Serikali: Hospitali ya Muhimbili kujengwa upya, itawekewa miundombinu ya kisasa

Serikali: Hospitali ya Muhimbili kujengwa upya, itawekewa miundombinu ya kisasa

Labda mimi sielewi maana ya kujenga upya ina maana yale majengo yanabomolewa pale muhimbiri? Kwa tunaokwenda muhimbili mara kwa mara tunaweza kukubaliana kuwa hichi anachisema Waziri hakina msingi kabisa maana kama ni muhimbili basi majengo baadhi yanahitaji ukarabati tuu na unadhifu tuu lakini sio kujengwa upya...huu ni uropokaji tuu wa waziri! Kuna maeneo mengi hayana hospitali zikajengwe na muhimbili iboreshewe vifaa tiba na madawa !
Pesa ikikaa sehemu moja ni rahisi kuipiga kuliko ukiitawanya walaji watakuwa wengi, ndiyo maana dikteta kila kitu alikuwa anaficha jeshini
 
alikuwa anamainisha kuwa tayari dar kuna hospitali ya mlonganzila hivyo pesa hiyo ipelekwe mikoani ili wagonjwa wa kutoka huko wapunguziwe adha na gharama za kuja dar.kodi hazilipwi na wakazi wa dar pekee yake hivyo wananchi wote wanastahili huduma sawa.
Bora ingejengwa hata Mwanza au Arusha ama Dodoma
 
Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema hospitali ya Muhimbili imejengwa miaka 60 iliyopita na miundombinu yake imeelemewa kabisa.

Hivyo serikali itajenga miundombinu mipya na ya kisasa kabisa itakayokidhi mahitaji ya miaka 50 ijayo itakayojikita kwenye Ubingwa na Ubobezi.

Chanzo: Muhimbili blog
Hii nchi ya kiboya sana !
 
Naona inefaa wangeimarisha zile za kanda, mzigo wa Muhimbili ungepungua sana. Mfano kanda ya Mbeya, Mwanza, Dodoma, Moshi na Mtwara ziwe na viwezeshi vyote, inepunguza watu kwenda Muhimbili. Ili Muhimbili iwe ya kimataifa boresheni hizi za kanda. Kelele za waziri zinafanya hata wanaotaka kuja kutibiwa kuogopa.
 
Kweli inahitaji kuboreshwa ila zinahitajika Hospitali hata mbili kubwa zingine badala ya kutumia billions kwenye hospitali moja
Watu wameongezeka tangu miaka ya 60 kwa hiyo tuongeze vyuo na hospitali pia
 
Ummy rudisha Mloganzila MUHAS utaona mabadiliko ya uwezo wa madactari chini kuliko.Watakuja external lecturers watatubadili kitaaluma.Tatizo siyo kuboresha.Tatizo ni uduni wa taaluma.
 
Hivi waziri anaposema kuwa hospitali itawekea miundo mipya hapa huwa amekusudia nini hasa? kinachonishangaza ni kuwa anasema itaweka miundo mbinu itakayoweza kukidhi mahitaji ya miaka 50. Hapa nipo nakuna kichwa kufahamu hasa alichosema na kukusudia! Naomba kuelimishwa.
 
Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema hospitali ya Muhimbili imejengwa miaka 60 iliyopita na miundombinu yake imeelemewa kabisa.

Hivyo serikali itajenga miundombinu mipya na ya kisasa kabisa itakayokidhi mahitaji ya miaka 50 ijayo itakayojikita kwenye Ubingwa na Ubobezi.

Chanzo: Muhimbili blog

Ni bora wangejenga hospitali mpya maeneo mengine labda uelekeo wa Mbagala, Tegeta au Pugu...ingesaidiana na ile ya Mloganzila na hiyo ya Muhimbili sasa
 
Sio kweli, hapo kustand ya kwenda dar na stand ya mikoani, jiulize hapo kwenu asubh bus nying zinaenda wapi? Dar au koromije?
Nyingi zinaenda mikoa jirani kwa mfano mwanza tabora shy bukoba basi za musoma dar ni moja tu tena ni JM
 
Mkirekebisha miundo mbinu, msisahau kurekebisha rushwa! Maana hapo ufikiri kuna kozi ya ubingwa kuhusu rushwa!
 
Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema hospitali ya Muhimbili imejengwa miaka 60 iliyopita na miundombinu yake imeelemewa kabisa.

Hivyo serikali itajenga miundombinu mipya na ya kisasa kabisa itakayokidhi mahitaji ya miaka 50 ijayo itakayojikita kwenye Ubingwa na Ubobezi.

Chanzo: Muhimbili blog
Inashangaza na kusikitisha sana kuona kuwa hawa mawaziri bado akili zao ziko Dar hadi miaka 50 ijayo!
Serikali inapaswa kujenga hospitali mpya kabisa na ya kisasa kabisa ya viwango vya kimataifa yenye huduma zote za kibobezi huko makao makuu ya nchi (Dodoma). Hiyo ndiyo itakuwa hospitali ya Taifa na itafikika na wengi kwa urahisi kwani Dodoma ni katikati ya nchi. Hilo li Muhimbili waachane nalo, libaki kama Dar es Salaam Regional Referal Hospital. Pia majeshi yetu yajenge hospitali ya kisasa ya kijeshi ya viwango vya kimataifa yenye huduma zote za kibobezi huko Dodoma. Hiyo ya Lugalo ibaki kama ilivyo kwa walio Dar au jirani na Dar kwa huduma za kawaida.
 
Nooooo, kuna Mikoa zaidi ya 25, Wilaya kibao hazina Hospitali, watu wanasafiri kutoka Mikoani kuja Muhimbili, hiyo fedha igawanywe ipelekwe Mikoani.

Dar tayari kuna hata Mloganzila haiko mbali.

Kajengeni Mikoani pia!
Ummy anatafuta pa kupiga hela...
Hospitali ya Muhimbili haipaswi kuwepo pale ilipo. Madhara yake ni makubwa sana kwa jamii ya Dar.
 
Doh, inajengwa sehemu gani tena pale? Tungejenga “Muhimbili” nyingine nje ya Dar es Salaam.
 
Unaita wivu? Kwa hiyo unaona ni sawa watu wa Mikoani kuja kutibiwa Muhimbili badala ya kujengewa Hospitali pia huko ?

Kweli Viongozi ni taswira ya watu wanaowaongoza!
Kuna hospitali tumejenga Chato. Wengine waende kule
 
Sisi wenyewe tulioko huku musoma ,tukisema" twende stend ya kwenda mikoani" ,tunamaanisha na dar ikiwemo. So dar nako ni mikoani tuu.
Basi pandeni basi muje Muhimbili. Karibuni sana
 
Back
Top Bottom