JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Serikali imethibitisha kutopokea taarifa rasmi ya utafiti unaoonesha wafugaji wa kuku wanatumia dawa za antibayotiki na hivyo kiasi kikubwa cha dawa hizo kuonekana kwenye maini, kisha kuwa na madhara kwa watumiaji wa kitoweo hicho kwa kusababisha usugu wa vimelea vya dawa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki kwenye mahojiano maalum amethibitisha hilo na kusema amewaelekeza wataalam kutoka wizarani kuipata taarifa hiyo na kuifanyiakazi ili kuwaepusha watumiaji na madhara.
Chanzo: Azam TV
Kuhusu Utafiti soma: Utafiti: Kuku wa kisasa kwenye Manispaa za Ilala na Kinondoni wana kiwango kikubwa cha dawa za kuua Bakteria