GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Hivi kuna mtu asiyejua umuhimu wa mtoto kufahamu lugha ya Kiingereza katika karne hii? Kuna mtu asiyefahamu kuwa shule za St. Kayumba ni kwa ajili ya watoto wa masikini?
Unajua kwa nini miaka ya nyuma vigogo wengi walikuwa wakiwapeleka watoto wao shule za Kenya?
Kwa asiyefahamu:
1. St. Kayumba ni kwa ajili ya maskini
2. Shule za English medium ni kwa ajili ya wenye hela. Ndiko wanakosomea watoto wengi wa vigogo.
Sisi tuliosoma St. Kayumba tunafahamu changamoto tuliyoipata miaka ya mwanzoni Sekondari. Silaha kubwa tuliyokuwa tukiitumia ilikuwa ni kukariri. Unahamisha maelezo ya kwenye daftari kama yalivyo, lakini tungeambiwa tuelezee kwa Kiswahili, tusingeweza. Tulikuwa tukikariri kwa mafanikio makubwa bila kujua tafsiri ya tulichokikariri.
Hiyo ndiyo changamoto wanayokutana nayo watoto waliotoka St. Kayumba. Na sijui kama hiyo changamoto itakaa ipatiwe ufumbuzi. Itapatiwaje ikiwa watoto wa watunga sera na wafanya maamuzi wanasoma kwenye shule zenye hadhi ya shule?
Pole ni kwa wale wasioweza kuwapeleka watoto wao shule za English medium.
Lakini kwa nini Serikali imeamua kuweka ubaguzi mkubwa kama huo? Naamini, kama shule zote nchini zingetumia "English" tokea chekechea hadi Chuo Kikuu, hali ingekuwa hivi:
1. Watoto wangejizoesha kusoma kwa kuelewa badala ya kukariri kama kunavyofanywa Sasa na wanafunzi wengi wa Sekondari
2. Viongozi wa Serikali na vigogo wengine wangehamasika kuwapeleka watoto wao shule za Serikali
3. Taifa lingejipatia wasomi wake wanaojiamini hata katika ngazi ya Kimataifa
4. Idadi ya Watanzania wanaofanya kazi na biashara Mataifa mbalimbali ingekuwa kubwa zaidi
5. Wakenya wansingewazodoa Watanzania na viongozi wao kuwa hawajui lugha ya Malkia.
Hivi Serikali haioni faida zote hizo? Inataka hizo fursa ziendelee kuwanufaisha watoto wa vigogo peke yao?