
Top Bottom